Clatous Chama angeshafukuzwa siku nyingi kama isingekuwa Yanga

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,342
4,801
Kwa muda mrefu timu ya Simba imekuwa inavutana na mchezaji wake clatous Chama lakini imeshindwa kumfukuza kutokana na jinsi media zimekuwa zikivumisha kuwa mchezaji huyo anahitajiwa na klabu ya Yanga. Simba imekuwa ikipiga mikwala mizito isiyo na athari. Ninavyoamini mimi ni kwamba kusingekuwa na promo ya kumuhusisha na Yanga hakika leo hii angeshafukuzwa.

Na watu wameendeleza kukoleza hizo Drama kwenye social media hasa pale chama anapokuwa kwenye mgogoro na timu yake hali inayoifanya Simba kuwa wanyonge/kushindwa kuchukuwa maamuzi magumu dhidi ya Chama.

Chama una kila sababu ya kushukuru hizi Drama za media. Maana Simba inaposikia eti Chamba anahitajiwa na Yanga inapata KIHARUSI.
 
Wakati mwingine ili kumkomesha Mwanamke mzuri na Mrembo ambaye ni mapepe ni kuhakikisha anazeeekea kwako aidha kwa kumbana sana ama kumzalisha fasta fast ili Wana wakipita naye wakute ashachoka.
Mourinyo aliwahi kusema, wakati mwingine baki na mchezaj hata kama humpendi ili mradi asiende kwa Adui.
 
Back
Top Bottom