Kwa heshima naombeni mpigie Kura Malisa GJ amekuwa mchango mkubwa sana kwa Jamii katika kugusa maisha ya Watanzania

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Comrade Malisa GJ.

Rafiki yangu mmoja kanitumia ujumbe "Malisa mbona huombi kura?" Ikabidi nimpigie kumuuliza kura za nini? Akaniambia za tuzo. Nikamuuliza tuzo zipi? Akaniambia umependekezwa kwenye tuzo ziitwazo Tanzania Inspiration Awards. Nikamwambia sina taarifa.

Akanitumia "link" nikapitia na kuona kweli nimependekezwa kwenye kipengele cha "Charity and Services" yani mtu anayefanya kazi za kujitolea na shughuli za kugusa jamii.

Nawashukuru wote mliopiga kura za kunipendekeza kwenye tuzo hizo bila hata mimi kujua. Basi nawaomba mnipigie kura niweze kushinda, nisiishie kwenye mapendekezo tu. 🤣

Jinsi ya kupiga kura bonyeza link hii TANZANIA INSPIRATION AWARDS 2020 kisha tafuta kipengele kilichoandikwa "Charity and Service" hapo outaona orodha ya majina kadhaa. Bonyeza kitufe kilichopo pembeni ya jina langu, kisha shuka chini kabisa utaona maneno "Wasilisha" bonyeza hapo. Utakua tayari umenipigia kura.

Asanteni na Mungu awabariki!

 
Umetumia maneno makali, ila hoja yako ni fikirishi..

Binafsi ninaunga sana Mkono Jitihada za Malisa kuisaidia Jamii. Ila alianza kunipa mashaka alipoanzisha utaratibu Wa Kuwatangazia Biashara watoa michango. Siyo vibaya (pia ana Uhuru huo); ila inaleta taswira ya kujionesha na kujitangaza zaidi kuliko kusaidia kidhati.

Kwa imani yangu MTU anayetoa msaada na akapenda ijulikane kuwa amesaidia, basi msaada wake ni kazi bure mbele za Mungu.
 
eti kwenye media personality yupo Pascal Mayala anapambanishwa na Maxence Mello 🤣 🤣 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…