Kwa heri mpenzi

MR NDEE

Member
Aug 2, 2011
54
21
Utunzi huu ulikikuwa maalumu kwa kidato cha nne shule ya sekondari Mtombozi iliyoko mkoani Morogoro. nimejaribu kufuata nyayo za Mabala Richard, sina hakika kama nimeweza kufata nyayo zake, majaji ni wasomaji
 

Attachments

  • KWAHERI MPENZI.docx
    18.7 KB · Views: 179
KWAHERIMPENZI

Kwakompenzi mASOMO


Sinabudi kusema kutoka moyoni kuwa ninakupenda kwa maisha yangu yote.Siwezi kusahau mahaba mazito uliyonipa na kunionesha. Neno pekeeninaloweza kusema ni kuwa NAKUPENDATOKA KATIKA SAKAFU YA MOYO. Nakumbuka sana MAPENZIYAKO, natambuakuwa, kila mwaka unaoa, na fauka ya hayo, kila mwaka unatoa talaka,nakumbuka talaka ya mwaka jana iliacha majonzi kwa wakezo wote ilawawili, uliwapa talaka lakini waliondoka wakiwa na mali nyingi nawalipata waume wanaowapenda zaidi.


Nakumbukamiaka minne iliyopita, nakumbuka sana, nakumbuka pete uliyonivikasiku ya Jumatatu, Ulinipokea kwa bashasha na furaha tele, hakikanilijisemea “MWANAUMENDIO WEWE”. mpenzi,uliniambia utaishi nami kwa furaha na amani kwa miaka minne, ndani yamaisha yetu ya ndoa uliniruhusu nichote madini ya aina mbalimbali,kuanzia lulu, redilaiti, tanzanaiti, almasi na hata dhahaba,uliniambia hati ya makabidhiano yataandikwa kwa wino wa dhahabuilinitajwe milele na milele katika vijiji vya Nemere, Lusangalala,Kisanzara na hata mjini Mtombozi.


Mpenzi,kwanini uliweka ukuta tulipofika miaka miwili? Ulidhamiria kuwa uavipenzi vyangu kwa presha? Nakumbuka sana ulitaliki wenzangu, wengineuliwatandika mijeledi wakaenda kusimulia mitaani.


Ilampenzi, sikulaumu kwa wale walijitaliki kwa kujijaza matumbo makubwa, yale matumbo yanayopungua baada ya siku tisa. Sikulaumu katu.Sitakulaumu abadani, uliwapa taa ya hatari, kinyume chake, waowalipenda na kuuthamini UJINGA,walipenda kupika SUFURIALAMAJUNGU,eti kusoma BONGOO? Mpenziunajua sasa wanaishi katika sayari gani? Mh! Ama kweli majuto nimjukuu na sasa wabweka bweeebweee,na wengine mikono kichwani wanatoa kamasi puani na mdomoniwanabwabwaja mhh mhh mamaa weee ni SHIIIDAAH,unasemawalikuwa wanasema KAN’TANGAZE?Basi,sasa wanachapa lapa LAP,LAP,wakiona watu wana jificha katika migomba na mishelisheli.


Bebii,usione kuwa nawakebehi na kuwacheka, La hasha! Najuwa watambua nikokitandani, ninaumwa, maleria si malaria, sijui usubi! Kichwa sikichwa, ila sijielewi, mila nazo sizisadiki, wamekuja wamanyanga natunguli nimewakimbiza. Wamekuja wakalamu nimewakubali, wameninasihikuwa mimi ni SHUJAAwa nafsi yangu. Wamenieleza ya kwamba, juhudi ndio msingi wamafanikio.


Mpenzi,naona nisikuchoshe kwa ngonjera na riwaya, zangu, nakuaga mpenziwangu, sijui nitakapoelekea, sijui kama nimekaa kwako kwa muda wotekuchakaza sofana soli,sijui kama nitakwenda kwa mume mwingine kwa miaka miwili, sijuikabisa, ila nina matumaini, na iwapo nitafanikiwa nitasema AMINA.


Mpenzimafanikio ya mume yamebebwa na mke, na mafanikio ya binadamuyanatokana na REHEMAza MUNGU,acha sasa nimuombe katika nyakati hizi ngumu maana MUNGUNI MWEMA.


“ EeMungu Mwenye kiti cha Enzi uliye mbinguni, uliyenyanyua mbingu nakuitandika ardhi, uliyemuumba Adamu na Hawa,uliyefunikaULIMWENGUkwamapenzi na mahaba, hakika u mwema na unayewapenda waja wako.

EeeMwenyezi Mungu, nakuomba uniondoshe majaribu na mateso haya, nakuombauniondoshe mnyororo wa shida na dhiki zaMDUDUhuyu,MduduhuyuanaitwaNEKITAeehMungu sitarudisha fadhila zaidi yakukupendanaKUKUTUKUZA,EeeMwenyezi Mungu asante kwaKUPOKEAmaombiyangu.”

AMINA
KWAHERI MPENZI BIN SHULE


IMEANDALIWANA
MWL.NDEE
 
Utunzi huu ulikikuwa maalumu kwa kidato cha nne shule ya sekondari Mtombozi iliyoko mkoani Morogoro. nimejaribu kufuata nyayo za Mabala Richard, sina hakika kama nimeweza kufata nyayo zake, majaji ni wasomaji

Nimependa, iko sawa kwa nafasi yake!
 
Back
Top Bottom