Kwa heri c.c.m udom

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
KUTOKA NDANI YA CHUO KIKUU CHA DODOMA-(UDOM) Taarifa za ndani ya Chuo hicho zinasema kuwa Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi Unakabidhiwa kwa Vijana wa Kazi-CHADEMA baada ya mipango ya kuwaengua wanachama wa CHADEMA Kugonga mwamba. Duru ya kwanza ya uchaguzi ilimalizika hapo jana tar 30/05/2012 baada ya vijana wa kazi kuchukua nafasi nyingi za ubunge mpaka ma-block leader. Muda mfupi ujao nafasi za U-rais, makamo wa rais na marais katika ngazi za vyuo yatatangazwa ambapo dalili zaonyesha wazi kuwa C.C.M waliopandikiza vijana wao sasa wanapumulia mashine. C.C.M kwa heri UDOM!


Tayari matokeo yametangazwa. Vidole viwili hewani
 
Inapendeza,lakini ni vizuri tupata matokeo rasmi maana usje kusikia tayari yamechakachuliwa.
 
Someni watoto, wanaowatumia wamesoma!

Nani alikudanganya kwamba chuo ni kwaajili ya kukodolea macho maandishi meusi peke yake! A proactive student is one who is inspired for application of knowledge acquired through reading and acting.

Msisikilize ushauri wawakukariri...kwanza walipita chuo lakini chuo hakikupita ndani ya vichwa vyao....
 
Hongeren japo sio vizur kugombea vioni kwa itikad ya vyama! Pale ni katba ya wanafunzi ndo inayoprevail na sio chama! So sikubliana na wanafunz kua na mtizamo wa kivyama vya siasa wakat wanawatafta viongz!
 
Eeh sasa na mkue muache mchezo wa kuahidiwa wali na ccm katika mikesha ya ccm mkaenda na kukesha uko uku mkiumwa na mbu wakati gharama ya kuununua wali ni ndogo sana ukilinganisha na malaria mnayokuja kupata
 
TAARIFA ILIYOTOKA SI YA KWELI
ccm udom inasonga mbele na kwa taarifa yako wagombea wote wa uraisi ni ccm kwanzia federation mpka collage level
 
KUTOKA NDANI YA CHUO KIKUU CHA DODOMA-(UDOM) Taarifa za ndani ya Chuo hicho zinasema kuwa Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi Unakabidhiwa kwa Vijana wa Kazi-CHADEMA baada ya mipango ya kuwaengua wanachama wa CHADEMA Kugonga mwamba. Duru ya kwanza ya uchaguzi ilimalizika hapo jana tar 30/06/2012 baada ya vijana wa kazi kuchukua nafasi nyingi za ubunge mpaka ma-block leader. Muda mfupi ujao nafasi za U-rais, makamo wa rais na marais katika ngazi za vyuo yatatangazwa ambapo dalili zaonyesha wazi kuwa C.C.M waliopandikiza vijana wao sasa wanapumulia mashine. C.C.M kwa heri UDOM!​

Ili kuweka kumbukumbu sawa badili tarehe kwenye maelezo yako iwe 30.5.2012
 
Kutokana na unyeti wa ukombozi uliopo hapo mbele yetu nawasihi wanavyuo wote mtuunge mkono kadri muwezavyo na msikubali kutumiwa na ccm kwa kuswombwa kwenda kwenye sherehe zao.msome ila lazma mshiriki ktk ukombozi,viva udom
 
Back
Top Bottom