TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Kwa haya, Utaifa wa chadema una walakini
!
Baada ya yote yanayotokea naomba turudi kuzungumzia maadili ya utaifa. Kwa maana ya utaifa kama msingi na alama ya uwepo wetu kama WATANZANIA, bila ya watanzania kuwa na maadili ya utaifa hakuna Maendeleo ama mabadiliko ambayo yatakuwa na maana.
Maadili ya utaifa yana maana kubwa sana kwa kila mtanzania, tujivunie utaifa wetu na tupende kutambulika kwa utaifa wetu.
Lakini maadili ya Taifa pia ni kutojiona bora kuliko wengine, kutokuwa mbinafsi kwa kujijali mwenyewe ama kikundi chako ama taasisi yako ama chama chako na badala yake kufanya kila jambo huku ukijali na kuweka mbele maslahi ya taifa. Tukianzia hapo, tutapata viongozi ama utawala unaojali zaidi maslahi ya taifa.
Tarehe 26/04/ ni siku ya muungano, muungano ni moja ya nembo muhimu kama Taifa, lakini pia ni ishara ya uwepo wa Taifa liitwalo Tanzania kwani Taifa hilo linatokana na maamuzi ya busara yaliyofanywa na waasisi wa muungano huo. Lakini pia ni elimu, historia na kumbukumbu kwa watoto na kizazi cha sasa kuwa kulikuwapo na matukio muhimu ya namna hii ambayo yalikuwa ni asili ya umoja wetu na utaifa wetu.
Kitendo cha viongozi waandamizi wa chadema kutohudhuria katika sherehe hizi kumeacha maswali na mkanganyiko mkubwa katika vichwa vya watanzania juu ya misimamo na itikadi za viongozi wa chama hiki kikuu cha upinzani hivi sasa.
Labda niseme kuwa, ni vyema kwa watanzania, wanaharakati na yeyote aliye katika ari ya kuona mustakibali mwema wa nchi hii akatambua kuwa tunahitaji kuheshimu na kufuata maadili ya taifa na kusimamia utaifa wetu.
Ni kweli kuwa tunahitaji mabadiliko katika Nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, siasa na hata mabadiliko katika mienendo ya jamii yetu ila kwa hili la kudharau misingi ya umoja wetu na utaifa si jambo jema na wala hatuhitaji kufanya mabadiliko kwenye misingi ya utaifa wetu.

- Je, kwa kitendo hiki wanataka watanzania waamini kuwa wao hawana haja ya muungano na kwa maana hiyo muungano kwao sio kitu cha msingi kuadhimishwa
- Ama hii ndiyo maana ya falsafa ya upinzani kuwa unapinga kila kitu kilichoasisiwa na viongozi wa chama tawala na serikali ( hata yale yanayowakilisha utaifa wetu)
- Lakini tafsiri ya kuwepo kwa viongozi wengine wa vyama vya siasa (ccm, cuf, tlp,udp, cck n.k) na kukosekana kwao wao pekee ni ishara kuwa wao ni bora kuliko hawa wengine wote..?
- Lakini kama hayo hayatoshi, viongozi hawa wananafasi gani katika matukio kama haya kulingana na falsafa ya wajibu wa raia citizens obligation to nation ni kweli wanayo nafasi ya kufanya dharau hii..?
- Haya pamoja na mengine mengi ikiwemo kauli ambayo mpaka leo haijawahi kukanushwa ya mmoja wa vongozi waandamizi wa chadema kuwa hatahakikisha kuwa nchi hii HAITAWALIKI vina nafasi gani katika dhana ya UTAIFA wetu.