Kwa hali hii warembo wa tanzania watafika popote?

Mchomvu

New Member
Mar 17, 2009
1
0
Ni miaka 16 sasa tangu Tanzania ianze tena kuendesha mashindano ya urembo tangu yalipofunguliwa tena mwaka 1994. Lakini mara nyingi watu wamekua wakijiuliza kwanini Tanzania haifanyi vizuri katika anga za kimataifa? Mara nyingi warembo wamekua wakichaguliwa kwa mbwembwe nyingi huku tukisikia tambo kutoka kwa wadau mbalil mbali kua mara hii lazima watafanya vizuri lakini hizo zimebaki kua ni hadithi tu na ndoto za mchana warembo hawa wamekua wakienda ktk mashindano ya dunia na kurudi kimya kimya huku kukiwa hakuna chochote walichoambulia. Ukiacha Nancy Sumary ambae alikua ni miss Tz mwaka 2005/2006 na akafanikiwa angalau kuingia nusu fainali na hatimae kua miss world Africa wengine wamekua kama wanaenda kutalii tuu.Kilichonisukuma kuandika ujumbe huu ni kile nilichokiona jana ktk mashindano ya kumsaka "the so called" mrembo wa TZ, hususani kipindi kile cha maswali na majibu, hivi kwa hali ile nilioiona pale tuna sababu yoyote ya kutafuta mchawi? Hivi kweli yale maswali waliokua wanaulizwa ni maswali ya kumshinda mtu yoyote mwenye uwezo wa kufikiri vizuri? Binafsi sikuona swali gumu pale ila nimesikitishwa sana na jinsi ambavyo wadada wale walivyokua wakijibu maswali, lakusikitisha zaidi wengine walichagua lugha ya kiingereza huku wakijua hawaifahamu vizuri kitu kilichowafanya washindwe kujieleza vizuri. Lakini alienishangza zaidi ni yule alieulizwa kua ni kiongozi wa aina gani angependa awe rais wa nchi hii kwakweli majibu aliotoa ni aibu tupu, swali kama lile hata mtoto wa kidato cha pili alie makini angeweza kulijibu kwa ufasaha zaidi. Nashukuru kua majaji waliliona hilo na matokeo yake hakuingia hata nafasi ya 3 naamini hili ndilo hasa ilimwangusha kwani kwa mtizamo wangu sifa zingine alikua nazo! Ni aibu tupu warembo wetu, kinachoshangaza miongoni mwao wapo ambao wapo katk vyuo vikuu, hebu tujiulize huko wanasoma nini? Kwa hali hii hatuoni kua tutaendelea kua wasindikizaji ktk mashndano ya miss world? Huo ni mtizamo wangu tu wadau, msijenge chuki..

Mdau, kutoka Mbeya.
 
Karibu sana katika Forum hii Mchomvu!
Yote uliyoongea hapo juu ni ukweli mtupu, sijui tufanye vipi ili tuweze kufanikiwa!
 
Elimu ya kutatanisha waliyonayo warembo wetu inaakisi mporomoko wa elimu kitaifa kwa ujumla, na hasa katika shule serikali. Tunahitaji serikali itakayoleta mageuzi makubwa katika quality ya elimu - na si kushupalia uwingi wa wanafunzi tu.
 
sasa kama wenye uwezo wa kielimu hawashiriki, iweje? inabidi tu wachaguliwe tu hao hao vilaza.
 
Mimi nauliza swali moja tu.

Mashindano haya ya Miss Tanzania YANATOA MCHANGO GANI KWA UTAMADUNI WA MTANZANIA? Jibuni hili. Mkiweza, mtakuwa mmepata UHALALI wa kuwapo kwa mashindano haya.

Sijasikia Wamarekani wakiendesha mashindano ya Miss Afrika!
 
kwa vile vivazi kuna utamaduni hapo MwanaHaki? i dont think so! kuhusu lugha naona wawe wanawauliza kwa lugha za makabila yao maana kiswahili na kingereza zote ni problem.

kwenye hizo top10 nahisi ndo wanakokosea, wanachaguaga mbovu? halafu top 10 hiyo hapo2 wanapata top5 kwa vigezo gani, ushapata top10 wapambanishe hao ndo upate top5!
 
Back
Top Bottom