Kwa hali hii nini hatima ya ahadi za JK?


Konakali

Konakali

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
1,507
Likes
76
Points
145
Konakali

Konakali

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
1,507 76 145
Wamarekani wameamua kuiangusha serikali za mitaa za Chama cha Obama, na wanaahidi Obama kutorudi madarakani kwa sababu ameshindwa kuwatimizia alivyowaahidi...! Iwapo watanzania tumemchagua JK kwa ahadi zake alizoahidiwa naye na Obama, na sasa Obama yupo mbioni kuondoka madarakani, hatima ya ahadi za JK ni nini? Mimi ningeomba uchaguzi wa Tanzania urudiwe kwa sababu hali tulioitegemea inabadilika...!
 
C

chanai

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Messages
279
Likes
0
Points
0
C

chanai

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2010
279 0 0
Ndugu yangu,
Tumekuwa tukipiga kelele kuwa hutuwezi kuondoa umaskini katika nchi hii kwa kutegemea misaada kutoka nje. Kama Dr Slaa alivyokuwa anaweka wazi, japo misaada itaendelea kuhitajika katika kufanikisha miradi mikubwa, tunahitaji kuwa na mikakati ya kuinua uchumi wetu wenyewe. Tanzania ina rasilimali nyingi sana ambazo kama zingetumiwa vizuri tungeweza kabisha kupiga hatua nzuri ya maendeleo na kupunguza umasikini uliokithiri. Kuna vyanzo vingi vya mapato vinapotea na nchi haifaidiki. Pia matumizi mabaya ya mali za umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi hii.

Inasikitisha sana kuona wakuu wetu wanabweteka na mikopo na misaada hata katika mambo ambayo tungeweza kuyafanya wenyewe. Nimekuwa nikisema mara nyingi kuwa huwezi kuwa na familia na unategemea jirani yako ndiye ahudumie. Unapoamua kuingia katika majukumu ya kifamilia ni lazima uwe na mikakati ya kujua jinsi gani utahudumia familia yako.

Leo hii tunategemea kupewa vitabu vya watoto wetu kutoka marekani. It is really an embarrassment. Kweli watanzania hatuwezi kuandaa na kuchapa vitabu vya sayansi hadi tutegemee misaada kutoka marekani?

Utashangaa raisi anahaidi eti ataleta wataalam wa kilimo cha nyanya kutoka Israel. Hii ni aibu kubwa sana. Inamaana Tanzania haina wataalam hata wa kuweza kuboresha kilimo cha nyanya? Kama ni hivyo, kwa nini Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) kisifutwe? Kina kazi gani?
 

Forum statistics

Threads 1,236,300
Members 475,050
Posts 29,253,365