MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Ofisini, Daladala,Magengeni,Vituo vya magazeti,vituo vya daladala, stands za magari,kahawa,mahotelin, vyuoni LOWASSA ndio stori.Ni kila mtu kura yake ni kwa LOWASSA! Ni kama utani vile, kwa hakika LOWASSA ndiye Rais ajaye.
Ifike mahala tuweke ushabiki pembeni kiukweli Lowassa ameteka stori kila kona ya nchi japo kuna baadhi ya vyombo vya habari vinajitahidi kwa nguvu kuukwepa ukweli wake, vimejivika miwani za mbao kwa makusudi.Vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli kuhusu hili visubiri aibu ambayo havitaisahau maisha yao yote.
Mimi najiuliza ipi itakayoifanya CCM ishinde Uchaguzi ujao! Hili liko wazi na dunia nzima inatazama.Kutoa tathmini ya ushindi wa Uchaguzi kupitia wingi wa watu kwenye kampeni ni kiashiria cha kushindwa vibaya sana, Kwanini usitoe tathmini ya ushindi kupitia hata takwimu ambazo zinazotolewa kupitia mitandao mbali mbali ambayo ya kijamii inaendeshwa hata na baadhi ya watu wasioegemea upande wowote wa siasa?
Binafsi nafikiri kwa sasa ni wakati wa CCM kujaribu kutafuta ukaribu na UKAWA kuishi kama ndugu kama kweli wao wanaifikiria na kuitathmini kesho yao kuliko kuendeleza chuki,fitina na uhasama kama ilivyo hivi sasa. Hakuna miujiza wa CCM kushinda Uchaguzi mkuu ujao na dalili ziko wazi wazi.
Najaribu kufikiria matumizi ya vyombo vya dola wanaojaribu kuvitumia hivi sasa ni kutofikiria kwamba hivi vyombo ni vya watanzania wote,ndio kazi ya vyombo vya Doda ni kutii amri za watawala lakini nasisitiza ifike mahali na watii amri kwa kuzingatia matakwa ya viapo vyao vya kazi. Itazame nchi kubwa yenye majeshi makubwa na yenye nguvu dunia nzima, pia yeye kutumia teknolojia ya hali ya juu lakini huwezi kusikia vinatumia na chama flani hata iweje! Chezeni mjuavyo, tukananeni mwezavyo lakini walinzi wa wananchi wako makini kwa Taifa lao, hawana ubaguzi.Na ndio maana marekani huwezi kukuta chama kimoja kikadumu kwenye utawala zaidi ya awamu mbili.
Vyombo vyetu vya dola tunaviomba vinapotii tii amri za watawala vizingatie viapo vyao na sio maslahi ya watawala, Tanzania ni yetu sote.