Kwa hali hii kampuni za antivirus zishirikiane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hali hii kampuni za antivirus zishirikiane

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Dec 27, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Unakumbuka wakati ulikuwa unahitaji antivirus kwa ajili ya kutafuta virus ndani ya komputa ikishawapata itawaondoa kwa kuwafuta na pengine kufuta files ambazo zimeathirika na virus hao ? huo ulikuwa ni wakati wa kale kidogo kwa sasa mambo ni tofauti .

  Kwa miaka 20 iliyopita watu wengi zaidi wamepata nafasi ya kutumia vifaa vya mawasiliano kama komputa na simu na aina zingine za mawasiliano hii ikalazimisha kampuni nyingi za ulinzi wa mitandao kuja na bidhaa za kupambana na uhalifu wa mitandao ndio hapo tukaanza kusikia Internet Security

  Sasa kuna matishio kama spyware ambazo ni programu zinazoingia kwenye komputa kwa ajili ya kutafuta taarifa na kumtumia Yule anayehitaji au kulazimisha komputa yako na programu zake zifuate kile ambacho programu hiyo inataka kama kukupeleka kwenye tovuti fulani kwa lazima , wakati huo kupambana na spyware ulihitaji antispyware ambapo antispyware bora uliyokwepo mpaka sasa hivi ni adaware

  Kuna keylogger ambazo ni programu zinazoweza kuhifadhi yale yote unayofanya kutumia keyboard ya komputa yako , kuna nyingine zinauwezo wa kuhifadhi jinsi unavyozungusha mouse ya kompyuta husika na vile unavyobonyeza au unavyofanya mabadiliko Fulani kwenye komputa hizo zamani kidogo vilikuwa ni vifaa vinavyofungwa kwenye komputa sasa imekuja kwenye programu .

  Hata firewalls ambazo ni ukuta kati ya komputa na mitandao mengine duniani , firewalls zimekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya watu haswa wale wasiojua wanafanya nini kwa kulazimika kuruhusu vitu wasivyovijua au kutokuwa na taarifa nazo za kutosha .

  Pamoja na hayo yote kuna Malware ambayo ni aina ya programu inayotengenezwa kwa ajili ya kuharibu utaratibu wa ufanyaji kazi wa komputa bila ya mtumiaji wa kompuya hiyo kujua tofauti na virus ambapo inaweza kuishi ndani ya komputa bila kuharibu kitu malware inauwezo wa kufanya uharibifu .

  Ukaja wakati ambapo kampuni zinazotengeneza antivirus zikalazimika kubadilika kutoka kwenye programu inayofanya kazi moja peke yake yaani kupambana na virus tu , ikabidi sasa antivirus hizo kuunganisha programu zingine ambazo zingeweza kupambana na matishio mengine yanayoendelea haswa kwenye mitandao kwa njia ya mtandao .

  Hapo ndipo tulipokuja kuona viongezeo mbalimbali kwenye programu nyingi za antivirus mfano kwenye mcafee kukawa na kiongezeo cha Advisor , Avg kuna Link Scanner , Symantec pamoja na Norton kuna viongezeo vipya kwa ajili ya matishio mengine ya usalama wa komputa na watumiaji wake kwa ujumla .

  Pamoja na viongezeo vyote hivyo hali imezidi kuwa tete mpaka sasa hivi kwa saba
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wapo kibiashara zaidi.kila kampuni inataka kuvuta wateja kwake. Nina wasiwasi kuwa wanaotengeneza antivirus ndio haohao wanatengeneza virusi.

  NB: Njia za zamani za kuhifadhi kumbukumbu ni bora zaidi kuliko hizi za kisasa.
   
 3. jngowi

  jngowi Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Thanx for your valuable information
   
 4. Bill of Quantity

  Bill of Quantity JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 1,250
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Thanks...
   
 5. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2015
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Asante kwa post walau nimejua termilogies..malware, firewalls etc. but nadhani ulikuwa unaendelea kuandika vile....
   
Loading...