Kwa hali hii, Je mimi ni Genius??

Kwa hali hii, Je mimi ni Genius??

Hi members, nitaanza kwa kujitambulisha hapa chini kabla ya kwenda kwenye mada kamili.

Jina: Free ideas(Not official)
Umri:29yrs
Elimu:Shahada
Kabila:Kanda ya ziwa
Familia: Married with 2 kids


Kiufupi nimesoma 0-A level hapa Tanzania kisha nikaenda nje ya nchi(Europe) kuchukua Bachala.

Binafsi kuna hali inanitokea hua mpaka mwenyewe nashindwa kujielewa kama ni kwangu tu ama hata kwa watu wengine, lakini kila nikijaribu kumsimulia mtu kuhusu yanayonitokea hua ananishangaa na kuona kwamba mimi sio mtu wa kawaida.

Nitaeleza japo kwa ufupi hapa chini kuhusu hali hiyo.

1. Nikiwa bado nasoma(primary), sikuwahi kakaa n kujisomea iwe wakati wa mitihani ala la!, kuna wamwaka niliugua mapunye(mashilingi)kichwani nikakaa nyumbani miez 10 nikaenda shule baada ya kupona mwezi wa 11.Week iliyofuata kukawa na mitihani ya kufunga shule kuingia darasa la sita.

Nilifanya mtihani ule bila maadalizi yoyote na kuna walimu walitaka nisiwanye mtihani kwa sababu sikuwepo almost mwaka mzima.Nikalia sana wakaniacha nikafanya.Matokea yalipotoka nikawa mtu wa pili (2) kati ya watu mia moja thelethini na nane( 138.) Mwalimu mkuu aliniita akitak nimwambie kama nilipewa mtihani na mwalimu yeyote , lakini aligundua kwamba sikupewa mtihani.
.
.
2. Napenda sana kukaa mwenyewe na hua nikiwa mwenyewe najikuta naongeaongea na wakati mwingine kucheka mwenyewe.Pia mama yangu aliponizaa anasema kwanza hakusikia uchungu wa uzazi kabisa.Pia nilipozaliwa tu nilicheka badala ya kulia kama watoto wengine.Nikiwa na miaka 3 nikikua na uwezo wa kusoma bila kukosea.
.
.
3. Nikiota kitu ndotoni hua haipiti siku tatu kinatokea kweli.Mwezi ulopita niliota nimepata ajali ya kugongana na bajaji kisha nikaumia kichwani.Baada ya siku mbili nilipata ajali kweli na nikaumia kwenye paji la uso.Hata rangi ya bajaji niliyoota ilikua nyekundu na kweli bajaji ilikua nyekundu.
.
.
4. Nina uwezo wa kujua mgeni gani atanitembelea nyumbani kwangu na kweli mgeni huyo atakuja.Wakati mwingine mke wangu hua anaogopa ninapomwambia leo atakuja mgeni kavaa nguo flani na atakuja kwa shida flani.Nilitabili mama yake mzazi atakuja mwezi flani na akakuja na mtoto mdogo na watakua wamevaa hibi na kweli ikawa hivyo.
.
.
5. Kuna siku nilikua mahala nimekaa vichakani kama kawaida yangu kukaa mwenyewe, nikahisi kuna nyuka mweusi nyuma yangu katokea shimoni.Nilichofanya ni kuinuka taratibu kusonga mbele na kweli ile nageuka nakuta nyoka mweusi.
.
.
6. Mwaka mmoja kabla ya babu wa Loliondo nikiwa nje ya nchi nilimwambia jamaa yangu kwamba mwakani kuna mtu ataibuka maarufu kwa kusema anatibu ukimwi tanzania na atapata watu wengi.Kweli ikawa jamaa yangu mpaka leo anaamini mimi ni ndugu yake huyo babu na kwamba nilijua paln zake.
.
.
7. Nikiwa masomoni nje ya nchi sijawahi kukaa na kujisomea zaidi ya kuangalia movie za ki-Intelejensia na documentary za sayansi lakini hakuna mzungu hata mmoja amewahi kunipita darasani ama kwenye presentation, nimekua nikifanya vizur sana.Baadhi ya presentation zangu na machapisho yangu naskia zinatumiwa chuoni hapo na walimu.(lecturers)
.
.
8. Ninaweza kujua kwamba week ijayo nitaumwa na kulazwa kwa siku kadhaa.Pia naweza kujua nitaumwa ugonjwa gani ama malaria ngapi na hata nikipimwa hua ni kweli idadi ile ile.Mwezi ulipita nilimwambia wife nimewaza kua nitaumia mguu mlangoni, nakweli nikaumia mguu na mpaka sasa sijapona vizuri.
.
.
9. Ninauwezo mkubwa sana wa kutumia computer kufanya kazi.
Naweza kuchapa kwa kasi sana bila kukosea hata herufi moja.Naweza kutatua tatizo la computer lililowashinda mafundi japo sijasoma kabisa maswala ya computer.
.
.
11. Naweza kujua mawazo ya mtu hasa kabla hajaongea hata kama ni mara ha kwanza kuonana nae.Lakini pia naweza kujua kama mtu anasema uongo ama ukweli.Mke wangu akiniaga anakwenda sehemu hua najua anakwenda wapi na muda atakaorudi najua au kama kuna dharura atapata hua najua.
.
.
12. Ninaweza kuongea lugha tano za kimataifa(tofauti na kiswahili na kiingereza) kwa ufasaha lakini sijafanya kozi ya lugha hata moja kati ya hizo.Lugha hizo ni pamoja na kifaransa, kijerumani, kichina, kihispania, kihindi na kiarabu.Nimejifunza kupitia simu ya mkononi.
.
.
13. Sipendi kabisa habari za Dini na maswala yamuhusuyo mungu(mimi ni Atheist) na hua najickia vibaya sana kujadili maswala hayo.Ninaamini hakuna mungu.Pia sina ushabiki wa vitu vinavyopendwa na watu wengi mfano mpira ama siasa.
.
.
14. Napenda kukaa sana vijijini (japo kwa sasa niko mjini sababu ya kazi)na kufanya kazi huko, sipendi kuajiliwa na wala sifurahii kabisa kulipwa mshahara na mtu mwingine.Napenda pia kuzunguka zunguka sehemu zenye mito ama maji yanayotiririka na kuyaangalia huku nikijiongelea mwenyewe.
.
.
15. Kuna mwaka flani nilikua kijijini eneo la mto akili ikanituma niangalie juu ghafla kikashuka kitu kizito sana kutoka angani kama jiwe kubwa, baada ya kutua chini ghafla kitu kile kikageuka ndege mzuri na sijawahi kuona ndege wa aina kama ile tena mpaka leo.Ndege yule aliruka ruka kunizunguka kisha akapaa kurrudi angani vertically. Cha ajabu sikuogopa kabisa hali ile.
.
.
16. Tangu nizaliwe nimefanya mapenzi kwa mara ya kwanza nikiwa na mke wangu.I mean sikuwahi kufanya mapenzi hapo kabla sijaoa.Katika kipindi hicho chote sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke yaani kutamani kufanya sex.
.
.
17. Tangu niwe na akili timamu sijawahi kutoa chozi kwa maana ya kulia.Hata misibani nikienda hua naona ni hali ya kawaida na napenda sana kuishika maiti hasa kichwani.Wakati mwingine hua naomba nioshe maiti iliradi niishike kichwa tu kisha nami najishika kichwa halafu naondoka msibani.
.
.
18. Napenda harufu mbaya sana.Nikipita mahali kuna mzoga naweza kumaliza nusu saa hapo navuta harufu mpaka tumbo hua linajaa.Nikimuona mtu analia ama yuko kwenye huzuni mimi hua nafsi inafarijika na napenda kumwangalia huku natabasamu.
.
.
19. Sina hasira hata mtu akiniudhi namna gani.Hua nacheka na kutabasamu muda wote.Kuna baadhi ya ndugu wanadhani mimi ninamatatizo ya kiakili.
.
.
20. Nikiwa kazini hua ninatumia muda mwingi kufanya kazi za wafanyakazi wenzangu maana zangu hua namaliza kabla ya saa 3 asubuhi.Ofisini tunapangiwa kazi za siku husika hivyo mimi namaliza mapema hata kama kazi ngumu na kisha huwasaidia wengine karibu wote.Kufika sa sita kazi zote zimekwisha.Boss wangu hua ananipa majukumu hata yasiyo yangu (ya kwake)lakini nayafanya kwa haraka na kwa usahihi kabisa.
.
.
21. Sikuwahi kujifunza koz yoyote ya udereva lakini ninaendesha gari aina zote kwa ufasaha.Ninaweza kutumia mitambo mbali mbali hata kama ni mara ya kwanza kuuona.


Mwisho:

Hali hii inaniletea usumbufu sana kwa kua wengine wananitafrisi vibaya kutokana na tabia zangu.

Nimeleta hapa nipate ushauri wenu na kama kuna yeyote ambaye hali kama hii inamtokea nipate kujua kama ni tatizo ama ni kawaida.





.....Free ideas.......
Utakuwa jinimtu wewe..! Binafsi nilikuwa na akili za ajabu ingawa tunapishana mengi napenda Mungu kuliko maelezo ingawa huwa naanguka na kusimama immediately..!
 
tu prove kwanza,..., sema hapa nikikuwa nawaza nini wakati naandika hii comment..!!
 
Sasa ulienda shule kufanya nini?

Genius anasema hapendi kabisa kuajiriwa. Ila cha ajabu bado ameajiriwa! 🙂🙂

Ukishajihisi wewe mwenyewe kuwa ni genius, basi sio genius for real. Bali ni kinyume chake.

Hii chai naona imekosa sukari.

-Kaveli-
naomba umwambie alipie Tangazo aiseee [emoji28][emoji23][emoji28][emoji23]....
tena sijui ni matangazo maana katiririka kweri.
 
Namba ya mchungaji,nna matatizo binafs.
Pastor katunzi 0718267171,yuko watspp anaweza kujibu ila kwa simu anaweza chukua muda kupokea kama yuko kwenye huduma kanisa lake nimla watu wengi na anawasaidia sana kwa macho nimeona majini,mapepo cjui umerogwa hapo mwisho nishaona mtu akitapika konokono kwa macho alirogwa na warogaji hapo Yesu yupo wala simsifii unaweza kwenda kanisani jpili hata cku za katikati ana ibada.
 
Naomba adi saa tatu usku uwe online mkuu[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
Niko online muda wote nisipojibu kwa wakati labda nitakua naanda mavazi ya kesho kazini, lakini najua saa tatu nitakua free.
 
Mi naona kama umeandaa episodes kwan maelezo yako kwa binadam wa kawaida haiwezekan,alaf mpinga Mungu maana tungesema labda ni mnabiii
Kwenye kumpinga mungu ndo nikatulia, ila kwa anayemkubali mungu inawezekana kabisa..
 
Hapo kwenye kipengele cha tatu naweza kufanya kitu kama hicho.Naweza kujua jina lako halisi hata kama nimekuona kwa mara ya kwanza.Sinauwezo wa kujua jina lako ikiwa hatuko face to face.Nikikuona naweza kujua jina lako, kabila , umri hata kijiji ulichotoka na naweza kujua pia mko wangapi katika familia yenu na wewe ni wangapi.Lakini hii hua naifanya nikiwa nakuangalia machoni
Ndugu mama yako atakuwa alizaa na jini..! Nikikutumia picha yangu utajua jina, kabila na kikijiji changu??(

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Nakushauri fanya mpango uingie taasisi ya usalama wa taifa. Itakufaa sana kwa uwezo wako huo. Ulisaidie taifa letu kwa kukabiliana na uncertainties na majanga yanayoangamiza taifa hili.

Acha kazi hiyo uliyonayo. Jiunge jkt zen uingie TISS iwe ndiyo career yako.

Usichelewe
 
Back
Top Bottom