Kwa CCM OK, Wapinzani NO!

Hume

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
340
108
Hivi jamani mimi natatizwa sana na utendaji kazi wa Bunge letu tukufu.

Wakati Zito anatoa hoja ya Kuundwa Kamati ya Bunge juu ya buzwagi, wote tunafahamu walivyokuwa wanapondwa na yaliyojitokeza hadi kufungiwa kwake.

Ni kwa nini sasa hoja ya Richmond iliyotolewa na Mwana CCM imeungwa mkono na wote wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga na kuponda?

Je, ni kwa sababu imetolewa na mwanaCCM au ina mantiki kuliko ile ya Buzwagi?
Je, imefanyika hivyo baada ya wao kuona rais kaunda tume waliyokataa kuiunda?

Kulikoni?
 
Miye nasubiri Mbunge wa Upinzani alete hoja ya kutaka Karamagi afungiwe kwa kuliongopea Bunge na aitwe atoe ushahidi kuwa aliyoyasema yalikuwa na ya ukweli.. halafu wapige kura ya kumlinda mwenzao..
 
Wakati wa kuzinduliwa Bunge hili Spika Six alisema hili litakuwa Bunge la Standard and Speed na kiasi fulani tulizugwa na kauli hiyo na kudhani naam, sasa Bunge tunalo. Maajabu ni kuwa hili limekuwa la mizaha na uzembe kwa mustakabali wa Taifa kuliko wakati mwingine wowote katika historia yake.
Maana baada ya Mhe. Rais kukubali kuunda tume ya kupitia mikataba ya madini na kumuweka 'mhalifu' Zito ndani ya kamati hiyo muhimu katika kipindi hiki ambacho hata kifungo chake hakijaisha imejidhihirisha wazi kuwa Wale wote waliosimama kupinga kwa nguvu hoja ya jambo hilo na kuigeuza kuwa ni dhambi mbaya,kuanzia Mudhihiri hadi Malecela hawana tofauti na Comedians
kwani hata kama ulikuwa ni msimamo wa chama,mbona mwenyekiti wao kawatosa? wao walileta dhihaka na uzembe na kupoteza muda wa Bunge pasipo sababu. Bunge liangalie msingi wa hoja bila kujali imetoka upande upi au inambana nani.
 
Miye nasubiri Mbunge wa Upinzani alete hoja ya kutaka Karamagi afungiwe kwa kuliongopea Bunge na aitwe atoe ushahidi kuwa aliyoyasema yalikuwa na ya ukweli.. halafu wapige kura ya kumlinda mwenzao..

Hapo ndipo tutakapopata nguvu ya sisi wananachi kushughulika na Bunge.

Mkjj,
Katiba yetu ina mwanya wowote kweli utakaotuwezesha kulibana Bunge kama halifanyi kazi tuliyowatuma? au tukiona tunahujumiwa kwa njia yoyote?

Najaribu kuiangalia naona kama kuna kipengele kimoja ambigous kweli
 
Hivi jamani mimi natatizwa sana na utendaji kazi wa Bunge letu tukufu.

Wakati Zito anatoa hoja ya Kuundwa Kamati ya Bunge juu ya buzwagi, wote tunafahamu walivyokuwa wanapondwa na yaliyojitokeza hadi kufungiwa kwake.

Ni kwa nini sasa hoja ya Richmond iliyotolewa na Mwana CCM imeungwa mkono na wote wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga na kuponda?
Je, ni kwa sababu imetolewa na mwanaCCM au ina mantiki kuliko ile ya Buzwagi?
Je, imefanyika hivyo baada ya wao kuona rais kaunda tume waliyokataa kuiunda?

Kulikoni?

Kuna shule kidogo unatakiwa kupatiwa;

1. Hoja ya kuundwa kamati ya Richmond ni hoja ya Bunge, kwa kuwa kamati ile ya Uchumi na Biashara ilikasimiwa madaraka na Bunge kuangalia mambo yote yanayohusu maeneo hayo... na ikaleta mapendekezo bungeni kwamba hawakuelewa jambo la Richmond na riport ya PPA na ya PCCB zinahitaji kuangaliwa zaidi kwa makini... Hoja hii si ya Shelukindo!!! na wala si ya Mbunge wa CCM, kumbuka kwenye Kamati za Bunge zote zinawabunge wa Upinzani.

2. Hoja ya Buzwaji haijaundiwa tume wala kamati hata mpaka leo!!! ila unaweza kusema issue ya Buzwaji imesaidia kuweka mazingira ya kuunda Tume ile ya Madini aliyounda rais hivi karibuni.

3. Nakumbuka hoja ya Richmond kuundiwa kamati haikuwahi kutolewa bungeni, ila kuna mizengwe ilifanyika mpaka hoja haikupelekwa bungeni.

4. Ni kweli kuna-issue ya wengi wape,,, maana ndio hivyo tena demokrasia pale bunge ni ya kura (waonunga mkono semeni ndiyooo, wasiounga semeni sio) sasa CCM wakisema ndio, mambo ndio hivyo tena, well, demokrasia yetu ni changa but we are improving slowly.

5. Zile kamati za Kudumu za Bunge zina nguvu kubwa sana kuliko mswada binafsi wa mbunge mmoja mmoja... but in short hakuna mbunge wa CCM ambaye ameleta mswada binafsi kwenye haya mambo mawili.
 
Miye nasubiri Mbunge wa Upinzani alete hoja ya kutaka Karamagi afungiwe kwa kuliongopea Bunge na aitwe atoe ushahidi kuwa aliyoyasema yalikuwa na ya ukweli.. halafu wapige kura ya kumlinda mwenzao..

Nahisi safari hii wabunge wa CCM wamestuka kwamba ndanda anakowapeleka si kwenyewe! Vinginevyo 2010 wataambulia patupu!

Kwa mtaji huu, huenda bunge likarejea kuwa bunge kwani wabunge wengi wa CCM hawatakuwa tayali kuweka 'yes' palipo na 'no' na 'no' palipo na 'yes'

Chanagamoto ya JK kumuweka Zitto kamati ya Madini pia ni another 'message sent'
 
ccm wameona wamezidiwa kete na wapinzani..re vita dhidi ya rushwa. in the court of public opinion ccm ni chama kinachohusishwa na kutetea rushwa na ufisadi.....it is time to reclaim the high moral ground from the opposition. kuna haja ya 'kupokonya' vita dhidi ya rushwa na ufisadi kutoka mikononi mwa upinzani.. ndio maana watu wenye vitisho dizaini ya ngombale ilibidi wawekwe kando!

otherwise mtu anajuliza kama takukuru yenyewe ilifanya uchunguzi na kutoa public clearance kwamba mkataba wa richmond haukuwa na mazingira ya rushwa..then WHY NOW? why not let sleeping dogs lie??

at this point nafasi ya hosea kama dg wa takukuru is no longer tenable. this is a no confidence vote in the institution..na nashangaa why he has not yet been given his marching orders....ama kuna issue hapa ambayo hatuambiwi?
 
Kikibwa hapa nadhani wamejifunza kutokana na adhabu walizokuwa wamezipata. Kumbuka mmojawapo alitoa hoja sasa hana mkono mmoja.

Haikuishia hapo bali wengine wamevunjika mbavu na hata kupoteza maisha baadhi ya wabunge na kada wa chama.

Inawezekana wakayi ule mchakato wa uchaguzi ulikua unaendelea so watu waliogopa kujionesha waziwazi kwamba wanaipondea serikali ya chama chao sasa uchaguzi umeisha so they have nothing to loose.

Inawekana walikua wanawapa muda wahusika waweze kuweka makabrasha yao vizuri ili tume ikiundwa isiweze kubaini makosa yaliyofanyika

so huo ndio mtindo wa kulinda

Nawakilisha
 
Hii ni Tanzania yetu sote na lazima tuwe tunakubaliana kama wasomi na wajuzi wa mambo.Kama si hoja za wapinzani kuunmgwa mkono na wananchi na kupelekea JK na kundi lake kushinikizwa na wazungu kujibu hoja basi hakuna cha Kamati wala nini kingalitokea. Lakini baada ya JK kuamua kumemza jiwe kanabwa na wenye pesa zao basi katumia njia nyingine ya kujibu hoja nayo ni kuunda Tume . Nasema Zitto hatalala na atasema kila kitu na hapa utaona utata mwingine . Kilitime kubaliana na wengi JK na CCM hawana namna na kaona CCM haina lake baada ya zomea zomea nk .Richmond ilipigiwa kelele sana na wapinzani na wao wamejifanya kuileta kupitia CCM .Kapandikizwa na kutaka kusaidia maneno ya JK majuzi kwenye mkutano wenu Dodoma .

Kama Zitto hafai na kama karopoka kama mnavyodhani nyie wana CCM , na kwa jinsi JK anavyojali Chama zaidi ya Nchi no way angalimweka Zitto hapo .Malecela si mwanasiasa hata kidogo na ndiyo maana katemwa na sasa wanajaribu kuonyesha kwamba yeye alikuwa na pressure za CCm kuwa chama kikongwe lakini alikuwa anakiua kwa kukatalia hata hoja za uwazi .

Ndiyo Hongera Zitto , Hongera Upinzani slowly wengi wape watatia akili. Hili ni siahara mbaya sana kwa Sitta maana anaonekana hana ajualo na Bunge la wengi .
 
Kwa upande wangu mimi hawa watu wanacheza michezo ya kisiasa tu ili kujisafisha kwenye macho na akili za watanzania wengi ambao hawatatumia akili zao kufikiria beyond this action.

Wamewatoa wachache sadaka kuokoa meli isizame kimoja. Wameamua kuwadhalilisha wale walioonekana waziwazi kumpinga zitto na kuwatumia wale wliopinga kichini chini kuwaonyesha watz kwamba nao wako kazini. Swala ninalojiuliza ni kwa nini JK hakuunda hiyo kamati mpaka miezi imepita?

Bado siwaamini hawa hata kidogo
 
Mtanadao ulishaliteka bunge na kuligeuza kijiwe cha siasa za vyama. Mtandao unamalengo ya kuona kuwa haupingwi mahali popote yaani bungeni hadi kwenye vyombo vya habari na ndio maana Rostam Aziz arijaribu kupenyeza kwenye vyombo vya habari kujihakikishia hili.

Wabunge wetu walidhani kwa kitendo chao cha kumnyamazisha zitto basi wamemaliza na wanamfurahisha JK, kumbe ni janja ya Lowasa kufanikisha mambo yake.

But any way hawa jamaa JK na Lowasa ni wasanii wanajua kucheza na mambo lakini lao ni moja. Mmoja anachezesha hiki kikishindikana anaingia mwingine na gia tofauti ili mradi ni kutuvuruga tu huku mambo yao yakiendelea.
 
Hapo ndipo tutakapopata nguvu ya sisi wananachi kushughulika na Bunge.

Mkjj,
Katiba yetu ina mwanya wowote kweli utakaotuwezesha kulibana Bunge kama halifanyi kazi tuliyowatuma? au tukiona tunahujumiwa kwa njia yoyote?

Najaribu kuiangalia naona kama kuna kipengele kimoja ambigous kweli

Hapana Katiba yetu inacho kipengele nacho ni kuwatimua maofisini 2010 kwa kuwanyima kura!!
 
Hivi jamani mimi natatizwa sana na utendaji kazi wa Bunge letu tukufu.

Wakati Zito anatoa hoja ya Kuundwa Kamati ya Bunge juu ya buzwagi, wote tunafahamu walivyokuwa wanapondwa na yaliyojitokeza hadi kufungiwa kwake.

Ni kwa nini sasa hoja ya Richmond iliyotolewa na Mwana CCM imeungwa mkono na wote wale waliokuwa mstari wa mbele kupinga na kuponda?

Je, ni kwa sababu imetolewa na mwanaCCM au ina mantiki kuliko ile ya Buzwagi?
Je, imefanyika hivyo baada ya wao kuona rais kaunda tume waliyokataa kuiunda?

Kulikoni?

Ndio tukasema ni haramu katika mfumo wa vyama vingi kuwa na bunge lenye wabunge lundo kutoka chama kimoja. Kwa hiyo sisi hapa kwenye forum mchango wetu mojawapo kwa taifa letu ni kujielimisha sisi wenyewe na kuwaelimisha wapiga wengine kwa ujumla ili katika chaguzi zijazo tuhakikishe hakuna chama kinachokuwa n absolute dominance bunegeni, it is as simple as that. Tukishajua hili, hatuna sababu ya kushangaa kinachotokea katika bunge letu. Kushangaa kwetu kunaonyesha jinsi ambavyo watanzania kwa ujumla tulivyo nyuma katika uelewa wa kisiasa na jinsi ambavyo tunahitaji sana elimu ya jamii, siasa, uzalendo na uraia wema. Tuendelee kujielimisha, ipo siku tutajua na ndio mwanzo wa kuamka.
 
Hapana Katiba yetu inacho kipengele nacho ni kuwatimua maofisini 2010 kwa kuwanyima kura!!

Hapa naona tunaongozwa na chama kimoja.Cha msingi hapa upinzani ujipange na kuweka vijana wengi wenye uwezo na ushwawishi mkubwa kwa wananchi kukabiliana na CCM next election.Hawa mafisadi tutawashinda tu hapa ni ugenius wa kisiasa tu utakaowakomesha

Kama jimbo langu naona huyo mbunge na waziri anaingiaga bungeni kwa sababu ya jina lake tu.Hajawahi kuona kijana wa kumfundisha siasa za kisasa.Asubiri muda ufike maanake nilimsikia akiwaambia watu eti ukifika muda wake wa kung'atuka atawatanagazia wanajimbo na kumpendekeza mrithi

Huyo ndiye aliyenivunja mbavu kwa kumiliki Jimbo,Ngoja mda ufike.
 
CCM wanajaribu kubadilika maana wanajua sasa hivi Watanzania wamebadilika na kitendo cha kumsimamisha Zitto kilipingwa vikali sana katika kila kona ya Tanzania. Hivyo wanabidi wawe makini sana au 2010 watakuwa ni historia.

CHABY BARASA in Dodoma
Daily News; Friday,November 16, 2007 @00:03

Standing committee meetings will effective the next session of parliament be open to members of the public.

The new procedure is one of 18 new rules passed by the National Assembly here yesterday in what Deputy Speaker, Anne Makinda said was to match with the times.

“We want the Tanzania Parliament to be modern and exemplary,” said Ms Makinda when explaining the need to amend the rules.

However, the changes also touched on her position. She will have to take an impartiality oath as Deputy Speaker effective the next meeting in January.

Speaker Samuel Sitta told the Daily News later that there was no rule requiring the Deputy Speaker to take oath for honesty, to be fair, harbour no hatred and to be loyal to the country.

He or she took oath only as an ordinary MP, explained Mr Sitta.

Under the changes too, ordinary citizens will now have the right to write to the Speaker to defend themselves against utterances made in the chamber where MPs enjoy parliamentary immunity against prosecution.

Staring next January also, the national anthem will be sang in parliament at the beginning and ending of every meeting, Mr Sitta said.

Coming also is a department of a parliamentary chief legal advisor with his team in order to stop depending on the Attorney General for parliamentary y legal advise, Mr Sitta said.

The MPs will hold a three day seminar before the next meeting of parliamentary to familiarise themselves with the rules, Mr Sitta said.
 
Sababu ni moja, na ni rahisi, waliotaka tume ni "WAPINZANI", jina lina jielezea lenyewe. You cant agree na mpinzani wako.
 
Back
Top Bottom