Kwa baba tuko watano, kwa mama wanne..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,227
116,839
Juzi kati nilijikuta kwenye kampani ya watu wa rangi mchanganyiko. Kulikuwepo na wazungu wachache, wahindi kadhaa, wasomali, waarabu na sisi waafrika wawili watatu.

Katika kupiga story tofauti tofauti...tukajikuta tumeangukia kwenye jambo ambalo binafsi niliona very interesting.

Ilianza kwa mmoja wa wahindi kumuuliza mswahili mmoja 'kwenu mmezaliwa wangapi'?

Mswahili akajibu, "Kwa baba watano,kwa mama wanne ila baba mmoja mama mmoja ni wawili."

Hapo ndo gumzo likazuka. Wazungu waliokuwepo hapo na wahindi wakasema 'hii kitu ni common mno kwa waswahili' kiasi ni vigumu kukuta mswahili atakayekujibu tu "kwetu tuko wanne baba mmoja mama mmoja". Karibu kila mswahili lazima ukute kwa baba tuko hivi,kwa mama tuko hivi.

Wahindi na wazungu wachache waliokuwepo wanadai kwao sio common sana hasa wahindi wao wanadai hiyo ni very rare case kwao lakini wanakuta karibu kila mswahili mwendo ndo huo huo.

Kiukweli binafsi nilikuwa sijawahi kukaa chini na kujiuliza hili jambo na binafsi naamini watu wote duniani hii kitu kawaida sana lakini kwa wale wachache tulikouwa pale ilikuwa kila mtu anasema kwao hakuna except kwa sisi waswahili.

Na nilivyowaelewa wanaona kama ndo kigezo cha kuwaponda waswahili kuwa ni watu wa ngono za ovyo ovyo na kuzaa ovyo ovyo bila kupangilia maisha wala kujali watoto wanaowazaa wataishi vipi.

Kwamba watu wa rangi zingine angalau kwao sio sana kama sisi waswahili ambako ni kawaida kukuta mama amezaa na wanaume watatu tofauti na kila mwanaume nae kazaa na wanawake tofauti kiasi unakuta kuna familia hata watoto hawajijui hasa wako wangapi kwa baba yao.

Maswali yangu kwako mwana JF,
Je kwenu mko wangapi?
Je wewe umeepuka hii?
Je mwanao umemuepusha na hii?
 
Aseeeh.. hata wasomali wanatuzidi mkuu?

Nwei : kwetu tupo wanne mama mmoja baba mmoja.

Kwangu bado sijajua maana menopause bado.

Wanavyodai wao...
angalau kwa wenzetu wengi sio jamba la kujivunia

but kwa sisi waswahili ni kama ni sehemu ya utamaduni wetu now
 
Mimi kwa Baba nane 'wanaojulikana' kwa mama watatu. Ukichukuwa 'Baba Union Mama' (kwa wale wataalamu wa 'Set') unapata tupo ndugu 11 jumlisha na yule aliyeaga dunia jumla 12.

Idadi ya weza kuwa zaidi nikifanya Union 'mama wengineo'.

Binafsi sijawaepusha wanangu kwa hili kwani siku hizi wanawake wengi wanazaa na mimi huku wengineo pia wakitamani na kuomba wapate uzao na mimi.
 
Back
Top Bottom