Kwa akili hii ya TANROAD na watawala wetu sioni foleni zikisha Dar

Labda wewe ndiye huelewi maana ya ring road... Huenda unachukulia picha ya ringi la baiskeli na kuwaza kuwa bara bara inatakiwa iwe ya duara kama ringila baiskeli ndio iitwe ring road.

Kwa taaarifa yako, Ring road inaanzia Tegeta- Goba- Mbezi- Kinyerezi...Majumba sita- Pale unavuka barabara unaendelea Kitunda- Kivule- Msongola- Mbagala- Kongowe- Tuangoma-Kigamboni!
Nyingine inachepukia Kifuru- Pugu- Chanika- Mvuti- Msongola- Mbagala
Mpe somo huyo Bibi
 
Sawa lakini kutokana na matendo ya kipuuzi wa madreva wetu, ndo maana serikali inakuja na maamuzi ya kipuuzi. Wenzetu wanasema stupid question needs stupid answer.
sikumbuki ni lini ccm na serikali yake kupitia wanasiasa wake uchwara iliwahi kukiri kosa hadharani, mara zote huwa inasukumiza madhaifu yake kwa watu wengine,Hivi unajua kwanini barabara zinazojengwa sasa ni tofauti na za hapo nyuma kwa maana ya upana? je magari yameongezeka upana?wakati wa ajari nyingi ccm wanasiasa wa ccm walisingizia madereva huku wakijua fika kuwa barabara nyembamba ni moja ya sababu kuu za ajari
 
Halmashauri ya Jiji nao wajitafakali utendaji kazi wao.

Kwanini wanaendelea kutoa vibali vya ujenzi wa majengo makubwa katikati ya jiji na maeneo ya mijini?
 
Halmashauri ya jiji kwanini mnatoa vibali vya ujenzi karibu na maeneo ya hifadhi ya barabara?

Hivi tuwaeleweje kwa mfano?

Angalia pale makumbusho jinsi magorofa yalivyojengwa barabarani,

Sijui pale barabara itajengwaje walisika jamaa wa kijiwe cha bodaboda wakijiuliza ilikuwaje.
 
Ingependeza vibali vya ujenzi wa magorofa yajengwe pembezoni mwa miji (outskirts ) ili wakati wa asubuhi na jioni watu watawanyike wasiende uelekeo mmoja.
 
Mimi nilidhani mipango ya kujenga ubungo interchange na upanuzi wa barabara ya Morogoro kuwa njia sita,tatu kila upande from Ubungo to Chalinze ilikuwa ni mkakati wa kupunguza kama si kuondoa kabisa msongamano katika barabara hiyo na kuwawezesha watanzania kupunguza gharama zinazosababishwa na msongamano huo.

Sasa badala ya kupunguza msongamano kama plan ya kwanza iliyokuwa,naona sasa tunahamisha foleni toka Ubongo na kuipeleka Mbezi ili kesho atokee malaika mwingine aje kutatua tatizo la foleni Mbezi,hatari sana.
Sasa wewe ulitaka ijengwe njia 8 toka Kimara hadi Chalinze kwa mkupuo? Si tunaenda hatua kwa hatua
 
Halmashauri ya jiji kwanini mnatoa vibali vya ujenzi karibu na maeneo ya hifadhi ya barabara?

Hivi tuwaeleweje kwa mfano?

Angalia pale makumbusho jinsi magorofa yalivyojengwa barabarani,

Sijui pale barabara itajengwaje walisika jamaa wa kijiwe cha bodaboda wakijiuliza ilikuwaje.
Ni wazo zuri ila hata miji ya wenzetu down town ndo kwenye magorofa mengi na shughuli nyingi zipo hiko
 
Ni wazo zuri ila hata miji ya wenzetu down town ndo kwenye magorofa mengi na shughuli nyingi zipo hiko

Kwa baadhi ya nchi ilifanyika na imekuwa ikifanyika hivyo kimakosa!
Lakini kwa baadhi ya nchi ni sababu ya upungufu wa maeneo unakuta ka nchi ni kadogo,
Pia kuna sababu za kijografia n.k

Lakini kwetu sisi maeneo tunayo ya kutosha na jografia yetu iko vizuri sana.

Lakini pia kuna tatizo la uadilifu na uzalendo kwa kiasi kikubwa.

Labda tujitafakali tunakwama wapi?

Ndo maana saingine Anko Magu analipuka maana mambo mengine yanachosha kuyasikia pale yanapofanyika kwa makusudi fulani na kusahau kuweka public interest pembeni
 
Mkuu hapa kwetu shida si huduma zote kuwa city centre bali shida ni miundombinu mibovu ya barabara na utawala mbovu under ccm,Magu huyo huyo amekuwa serikali for more than 20 years na barabara hizo mbovu,nyembamba na zenye matuta na zebra crossing kila baada ya kilometa moja yeye ndo kasimamia ujenzi wake,mama hskuwa sehemu ya huo ujinga mbona hakujiuzuru?
 
traffic wasiwe wanapokea rushwa kwa madereva wanaotanua na kuvunja sheria hasa daladala
Wiki kama nne tulikaa mbezi toka saa kumi jioni ...tumekuja kutoka saa 4 na nusu Usiku...tulikuwa tunaelekea Mulimba...Msamvu...tulifika saa tisa kasoro chache za Usiku...usinulize mlimba nilifika saa ngapi na nilikuwa katika hali gani. Kibaya kuna dereva wahuni wali'tanua' kote kote...wakablock lanes zote...hakuna wa kutoka wala kuingia....
 
pole sana mkuu,wala si uhuni wa madereva ila uwezo mdogo wa kufikiri wa watawala wetu.kila mtu anajua shida iliyopo kwenye makutano ya barabara zote jijini Dar,so hapakuwa na haja yoyote ya kufikiria kuweka taa pale Mbezi,kwa mtazamo wangu a simple bridge ilitosha kumaliza foleni ya mbezi ili magari ya Morogoro road yapite juu ya daraja na magari ya Goba yapite chini,simpo like dhati
 
naona ring road imetajwa sanaa hapa ila njia sahihi kwanza ni kupeleka bandari kavu nje wa mji wa dsm hasa hasa itapendeza wakiweka chalinze hapo wataondoa kero za malori kuja mjini, la pili ni kuboresha usafiri wa umma toka mjini CBD mpaka nje ya miji au viunga vya miji urban sprawl mfano huko uswahili kwetu mbezi, tgt, gomc, mbagal
 
Chanzo Kingine cha Traffic jam Tz ni Parking. Watu hupaki magari ya Ofisi zao ktk njia za Pembeni au za watembea kwa miguu/baiskeli. Hivyo njia hizi hufungwa na makundi yote kutegemea Main Road.

Suluhu ni

1. Kuagiza kila mjenga gorofa au Nyumba ya Biashara mjini aweke Underground parking chini ya Ardhi hadi floor 3 hivi. Gari za ofisi zilipo ndani ya jengo hilo zipark ndani (chini ya ardhi).

2. Kuweka Kingo kubwa za tofali za zege, kutenganisha barabara za watembea mguu na magari. Bodaboda wa Bongo huvamia hizi barabara za waenda kwa miguu na kuzifanya zao. Kingo hizi zita dhibiti Magari na Bodaboda kupark au kutembelea sehemu isiyo yao.

3. OUTSOURCING. Ramani za mji yote ya Tz zifumuliwe nchi nzima. Na hii kazi wapewe WACHINA. Naamini mradi wa kununua Madiwani na Wabunge umeisha.

Tutenge Billion 100 nchi nzima, tuwape Wachina wadesign Tz ya miaka 1000 ijayo.
 
Mkuu kabla nchi hii haijawa chini ya ccm kwa 100% mradi wa kununua mdiwani na wabunge hauwezi kuisha
 
Back
Top Bottom