Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,520
- 86,081
Waswahili walisema kuwa "Kumpiga chura teke ni kumuongezea mwendo". Ni kweli ataumia kidogo kwa sababu utakua umemshtua ila ukweli ni kwamba umemuongezea mwendo. CCM wanafurahi wapinzani kukamatwa ovyo tena wakiwa kwenye vikao vya ndani, wapinzani kuzuiliwa kufanya Mikutano yao ili tu asikike mtu mmoja/chama kimoja kwa manufaa ya mtu au chama.
Kampeni zilizopita CCM walipata muda kabla ya kampeni kupinga au kujibu baadhi ya hoja za wapinzani na hivyo kuzidhoofisha kwa kiasi kikubwa kabla ya Uchaguzi Mkuu. Wapinzani wa leo hii ambao hawana mahali pa kuikosoa CCM na CCM ambao pia watakosa cha kujibu kwakuwa Upinzani umezuiliwa kusema itakua pigo kubwa sana sana kwa CCM kuja kujibu hoja/kashfa/tuhuma zitakazoibuliwa na Upinzani wakati wa uchaguzi na hivyo kuiweka CCM upande mbaya zaidi kuliko hata ilivyo sasa.
Ombi langu, CCM waendelee kuzuia mikutano ya Upinzani ila wahakikishe wana majibu ya kutosha ya kuja kujibu wakati Wapinzani watakaposema. Upinzani nao wataendelea kukusanya evidence za madudu ya CCM halafu watakuja kukutana ulingoni wakati ukifika, yaani CCM watajikuta wanajibu hoja/kashfa za upinzani badala ya kueleza waliyoyafanya na watakayoyafanya.
Twende kazi