SoC03 Kuzingatia kariba za watu kwenye usaili na uteuzi kutachochea uwajibikaji

Stories of Change - 2023 Competition

jemsic

Member
Jul 1, 2020
21
51
UTANGULIZI
Imetokea mara nyingi tumesikia Rais akiteua au kuchangua watu mbalimbali kushika nyadhifa serikalini au pengine watu kuitwa kwenye usaili wa kazi ili kuchambua na kupata wafanyakazi bora. Pamoja na ujuzi na uzoefu wa watu, ili kuteua au kupata wafanyakazi wenye weredi na ufanisi mkubwa kwa lengo la kukuza uwajibikaji, kariba za watu zimepaswa kuwa ni kitu cha kuzingatiwa sana. Wanafalsafa mbalimbali wameelezea jinsi gani uteuzi au usaili bora unaweza kufanyika kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo hudhihirisha kariba za watu ili kudumisha uwajibikaji. Mwanafalsafa William Marston kaelezea nadharia yenye muundo unaojumuisha kariba nne ambazo huwafanya wafanyakazi kufanya vizuri katika kitengo alichopo na kariba hizo ni uthabiti, uadilifu ushawishi na usimamizi.

AINA NNE ZA KARIBA
1690536402205.png

Kariba ya uthabiti
hujumiusha wafanyakazi au watawala wenye kupenda utulivu na kutokwazana kabisa na mtu yeyote katika kazi au utawala hata kama inabidi itokee hivyo. Wafanyakazi wenye kariba hii mara nyingi hutatanguliza na kudumisha maelewano baina yao na wengine na hutoa msaada na kushirikiana na wengine hasa wale wanaofanya nao kazi au kuwaongoza. Ni watu wenye huruma, kuaminika, subira na walio thabiti katika kutekeleza majukumu yao. Wafanyakazi wa mtindo wa uthabiti hustawi kwa kufanya kazi nyingi na kuunda mazingira ya kufanya kazi kwa timu chanya na yenye usaidizi wa kutosha kila inapobidi. Mara nyingi wenye kariba ya uthabiti hupendwa sana na jamii kwa sababu ya kuwa na mwelekeo wa kuepuka migongano. Ubaya wa kariba hii ni kwamba hupelekea mara nyingi wafanyakazi hawa wanahisi kulemewa na madai au pengine shughuli ambazo zinakuwa nje ya uwezo wao kwa sababu mara nyingi hawakatai.

Kariba ya pili ni uadilifu ambayo watu wenye kariba hii huwa na faragha, umakini na uwezo mkubwa wa uchambuzi wa kimantiki katika kutatua matatizo kwenye jamii. Watu wa kariba hii huchukuliwa kuwa na weredi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya utawala japo hutokea kipindi wakapwaya kwa sababu za kibinadamu. Wafanyakazi wenye kariba ya uadilifu ni wasikilizaji wazuri na hivyo huwa wasuluhishi wazuri pia wa matatizo na changamoto katika jamii. Wafanyakazi hawa wanahusishwa zaidi na viwango vya juu vya kuweka vipaumbele na mipango na kuitekeleza kwa jitihada kubwa. Watu wenye kariba ya uadilifu ni makini katika kushughulikia jambo kwa uangalifu sana. Kwa upande mwingine, wafanyakazi mwenye kariba ya uadilifu anapotambua tatizo au hatari huweza kuchelewesha maamuzi kwa sababu ya muda mrefu wa kufanya uchunguzi na utafiti na hivyo inaweza kuleta athari mbaya zaidi.

Kariba ya tatu ni ushawishi amabo hujumisuha watu wenye uchangamfu sana na wenye kupenda mazungmzo na majadiliano. Watu hawa mara nyingi huwa na marafiki wengi sana na huzoeaza na wafanya kazi wenzake kwa haraka hata kama mfanya kazi ni mgeni. Pia, huwaamini wengine kirahisi na wanapenda kufanya kazi katika na makundi ya watu wengi. Wafanyakazi wa kariba ya Ushawishi huwa na shauku na matumaini wakati wa kutekeleza majukumu na kazi zao kwani hutafuta njia rahis zaidi ya kufanikisha kazi kwa weredi. Zaidi sana hutafuta jambo la kufurahisha au kuchangamsha ili kupunguza uzito wa kazi na kuifanya ionekane rahisi hata kama ina ugumu uliopitiliza. Hivyo basi ni wazuri katika uhamasishaji katika kazi na hata kukuza mahusiano bora kati ya wanafanya kazi. Lakini, kariba hii ubaya wake ni soga nyingi na pengine mizaha ambayo hufanya kazi kuchukua muda mrefu kukamilika kutokana na kuvuruga umakini.

Na kariba ya nne na ya mwisho ni usimamizi
ambayo hujumisha watu ambao huwa na misimamo mikali na kuwa na maamuzi magumu na yasiyopinda. Watu wenye kariba ya usimamizi ndani yao huweka malengo na kufanya kazi kwa kasi ili kuyatimiza kwa kila namna. Wafanyakazi wa kariba ya usimamizi hupenda kujiwekea shinikizo ili kufanya kazi na kuonesha mfano kwa wafanya kazi wenzao. Hata inapotokea wakawa na kasi ndogo katika utendaji wao hutafuta mbinu mbadala ya kuongeza kasi ya utendaji. Watu wa kariba hii hupenda kuonesha njia na namna mpya ya kufanya mambo katika kundi la watu na pengine huelekeza njia nyepesi katika ufanyaji kazi. Watu hawa na umuhimu kwenye kazi hasa pale unahitajika usimamizi ili kuhakisha malenngo yanakamilika. Lakini kwa upande mwingine, kariba hii huleta madhara hasa pale ambapo wahusika huwa na maslahi binafsi hasa pale wanaposimamia kwa ubabe na kutumia kauli kali kwa wenzake.

MAPENDEKEZO
Kariba za watu katika ufanyaji kazi zimekuwa sio kitu cha kuizngatiwa sana japo kina umuhimu mkubwa ili kufikia malengo ya kazi na taasisi husika. Mara nyingi hata katika usaili waajiri na maafisa rasilimali watu wawekuwa wakizingatia vyeti vya taaluma kama kigezo pekee katika kuwapata wafanyakazi. Na ni kweli hupata wafanyakazi wanaowataka lakini wenda wakakosa wafanyakazi bora kwa kutokuangalia kariba kama sifa mbadala mfanyakazi kitengo fulani. Kwa kuzingatia kariba na vyeti vya taaluma kwa pamoja tutapata wafanyakzi bora katika vitengo mbalimbali.Yafuatayo ni mapendekezo ya namna ya kuzitumia kariba za watu ili kukuza uwajibikaji:​
  • Wasaili na maafisa rasiimali watu wazingatie kariba pamoja na vyeti vya taaluma vya wasailiwa katika kupata wafanyakazi bora na wawajibikaji​
  • Mfumo wa kuzingatia kariba za watu unapaswa pia uzingatiwe katika upandishwaji wa vyeo kwa wafanyakazi. Kwani ikizingatiwa itakuza sio tuu uwajibikaji lakini pia utawala bora kwa tasisi na nchi kwa ujumla.​
HITIMISHO
Kariba zote ni za pekee na watu wenye kariba hizi tofauti hufaa katika sehemu, nyadhifa na vitengo mbalimbali na zinapotumika vizuri hukuza uwajibikaji wa kila mmoja katika taasisi. Umuhimu wa kutambua kariba za watu ni kwamba humtofautisha mtu mmoja na mwingine na pia inaathiri namna mhusika atavyotelekeza majukumu yake kwa kushirikiana na wengine, namna watavyoshughulikia msongo na namna jumla ya utendaji wa kazi zao. Kuna kariba mbalimbali ambazo wafanyakazi walioteuliwa au kusailiwa na kupata ajira huwa nazo ili kufanya kazi husika. Mchangnyiko wa sifa nyingi ikiwa ni pamoja na utashi wa mawasiliano, ushirikiano na wengine, uwezo wa kujenga hoja, misimamo na uwezo wa uongozi pamoja na utatuzi wa matatizo na changamoto mbalimbali katika jamii huzingatiwa ili kuleta kariba yenye kufaa kukidhi vigezo vya wafanyakazi wanaowajibika.

KUMBUKUMBU ZA REJEA
Marston, W. M. (2013). Hisia za watu wa kawaida (Vol. 158). Routledge
Mulgan, R. (2000). 'Uwajibikaji': dhana inayopanuka kila wakati?. Utawala wa umma, 78(3), 555-573.​
 
UTANGULIZI
Imetokea mara nyingi tumesikia Rais akiteua au kuchangua watu mbalimbali kushika nyadhifa serikalini au pengine watu kuitwa kwenye usaili wa kazi ili kuchambua na kupata wafanyakazi bora. Pamoja na ujuzi na uzoefu wa watu, ili kuteua au kupata wafanyakazi wenye weredi na ufanisi mkubwa kwa lengo la kukuza uwajibikaji, kariba za watu zimepaswa kuwa ni kitu cha kuzingatiwa sana. Wanafalsafa mbalimbali wameelezea jinsi gani uteuzi au usaili bora unaweza kufanyika kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo hudhihirisha kariba za watu ili kudumisha uwajibikaji. Mwanafalsafa William Marston kaelezea nadharia yenye muundo unaojumuisha kariba nne ambazo huwafanya wafanyakazi kufanya vizuri katika kitengo alichopo na kariba hizo ni uthabiti, uadilifu ushawishi na usimamizi.

AINA NNE ZA KARIBA
View attachment 2701267

Kariba ya uthabiti hujumiusha wafanyakazi au watawala wenye kupenda utulivu na kutokwazana kabisa na mtu yeyote katika kazi au utawala hata kama inabidi itokee hivyo. Wafanyakazi wenye kariba hii mara nyingi hutatanguliza na kudumisha maelewano baina yao na wengine na hutoa msaada na kushirikiana na wengine hasa wale wanaofanya nao kazi au kuwaongoza. Ni watu wenye huruma, kuaminika, subira na walio thabiti katika kutekeleza majukumu yao. Wafanyakazi wa mtindo wa uthabiti hustawi kwa kufanya kazi nyingi na kuunda mazingira ya kufanya kazi kwa timu chanya na yenye usaidizi wa kutosha kila inapobidi. Mara nyingi wenye kariba ya uthabiti hupendwa sana na jamii kwa sababu ya kuwa na mwelekeo wa kuepuka migongano. Ubaya wa kariba hii ni kwamba hupelekea mara nyingi wafanyakazi hawa wanahisi kulemewa na madai au pengine shughuli ambazo zinakuwa nje ya uwezo wao kwa sababu mara nyingi hawakatai.

Kariba ya pili ni uadilifu ambayo watu wenye kariba hii huwa na faragha, umakini na uwezo mkubwa wa uchambuzi wa kimantiki katika kutatua matatizo kwenye jamii. Watu wa kariba hii huchukuliwa kuwa na weredi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya utawala japo hutokea kipindi wakapwaya kwa sababu za kibinadamu. Wafanyakazi wenye kariba ya uadilifu ni wasikilizaji wazuri na hivyo huwa wasuluhishi wazuri pia wa matatizo na changamoto katika jamii. Wafanyakazi hawa wanahusishwa zaidi na viwango vya juu vya kuweka vipaumbele na mipango na kuitekeleza kwa jitihada kubwa. Watu wenye kariba ya uadilifu ni makini katika kushughulikia jambo kwa uangalifu sana. Kwa upande mwingine, wafanyakazi mwenye kariba ya uadilifu anapotambua tatizo au hatari huweza kuchelewesha maamuzi kwa sababu ya muda mrefu wa kufanya uchunguzi na utafiti na hivyo inaweza kuleta athari mbaya zaidi.

Kariba ya tatu ni ushawishi amabo hujumisuha watu wenye uchangamfu sana na wenye kupenda mazungmzo na majadiliano. Watu hawa mara nyingi huwa na marafiki wengi sana na huzoeaza na wafanya kazi wenzake kwa haraka hata kama mfanya kazi ni mgeni. Pia, huwaamini wengine kirahisi na wanapenda kufanya kazi katika na makundi ya watu wengi. Wafanyakazi wa kariba ya Ushawishi huwa na shauku na matumaini wakati wa kutekeleza majukumu na kazi zao kwani hutafuta njia rahis zaidi ya kufanikisha kazi kwa weredi. Zaidi sana hutafuta jambo la kufurahisha au kuchangamsha ili kupunguza uzito wa kazi na kuifanya ionekane rahisi hata kama ina ugumu uliopitiliza. Hivyo basi ni wazuri katika uhamasishaji katika kazi na hata kukuza mahusiano bora kati ya wanafanya kazi. Lakini, kariba hii ubaya wake ni soga nyingi na pengine mizaha ambayo hufanya kazi kuchukua muda mrefu kukamilika kutokana na kuvuruga umakini.

Na kariba ya nne na ya mwisho ni usimamizi ambayo hujumisha watu ambao huwa na misimamo mikali na kuwa na maamuzi magumu na yasiyopinda. Watu wenye kariba ya usimamizi ndani yao huweka malengo na kufanya kazi kwa kasi ili kuyatimiza kwa kila namna. Wafanyakazi wa kariba ya usimamizi hupenda kujiwekea shinikizo ili kufanya kazi na kuonesha mfano kwa wafanya kazi wenzao. Hata inapotokea wakawa na kasi ndogo katika utendaji wao hutafuta mbinu mbadala ya kuongeza kasi ya utendaji. Watu wa kariba hii hupenda kuonesha njia na namna mpya ya kufanya mambo katika kundi la watu na pengine huelekeza njia nyepesi katika ufanyaji kazi. Watu hawa na umuhimu kwenye kazi hasa pale unahitajika usimamizi ili kuhakisha malenngo yanakamilika. Lakini kwa upande mwingine, kariba hii huleta madhara hasa pale ambapo wahusika huwa na maslahi binafsi hasa pale wanaposimamia kwa ubabe na kutumia kauli kali kwa wenzake.

MAPENDEKEZO
Kariba za watu katika ufanyaji kazi zimekuwa sio kitu cha kuizngatiwa sana japo kina umuhimu mkubwa ili kufikia malengo ya kazi na taasisi husika. Mara nyingi hata katika usaili waajiri na maafisa rasilimali watu wawekuwa wakizingatia vyeti vya taaluma kama kigezo pekee katika kuwapata wafanyakazi. Na ni kweli hupata wafanyakazi wanaowataka lakini wenda wakakosa wafanyakazi bora kwa kutokuangalia kariba kama sifa mbadala mfanyakazi kitengo fulani. Kwa kuzingatia kariba na vyeti vya taaluma kwa pamoja tutapata wafanyakzi bora katika vitengo mbalimbali.Yafuatayo ni mapendekezo ya namna ya kuzitumia kariba za watu ili kukuza uwajibikaji:​
  • Wasaili na maafisa rasiimali watu wazingatie kariba pamoja na vyeti vya taaluma vya wasailiwa katika kupata wafanyakazi bora na wawajibikaji​
  • Mfumo wa kuzingatia kariba za watu unapaswa pia uzingatiwe katika upandishwaji wa vyeo kwa wafanyakazi. Kwani ikizingatiwa itakuwa sio tuu uwajibikaji lakini pia utawala bora kwa tasisi na nchi kwa ujumla.​
HITIMISHO
Kariba zote ni za pekee na watu wenye kariba hizi tofauti hufaa katika sehemu, nyadhifa na vitengo mbalimbali na zinapotumika vizuri hukuza uwajibikaji wa kila mmoja katika taasisi. Umuhimu wa kutambua kariba za watu ni kwamba humtofautisha mtu mmoja na mwingine na pia inaathiri namna mhusika atavyotelekeza majukumu yake kwa kushirikiana na wengine, namna watavyoshughulikia msongo na namna jumla ya utendaji wa kazi zao. Kuna kariba mbalimbali ambazo wafanyakazi walioteuliwa au kusailiwa na kupata ajira huwa nazo ili kufanya kazi husika. Mchangnyiko wa sifa nyingi ikiwa ni pamoja na utashi wa mawasiliano, ushirikiano na wengine, uwezo wa kujenga hoja, misimamo na uwezo wa uongozi pamoja na utatuzi wa matatizo na changamoto mbalimbali katika jamii huzingatiwa ili kuleta kariba yenye kufaa kukidhi vigezo vya wafanyakazi wanaowajibika.

KUMBUKUMBU ZA REJEA
Marston, W. M. (2013). Hisia za watu wa kawaida (Vol. 158). Routledge
Mulgan, R. (2000). 'Uwajibikaji': dhana inayopanuka kila wakati?. Utawala wa umma, 78(3), 555-573.​
Asante
 
Back
Top Bottom