Kuzimwa kwa mtandao nchini, TCRA yapewa tahadhari kuelekea uchaguzi/ pin na TMC watoa tamko

Kuzimwa kwa mtandao nchini, TCRA yapewa tahadhari kuelekea uchaguzi/ pin na TMC watoa tamko

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
29,869
Reaction score
34,025
30 May 2025
Dar es Salaam


View: https://m.youtube.com/watch?v=nUGKwZ44tlQ

Tech & Media Covergency na PIN wazungumzia kuhusu changamoto za TEHAMA barani Africa huku mtandao wa X ukiwa umezimwa, na nchi mwenyeji wa mkutano huo wa wadau wa Barani Africa unafanyika Tanzania jijini Dar es Salaam.

Wadau wanasema mamlaka za udhibiti kama TRCA mamlaka ya udhibiti mawasiliano Tanzania zingeweza kutumia njia nyingine badala ya kuzima kabisa mtandao wa X

Wadau hao wasema kuzima mtandao kuelekea uchaguzi mkuu ni njia yenye madhara makubwa, kwani kukosekana uhuru wa mawasiliano kunakimbiza wawekezaji kwa muda mrefu kwa miaka mingi. Hivyo mamlaka kama TCRA zingeweza kutumia njia mbadala badala ya kuzima kwani zoezi la uchaguzi mkuu ni la kuja na kufanyia kila baada ya miaka 5 lakini wawekezaji wanaweza kukimbia kwa miaka 10 kutokana na tishio la kukosekana mawasiliano na uhuru wa kufanya shughuli mbalimbali kwa kigezo cha mazingira kandamizi ya kisiasa.
 
30 May 2025
Waziri Maryprisca Mahundi afungua mkutano manguli wa technolojia ya TEHAMA Africa

View: https://m.youtube.com/watch?v=uuMB_VlkJU8

Huku asilimia 60 tu ya Waafrika bado hawana nafasi ya kufikiwa mitandao ya TEHAMA , watunga sera na viongozi wa teknolojia wanakutana Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya Jukwaa la Utawala wa Mtandao wa Afrika (AfIGF). Mkutano huo unalenga katika kupanua ufikiaji wa mtandao, kudhibiti AI Akili Mnemba , na kuimarisha usalama wa mtandao ili kuendesha mageuzi ya kidijitali ya bara hili.
 
Back
Top Bottom