Kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa?

Just pride tu kuwa wazazi wangu walizaa mtoto basi na me nikiwa naye kama wazazi wangu. Ni kama repetitive pridd tu.
 
Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Every species does everything it does to stay alive. Every species does everything possible to pass on their genes

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa inaonekana mbinafsi sana... hivi ulivovikuta duniani imagine wazee wangesema waviharibu ingekuaje
 
Umejibu kwa mhemuko, swali ni kiumbe yyoyote yule anapata faida gani akizaa mtoto. Achana na kujikita kwa binadamu tu.

Yaani kwa mfano, ule mwembe unazaa maembe ambayo ndani yana mbegu ambazo zikiota zinakuwa mwembe mwingine. Sasa ule mwembe uliozaa maembe unapata faida gani endapo lile tunda la embe litaota na kuwa mwembe?

Mnyoo jnapata faida gani ukizaa kimnyoo kingine kidogo?

Mjusi anapata faida gani akizaa kamjusi kengine kadogo? Nk

Tungoje Majibu, Bila Jazba, Kejeri, Mihemko, Hasira
 
Tunazaana kwasababu tunakufa.Aliyeumba viumbe hai vinavyokufa aliweka uzao ndani ya hivyo viumbe.Kwahiyo kufa ndiko kunakoongoza uzao ulioko ndani ya viumbe hai.Kwahiyo viumbe wanaokufa wanapambana wasitoweke kwenye uso wa dunia kwakuakikisha wanazaana.Ni vita kati ya kifo na uzazi.Na hilo ni jambo la asili ambalo binadamu pamoja nakujaribu kuliingilia bado hataweza kulikomesha kwasababu akikomesha kuzaa maana yake kifo kitakua kimeshinda na matokeo yake binadamu atatoweka duniani.Kama kungekua hakuna kufa pia kungekua hakuna kuzaana.Tungeumbwa wengi alafu tukaishi tu.ila waliumbwa wachache wakawekewa kifo na uzazi ili iwe ni vita kati ya kuwepo au kupotea.Kwahiyo kuzaa kuna maana kubwa sana kiuzao kuliko faida ya binadamu mmoja mmoja.
Kwani binadamu tukitoweka duniani hasara yake ni nini?
 
Mwili wa binadamu na viumbe wengine wote unahangaika sana na mambo mawili. Kusurvive na kuzaliana. Sasa najiuliza kuzaliana kunamsaidia nini kiumbe anayezaa. Kuendeleza kizazi cha ng'ombe, kunamsaidia nini ng'ombe anayezaa. Binadamu walioishi miaka ya BC huko, wanafaidika vipi na kuendeleza uzao wa binadamu? Kungekuwa hamna kufa ningeweza kidogo kuelewa.

Zaidi naona uzazi unamnyonya mzazi kiafya, kichumi nk. Kuzaliana kunamsaidia nini anayezaa?
Viongozi wa Kanisa katoliki Wana majibu sahihi na biashara hii waliikimbia kuanzia masister,mabrother , mapadre,Maaskofu hadi papa.

Hii biashara hazilipi mkuu
 
Hakuna faida yoyote anaipata:-

-Mende kumzaa mende
-Funza kumzaa funza
-Simba kumzaa simba
-Mwanadamu kumzaa mwanadamu

Tunatekeleza maagizo ya aliyetufanya tuwe viumbe hai, yeye ndiye anayejua faida zake.

Unapotekeleza agizo linaweza lisiwe na manufaa ya moja kwa moja kwako.
 
Faidaaaa uliyopataaa ni kupunguzaa nyegeee.. Mpaka junior atakapokuja kutoboa kimaishaaaa ule mema ya nchii.
 
Back
Top Bottom