Kuwepo na Baraza la Uchumi, Biashara na uwekezaji la Taifa

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe kwenu wadau,
Natumai wote mu wazima na salama kabisa. Kama ilivyo kawaida, katika Kulwa hili kila Mwananchi ana uhuru wa kuchangia na pia kutoa mawazo yake, Naomba na mie leo nitoe tu mchango wangu kwenye mambo ambayo ningependa yawepo kwa mustakabali mpana wa nchi yetu

Kuna mambo nawish sana yawepo nchini, tena yawe kisheria. Najua wenye mapenzi mema akiwemo mzee JPM na wengineo wote watanielewa.

1. Kuwepo na Baraza la Uchumi, Biashara na uwekezaji la Taifa.
Kama tulivo la Baraza la Usalama la Taifa( ambalo najua lipo kisheria) napendekeza kuwe na hili Baraza pia ambalo kazi yake kuu itakuwa ni kumshauri raisi na serikali juu ya maamuzi na mambo yote ya kiuchumi, kiuwekezaji na Biashara.
Mapendekezo yangu ni kuwa, Baraza hili moja ya majukumu yake kimsingi na Kisheria ni iwe kufuatilia sera za uchumi duniani, maendeleo ya biashara, uchumi na uwekezaji duniani kote na kisha kumshauri raisi na serikali juu ya njia za kufuata, sera za kutunga na pia maamuzi ya kufanya.

Baraza hili napendekeza wajumbe wake wake Gavana wa bank kuu ya Taifa, Waziri wa fedha, Waziri wa Biashara. Napendekeza pia kuwe na wajumbe huru ambao ni Mjumbe mmoja kutoka makampuni ya kigeni yaliyowekeza Tanzania, Mjumbe mmoja anayewakilisha Mabenki ya Biashara, Mjumbe mmoja anayewakilisha Makampuni makubwa ya ndani, pamoja na wajumbe wengine 3 ambao Raisi atawateua kutokana na uzoefu wao kwenye biashara na masoko ya Kimataifa.

Wajumbe hawa wote watakaoteuliwa wafanyiwe vetting ya kiwango cha juu kabisa na mwishoni wahojiwe na kamati ya bunge kupima competency yao.

Kamati ya bunge ipewe mamlaka ya kumshauri Mh Raisi kumuondoa mjumbe ambae itaona hajakidhi vigezo.

2. Kuwepo na Baraza la Amani, Umoja na Mshikamano.

Hiki hakitakuwa kitu kipya sana kwa sababu tayari kwenye mikoa kipo kwa muundo wa kamati za dini za mkoa(kama sijakosea)

Baraza hili nalo litakuwepo kisheria na litahushisha uwakilishi wa dini na madhehebu kama ilivyo kwenye kamati za Mkoa.
Majukumu ya Baraza hili litakuwa kumshauri Mh. Raisi juu ya mambo yote ya Dini, umoja na mshikamano.

Litakuwa pia moja ya alama kuu za umoja wa kitaifa.


3. Baraza la Ardhi, Mipango na Matumizi bora ya Ardhi.

Hili Baraza litahusisha watu wenye weredi, uelewa na uzoefu mkubwa sana kwenye masuala ya Ardhi. Pamoja na waziri wa Ardhi na watu wanaotoka kwenye taasisi zinazohusiana na Ardhi ila litahusisha pia watu walioteuliwa na raisi na kupitishwa na Bunge.

Baraza hili litaishauri serikali na nchi juu ya mipango mizuri ya Ardhi, matumizi mazuri ya ardhi, mipango mizuri ya makazi, biashara na kupendekeza njia bora zaidi za kutumika.

Napenda kusema kuwa nimeona nishauri hivi na niweke hivi maana nimeona kuna tatizo kubwa sana nchini hasa kwenye mambo haya na viongozi na serikali wanaitaji msaada wa watu wenye weredi sana, Walio na uwlewa mpana wa dunia kwenye mambo mbalimbali ili nchi yetu iweze kusonga mbele vizuri tena kwa matokeo chanya zaidi.

Amani iwe nanyi
 
Mawazo mzuri sana...


Cc: mahondaw
Asante ndugu. Kuna sehemu naona tunatakiwa kwenda na nafikiri Hii ndo njia sahihi ya kufika huko. Vyombo hivi pamoja na Baraza la ulinzi na usalama wa Taifa ndo vitakuwa vyombo nyeti zaidi katika taifa hili na ndo vyombo vya juu kabisa vya kulishauri Taifa na nchi.


Naomba Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom