Kuweni serious na vijana, msiongee tu

Kuweni serious na vijana, msiongee tu

Arnold Kalikawe

Senior Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
152
Reaction score
378
Kila ninapopita nakutana na sakata la vijana, jinsi viongozi wanavyowazungumzia ni watu wasiojituma, wasiopenda kufanya kazi, yaani vijana wa Kitanzania wanaonekana hawapendi kazi kuliko vijana wengine duniani.

Viongozi walioajiriwa wanatuambia sisi tujiajiri. Mtu unaweza vipi kujiajiri pasipo mtaji? Kwanza kabla ya kumlaumu kijana hataki ajira ama kufanya biashara, kwanza tumpe kazi ama mtaji.

Siwezi kusema fulani hapendi kazi na wakati sijawahi kumpa ajira. Kwanza mpe kazi, ikimshinda ndipo utoke na kusema kijana fulani hapendi kazi. Sasa hata kazi sijampa halafu bado nasema kijana fulani hapendi kazi.

Zinapotokea nafasi za ajira 100, wanakwenda vijana laki moja, hivi ni kweli hawapendi kazi hawa? Si wangejitokeza vijana watano tu.

Badala ya viongozi kulaumu, kwanza watengeneze mianya ya ajira, nafasi ziwe nyingi halafu hapo sasa tuanze kuwalaumu hawa vijana wetu.

Mtu amemaliza chuo, hana mchongo, anatamani afanye biashara baada ya kuona ajira ngumu, lakini hawezi kufanya biashara kama hana pesa, ni lazima atafute pesa kwanza, je, ana njia ya kuzipata hizo pesa? Mikopo ipo, lakini ubaya wa mikopo anatakiwa kuanza kurejesha mwezi huo, na kwa kawaida ya biashara huwa inapewa miezi 3 mpaka kusimama. Je, huyu kijana tutakuwa tumemsaidia ama tumemuongezea tatizo?

Viongozi wengi wakishaona mambo poa, wanaongea lolote lile kwenye vyombo vya habari. Mtu tangu amezaliwa, yupo familia ya kishua, akaajiriwa na chama, hajapitia hata msoto halafu baada ya kutusua, anaibuka na kusema vijana hawajitumi, hawajishughulishi, vijana wanazingua.

Ukitaka kumpima kijana kama anapenda kazi ama la, kwanza mpe hiyo kazi, ukitaka afanye biashara, mpe pesa, usimkopeshe, pia mpe na mawazo ya biashara. Chukua hii milioni tano, kafanyie hiki na kile, ama kama ana wazo lake, mnakaa meza moja na kulijadili hilo wazo.

Sasa hujawahi kumpa kijana ajira wala mtaji halafu unasema vijana hawapendi kazi na hawajitumi. Huwa napata walakini nao hawa viongozi wanaosema hivyo.

1697546829691.jpg
 
kweli hawafanyi wanawaza mali za haraja huku hawajui.kutafuta wanabet kuka kaaa kaaa tu kuwaza starehe kuvuta mibangi kunywa mipombe mishisha kufanya umalaya Hadi K ni pesa
 
Back
Top Bottom