Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Kuweni makini, utapeli mpya umeibuka Dar

Watu hawa binafsi huwa siwapi nafasi ukinipigia simu sikujui,hunijui mimi sio muuza au mnunua madawa,mwisho wa stori simu inakatwa hapo hapo na hautonipigia tena in short simple rule" i dont mess with any unknown person"
 
Usanii huu umetumika sana, hii ni zaidi ya mara kumi nasikia watu wakishuhudia kuibiwa kwa namna hii. Tuwe macho
 
Leo kuna mmoja kanipigia simu kwa mtindo huohuo akijifanya tulipotezana siku nyingi. Matokeo yake akajichanganya akadai tuliwahi kuishi wote makongo. Nikamwambia mbona mimi sijawahi kuishi makongo? Akajibaraguza baadaye akasema "mimi ndio niliwahi kuishi makongo" yaani yeye mwenyewe. Nilipoona anaanza story za kujifanya ananijua sana nikamuuliza "kwahiyo?". Akanijibu ngoja nikuunganishe na bosi wangu kuna dili anataka akuunganishie. nikamuuliza Dili gani?" akaniambia kuna biashara ya ku supply chemicals". Nikamwambia usinipotezee muda sijawahi wala siko iterested kufanya biashara hiyo. Akajua nimeshastuka, akakata simu. Don't give them a chance. Tufanye kazi jamani, hata zege tukabebe lakini sio kutegemea kupata hela kirahisirahisi tu utapoteza mpaka nauli ya kurudi kijijini kwenu.
 
Maskani yao kwa dar ni airport wanawadanganya wanatokea ngara kwa wakimbizi na wanataka hizo dawa kwa ajili ya kuhifadhia nafaka
 
Believe me bado kuna watu wan fall into TRAPS for Nigerian scam letters! Kwamba mimi ni mtoto wa fulani ninataka unisaidie ku transfer pesa USD $ 1,000,000,000,000 ktk account yako nitakupatia comission ya 20%. Halafu unaambiwa utume processing fees $ 5000 ya bank! Ukituma tu $ 5000 ndiyo mwisho wa mchezo unakuwa UMETAPELIWA.
 
Hawa matapeli wamecharuka sana, ila cha ajabu unaweza ukakuta mtu amesoma hii post but still anaingizwa mjini.
 
Bro huo utapeli wa long time kitambo!! anyway umesema upo ZNZ vile eeh! nilisahau!
 
Ni utapeli mpya kwa wewe,lakini naamini na wengine ambao walikuwa hawajauikia umewafumbua
 
Nilikua njiani naelekea ofisini kwangu, nikiwa mitaa ya Darajani Zanzibar simu yangu iliita aliyenipigia alijitambulisha na nilikua simjui, alisema yupo Mkoani Kigoma anafanya kazi shirika moja la kimataifa, alinieleza anahitaji mtu wa kushirikiana naye katika mambo ya kibiashara anayetoka Zanzibar, alidai alipatiwa namba yangu na moja kati ya rafiki zangu wanao ishi Uk, na hakutaka nimuulize niliendelea kumsikiliza.

Akaanza kunielekeza anafanya Biashara ya kununua Product ambayo inahifadhi vyakula visiharibike na akanipatia namba ya mtu anayehusika katika utengenezaji wa production na jina lake akadai anaitwa Ibrahim na anapatikana Mahonda Zanzibar, akaniambianimpigie Ibra kumuuliza kama hiyo Production ipo na inapatikana kwa bei gani, nilimpata Ibrahim na akanieleza wanazo bidhaa kutoka ncho tofauti lakini best zinatoka Sweeden na bei yake kwa chupa 2 ni T shs 1,200,000/= nikamjibu yule jamaa aliyenitambulisha kwa Ibra kwamba bei yake ndio hiyo, baada ya hapo akaniambia kwamba pia wapo mabosi wake wa kizungu wamefikia Zamani Kenpisky Hotel Pwani Mchangani wananunua hiyo bidhaa kwa bei ya juu sana mara 2 ya bei ya kununulia, wakati nawasiliana na hawa jamaa tokea dakika ya kwanza niligundua kwamba hawa ni matapeli na nilichukua hatua za kuripoti tukio hili kituo cha Polisi na walifika kwa wakati nikawa nawashirikisha katika mawasiliano na hawa matapeli.

Polisi niliwapatia namba za simu za hawa jamaa wakaweza kuzifanyia utafiti na wakagungua wenye kuzimiliki, na sasa baada ya muda mfupi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwamba anaitwa Fred yupo Kenpsky na ameelekezwa kwangu kuja kununua Product mimi sikujivunga nikamwambia zitapatikana ndio hapo akaniambia kabla sijapeleka mzigo nimpelekee sample 1 pair ili akiridhika nao ndio tunaondoka pamoja na kwenda kuchukua mzigo wote.

Nikamweleza yule jamaa aliyenipigia simu mwanzoni kwamba wanunuzi wanahitaji sample wakiridhika ndio wanunue mzigo wote, hivyo akaniambia niwasiliane na Ibra kuhusu sample nikampigia akaniambia beio yake ndio hiyo aliyoniambia hapo juu Milioni moja na laki mbili, nikamjulisha jamaa akaniambia nifanye maarifa nipeleke hizo pesa.

Nikawaeleza Polisi tukaweka mtego baada ya muda kidogo nikawaambia kwamba fedha tayari waniletee mzigo, wakanielekeza walipo wakaniambia wapo Kibweni tukaenda mimi nilitangulia na polisi wakiwa nyumba yangu kwa umbali kidogo, nikapiga simu akaja kijana mmoja akaniuliza ni wewe niliyeagizwa kuhusu mzigo nikamwambia ni mimi na mzigo uko wapi nikupatioe hizo fedha? akaniambia nimsubiri kidogo akaufuate niliendelea kusubiri pale na kupiga simu hakutokea baadae alizima simu kabisa.

Nikawaarifu polisi kwamba jamaa wameshtuka nikarudi ofisini kwangu. nilichoamua kufanya baada ya hapo niliwapigia simu wale jamaa wote tuliokuwa tunawasiliana kwamba nawashukuru sana mzigo nimeupata na tumeshafanya biashara nimemkabidhi jamaa Milioni moja na Laki mbili ispokuwa jamaa aliyepokea pesa alitaka wale jamaa wote wasijue kama tayari ameshapokea fedha.

na nikawashukuru sana sikujua kilichoendelea baada ya hapo, hii ni tahadhari natoa kwa wenzangu wa JF na watanzania tuwe makini na tujiepushe na tamaa za kijinga tutaingizwa mjini.

nawasilisha.
Polisi ni sehemu ya mtandao, ukiwajulisha tuu, wao wanapewa taarifa kuwa wanafuatiliwa !
 
hawa wapumbafu walinical huyo mzungu wao anaongea kingereza fake nikawatel wajipange, wapumbafu wanatumia no. zinafanana eti za dr. na yao no.zao 0713877573/0713877571.nikatrace mwenye no inayoishia 71 anaitwa pamela n 73 patric amound no zimesajiliwa hivyo...bt sikufanikiwa kuwapata direct naombei tushirikiane tuwatie nduvuni..tuwape dozi tu..hali ya maisha tight harafu wapumbavu kadhaa wanazingua kila siku..hakuna kurudi nyuma wanajamii.
 
There you are my friend! Nimepata barua hizo ya 20 kwa miezi mitatu kupitia mtandao wa netlog. Wengi mabinti warembo wanajitambulisha kama wakimbizi wanaoishi Dakar-Senegal na pia watoto wa wanasiasa au wafanyabiashara maarufu ambao ni marehemu. Wanaomba friendship kisha wanataka uwe trustee ktk fund transfer kutoka ya kimagharibi. Mara nyingi processing ipo in term of dollar or pound kama 2000,5000 nk. Barua ya mwisho nimepata jana ya binti aitwaye Peace Ndadaye anaomba nimsaidie kutransfer us dollars 7000000. Chekecha bongo ooh! Namzungusha mpaka ajue mie mzee wa chai.
Believe me bado kuna watu wan fall into TRAPS for Nigerian scam letters! Kwamba mimi ni mtoto wa fulani ninataka unisaidie ku transfer pesa USD $ 1,000,000,000,000 ktk account yako nitakupatia comission ya 20%. Halafu unaambiwa utume processing fees $ 5000 ya bank! Ukituma tu $ 5000 ndiyo mwisho wa mchezo unakuwa UMETAPELIWA.
 
Nilikua njiani naelekea ofisini kwangu, nikiwa mitaa ya Darajani Zanzibar simu yangu iliita aliyenipigia alijitambulisha na nilikua simjui, alisema yupo Mkoani Kigoma anafanya kazi shirika moja la kimataifa, alinieleza anahitaji mtu wa kushirikiana naye katika mambo ya kibiashara anayetoka Zanzibar, alidai alipatiwa namba yangu na moja kati ya rafiki zangu wanao ishi Uk, na hakutaka nimuulize niliendelea kumsikiliza.

Akaanza kunielekeza anafanya Biashara ya kununua Product ambayo inahifadhi vyakula visiharibike na akanipatia namba ya mtu anayehusika katika utengenezaji wa production na jina lake akadai anaitwa Ibrahim na anapatikana Mahonda Zanzibar, akaniambianimpigie Ibra kumuuliza kama hiyo Production ipo na inapatikana kwa bei gani, nilimpata Ibrahim na akanieleza wanazo bidhaa kutoka ncho tofauti lakini best zinatoka Sweeden na bei yake kwa chupa 2 ni T shs 1,200,000/= nikamjibu yule jamaa aliyenitambulisha kwa Ibra kwamba bei yake ndio hiyo, baada ya hapo akaniambia kwamba pia wapo mabosi wake wa kizungu wamefikia Zamani Kenpisky Hotel Pwani Mchangani wananunua hiyo bidhaa kwa bei ya juu sana mara 2 ya bei ya kununulia, wakati nawasiliana na hawa jamaa tokea dakika ya kwanza niligundua kwamba hawa ni matapeli na nilichukua hatua za kuripoti tukio hili kituo cha Polisi na walifika kwa wakati nikawa nawashirikisha katika mawasiliano na hawa matapeli.

Polisi niliwapatia namba za simu za hawa jamaa wakaweza kuzifanyia utafiti na wakagungua wenye kuzimiliki, na sasa baada ya muda mfupi nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwamba anaitwa Fred yupo Kenpsky na ameelekezwa kwangu kuja kununua Product mimi sikujivunga nikamwambia zitapatikana ndio hapo akaniambia kabla sijapeleka mzigo nimpelekee sample 1 pair ili akiridhika nao ndio tunaondoka pamoja na kwenda kuchukua mzigo wote.

Nikamweleza yule jamaa aliyenipigia simu mwanzoni kwamba wanunuzi wanahitaji sample wakiridhika ndio wanunue mzigo wote, hivyo akaniambia niwasiliane na Ibra kuhusu sample nikampigia akaniambia beio yake ndio hiyo aliyoniambia hapo juu Milioni moja na laki mbili, nikamjulisha jamaa akaniambia nifanye maarifa nipeleke hizo pesa.

Nikawaeleza Polisi tukaweka mtego baada ya muda kidogo nikawaambia kwamba fedha tayari waniletee mzigo, wakanielekeza walipo wakaniambia wapo Kibweni tukaenda mimi nilitangulia na polisi wakiwa nyumba yangu kwa umbali kidogo, nikapiga simu akaja kijana mmoja akaniuliza ni wewe niliyeagizwa kuhusu mzigo nikamwambia ni mimi na mzigo uko wapi nikupatioe hizo fedha? akaniambia nimsubiri kidogo akaufuate niliendelea kusubiri pale na kupiga simu hakutokea baadae alizima simu kabisa.

Nikawaarifu polisi kwamba jamaa wameshtuka nikarudi ofisini kwangu. nilichoamua kufanya baada ya hapo niliwapigia simu wale jamaa wote tuliokuwa tunawasiliana kwamba nawashukuru sana mzigo nimeupata na tumeshafanya biashara nimemkabidhi jamaa Milioni moja na Laki mbili ispokuwa jamaa aliyepokea pesa alitaka wale jamaa wote wasijue kama tayari ameshapokea fedha.

na nikawashukuru sana sikujua kilichoendelea baada ya hapo, hii ni tahadhari natoa kwa wenzangu wa JF na watanzania tuwe makini na tujiepushe na tamaa za kijinga tutaingizwa mjini.

nawasilisha.

nyingine ni hii hapa.

Wewe ni mtoa huduma, unauza mathalani duka. Anakuja jamaa anachagua kitu anakipenda, anapoulizia bei yake, unampa bei labda tuseme laki mbili, yeye ana 50,000/= out of 200,000/= hivyo ana upungufu wa 150,000/=. Anakwambia bidhaa yako nimeipenda, lakini nimepungukiwa na cash money ILA NINA PESA YA KUTOSHA M-PESA au mitandao mingine. Anakwambia umpe bidhaa halafu yeye anakulipa kwa M-PESA, unakubali, anakulipa kweli kwa M-PESA tena kuonesha kuwa ni muungwana, anakuongezea na 5,000/= eti ya usumbufu wa kutoa pesa aliyoirusha kwako kama malipo ya huduma aliyopokea kwako. Unaletewa ujumbe kuwa umepokea kiasi fulani toka kwa fulani, unaridhika na kumpa bidhaa yako mnaagana anaondoka.

Baada ya mda unakuta ile pesa haipo, imesharudishwa kwenye nayo, yaani aliyekurushia. Anachokifanya aliyerusha pesa, anawapigia VODACOM M-PESA, anawaambia alikuwa anatuma pesa kwenda namba fulani, lakini akakosea namba moja ikaenda kwa mtu asiyemkusudia, hivyo anaomba arudishiwe pesa yake. Vodacom baada ya kumwuliza pin code, wanaamini jtapeli alikosea na kweli wanamrudishia pesa zake wewe unahesabu maamuvu.

CYBER CRIME IS NOW RAMPART IN OUR COMMUNITY, TAKE CARE, TOA TAARIFA POLISI WANAWEZA KUSAIDIA KUPITIA KITENGO CHAO CHA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO
 
there you are my friend! Nimepata barua hizo ya 20 kwa miezi mitatu kupitia mtandao wa netlog. Wengi mabinti warembo wanajitambulisha kama wakimbizi wanaoishi dakar-senegal na pia watoto wa wanasiasa au wafanyabiashara maarufu ambao ni marehemu. Wanaomba friendship kisha wanataka uwe trustee ktk fund transfer kutoka ya kimagharibi. Mara nyingi processing ipo in term of dollar or pound kama 2000,5000 nk. Barua ya mwisho nimepata jana ya binti aitwaye peace ndadaye anaomba nimsaidie kutransfer us dollars 7000000. Chekecha bongo ooh! Namzungusha mpaka ajue mie mzee wa chai.

mie nilipokea wengi wakiahidi kunipa pesa nzuri. Tunashindana sehemu moja. Ilifikia sehemu mpaka nikafungua akaunt standard chartered bank, lakini walipotaja kuwa ili hizo pesa zitumwe ni lazime nitume kama dola 400 za kumlipa lawyer, nawaambia mimi nina shida nyingi sana, mke wangu kalazwa, kipato changu kwa mwezi ni dola 100, hivyo itanigharimu miezi 4 kukusanya kiasi chao. Wanasepa jumla
 
Wana JF hii ni kweli hata mimi imenitokea kama wiki mbli zimepita,jamaa alijatambulisha anafanya kazi WFP-Mtwara akaniambia anatafuta dawa ya kuwekea kwenye maghala yao,akasema yeye huwa ana wazungu wake ambao ni wa norwey,jamaa alionekana kunifahama mpaka wazazi wangu.nikmuliza tulionana wapi?? jamaa anataja kila kitu.. akawa anahitaji a/c yangu nikamwambia ilishafungwa...juzi tena nikapigiwa cm kuwa kuna tender ya kuwafundisha kiswahili wakurugenzi wa Kampuni ya AFRICAN BARICK GOLD kwa muda wa miezi 3 kwa gharama ya 150mil.
 
AKikupigia akwambia anafanya kazi World Food Progrmmme, Ngara; mjibu sikusikia vizuri, umesema unafanyakazi Angaza ? Njoo hapa, Central Police Station tuongee zaidi.
 
Mbona upo siku nyingi sana. Nimeshatafutwa na watu kibao wanipe deal hazina mbele wala nyuma.
 
Back
Top Bottom