Kuweka salio kupitia modem ya tigo

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984
jamani naombeni msaada kama kuna mtu anafahamu namna ya kuweka salio kupitia modem hasa modem ya tigo maana ndio naitumia.
napata shida sana kuweka line kwenye simu halafu unaweka salio then ndio unajiunga vifurushi vya internet.sasa nikifahamu namna ya kuweka moja kwa moja kupitia modem itakua rahisi sana na haileti usumbufu.

tiririkeni wadau.......
 
nelly poul , Ni baadhi ya modem dashboard ndio zinakubali USSD code. Kama modem yako ni huawei kama hii pichani click hapo kwenye icon "Buy Package"
- Hapo waweza ongeza salio
- Au ukajiunga na kifurushi kwa kutumia ussd code husika
ti_Go.jpg
 
utahitaji dashboard yenye uwezo huo.

una rafiki yako anayo dashboard ya aina hiyo? muombe modem yake eka dashboard yake kwako halafu tumia hio

au jaribu hii
https://m.box.com/shared_item/https://www.box.net/shared/0taesd40ye

Link naona ime typiwa vibaya hiyo

https://app.box.com/shared/0taesd40ye

sijui itakua ni mobile partner ya zamani(muonekano kama Modem za CDMA za zantel) lkn yenye USSD commands,ukiachana na hii yenye wifi hotspot ambayo sijawai pendezwa nayo kabisa!
 
driver za modem zipo?

Natumia Mobile partner tayari sema haina USSD option[Attached image]

Tatizo la hiyo dashboard ukicheki picha vizuri ni kwamba hai detect modem

Na kitu cha ajabu nilitegemea iombe ku Replace MP ya awali lakini haijfanya hivo na ziko mbili

MEViO2.png
 
Duuh kumbe wanazi Disable kwenye XML files nimecheki video nimecheka

Means hata dashboard ya mitandao yote zina support Phone Calls na USSD sema wana disable somewhere

3EAnj0.png


 
Nilitaka kuja na swali kama hilo jana ila langu lilikuwa msaada wa kupata source code ya huawei dashboard ili nitengeneze simple application ya kurecharge na kununua internet bundle. Ila wakati nataka kuuliza wsali langu nikaishia hapa Direct links mega thread x2x0x1x5x

so please mwenye maujanja ya Source Code ( Vb au C# ) anidondoshee kidogo maana niliachana na projects za modem kitambo kidogo,
 
jamani naombeni msaada kama kuna mtu anafahamu namna ya kuweka salio kupitia modem hasa modem ya tigo maana ndio naitumia.
napata shida sana kuweka line kwenye simu halafu unaweka salio then ndio unajiunga vifurushi vya internet.sasa nikifahamu namna ya kuweka moja kwa moja kupitia modem itakua rahisi sana na haileti usumbufu.

tiririkeni wadau.......
Pole kwa usumbufu! Njia nyingine ni kuwa na line 2 za tigo ambapo moja inakaa kwenye modem permanently. Na hiyo nyingine kwenye simu. Haina haja ya kuitoa. Sana sana utatumia line hiyo yako nyingine ya tigo kununua any bundle you want through option ya "mnunulie rafiki".
1459312112169.jpg
1459312143289.jpg
1459312151029.jpg
1459312154630.jpg
 
asanteni sana aise mungu awabariki wote. nimenufaika na majibu na yamenisaidia sana na nimeweza kufahamu
vitu vingine nilikua sijavifahamu.
 
mbona yangu hamnisaidiii please wajameni nipeni tafu kidogo,
Kama lengo ni kutia Salio *102*namba _ya_voucher# na kujiunga vifurushi kama *148*00# and so forth ambazo zinaitwa USSD Commands.Waweza kuyafanya tu kwa kuanza Kutafuta Serial Port kama ipo Open kwenye PC au inatumika na dashboard
Ukishajua kama ipo Open labda ungependa u connect kwa hiyo Serial port afu utume AT Commands zenye hizo strings zako.

Kwa hivo unaitaji tu Kujua Serialport class library na jinsi ya kuzituma hizo AT Commands nimeona zile Program zako za blackpanter naamini zina involve hicho kitu i.e Serial Comminication + AT commands

Waweza google mifano iliyoko available ya kutuma hizo AT Commands then uka Remodify.
mifano: How to retrieve response result in sending USSD commands in c#?
 
First I thank you for raising your concerns
Mkuu Njunwa Wamavoko
Kuna pahali pananichanganya kwenye masuala ya ussd, sms dpu, baadhi ya modems zinataka u- Encode "*148*00#" to PDU format, which is "AA180DA782C146" tofauti na How to retrieve response result in sending USSD commands in c#? ame send straight text. yaani
"AT+CUSD=1,\"*148*00# ( njia hii napata error )

Baandi ya modems na ambayo ninayo kwa sasa ( ile ya Tigo ya lte ) zinaleta majibu ya USSD kwa njia ya PDU encoding. ( hapa ndipo panaponipasua kichwa )
natuma command hii AT+CUSD=1,"AA180DA782C146",15 napata OK . ila output yake inanichanganya kidogo, inakuwa katika mfumo wa DPU badala ya kuwa hivi.

1.OFA MAALUM
2.MiniKabang
3.Tigo-Tigo Xtreme
4.Vifurushi vya Kimataifa
5.Internet vifurushi
6.Music
7.Huduma Nyingine
8.Huduma kwa wateja

output yangu inakuwa hivi,

D4E4F1099A229F5045CCF5340641CD6090596D2A64AE66DA9D5E86C561F759317351D3E7778B9A3EBF4158BABCDC2E83143497356DAECBEB73741A64CF8741CB743B4C0FA7CD6145CD9574D3CB7277990EB2A7CD75797D8E4E83143657B33E4F8F153717B24EAEB7C320673EED3EA7DD6505CE85AC93EBED30687D0F83EE617A591D06",15

Najua nitahitaji ku encode to readable text ila PDU yangu naona inamatatizo ndio maana nachanganyikiwa
Ila
Thank you for your kind cooperation
 
Back
Top Bottom