Kuwaita wafadhili wetu “mabeberu”, kabla hatujaweza kujitegemea, ni ushamba unaoweza kuliangamiza Taifa tusipokuwa makini!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,990
22,523
Wanajamvi,

kuwaita wafadhili wako na wahisani “mabeberu”, na kuitumia hiyo kauli mbiu kwenye siasa, ni sawa na kuwalisha chuki wananchi dhidi ya wafadhili, kwa maslahi ya kisiasa, yale ya binafsi pamoja na chama. Huu ni ushamba mkubwa na wa hatari kabisa kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Ningeunga mkono jitihada hizo za kumtukana mamba, endapo ningeona kuwa tumeshauvuka mto!

Hili ni ushamba kwasababu ni la kujitakia tu. Sawasawa kabisa na kujipiga risasi ya mguu mwenyewe, huku ukichekelea! Sasa kama kura zote ziliibiwa kiasi hicho, na hili wahusika walilifahamu hata kabla ya kampeni kuanza, kulikuwa na sababu gani sasa za kuweka uadui dhidi ya wafadhili na wahisani kwa kuwaita mabeberu wenye nia mbaya na maendeleo ya Taifa letu? Tena hata wakati wa kuwazungumzia wagombea wengine!

Matokeo yoyote yale mabaya kwa Taifa letu, yatakuwa yamesababishwa moja kwa moja na bila chembe ya shaka, na genge la uhalifu na kigaidi linalojificha chini ya mwavuli wa chama cha siasa!

Sioni jambo lolote kubwa ambalo limebadilika kutoka tawala za ccm zilizopita, zaidi ya jitihada za kuzima sauti mbadala na zenye kufichuwa ufisadi ndiyo kuwa zinazidi! Hivyo genge hilo, linatumia propaganda ya mabeberu, na kuligawa Taifa kwa tamaa zao! Ili kuendelea kulifisadi Taifa tu.

Uzalendo kwa Taifa, ni kuiondoa na kuikataa CCM kwa nguvu zetu zote. Hapo ndipo Taifa litapona, siyo kinyume chake.

Sasa tunaona hata tatizo la ugaidi nchini mwetu likianza kushamiri, haswa kule Mtwara, ambapo CCM hawana njia ya kukwepa lawama.

Sehemu ambazo ugaidi hukuwa, maisha ya wananchi wa maeneo hayo na haswa vijana huwa magumu sana, na hivyo kuwa rahisi kuingia kwenye ugaidi.

Hili suala na sehemu nyingi tu Tanzania, lingeweza kumalizwa na muundo mpya wa serikali. Hapa ya majimbo ingefaa zaidi.

Kwasababu wananchi huwa wanajiskia huru, na pia kunufaika moja kwa moja na rasilimali zinazowazunguka, na hivyo kuwaletea maendeleo yanayoleta unafuu kwenye maisha yao ya kila siku. Bila kusubiri huruma za aliyeko magogoni nk!

Lakini ccm wamezoea kukusanya tu mapato na kufanya ufisadi bila kuwajali wananchi. Kwingine inawalazimisha wananchi wawe na itikadi ya ccm ndipo wapelekewe maendeleo. Je ina maana hayo maeneo haya kuwepo wakati wa chama kimoja?

Sasa ukizingatia kuwa tunaweza kuwekewa vikwazo, kwasababu ya yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na jitihada za kuminya demokrasia, watakaoendelea kuteseka bila sababu ni wananchi ambao wengi ni masikini.
 
Suala la ugaidi, linaweza kumalizwa haraka sana kwa kuwa na serikali za majimbo.
 
Ndiyo. Mzee Nyerere aliwaita mabeberu wakaiangusha bei ya zao la mkonge halina bei hadi leo. Alipokuja Mzee Mwinyi akabadilisha jina wakawa wahisani au wafadhali, Mzee Mkapa akawaita wawekezaji. Mzee Kikwete akawaita wadau wa maendeleo sasa awamu hii tunaanza kurudi kule kule kwa Nyerere ambaye walimtaiti mpaka akaukimbia urais
 
Ni elimu yako ndogo tu ndio inakufanya uone neno beberu ni tusi ,malaumu babako kwa kushindwa kukupa elimu ya kutosha

Capitalism -ubapari
Capitalist -bepari
Imperialism -ubeberu
Imperialist -beberu
Socialism -ujamaa
Socialist -mjamaa

Kwa kuwa wao hutuita wajamaa nasi tunawaita mabeberu (imperialists -mabaeberu)

Imperialism is highest level of capitalism -ubeberu ni ubepari uliokomaa

USSR
 
Unajua maana ya BEBERU? why tusiwaite hivyo hali ya kuwa ni kwel Mabeberu? Nawasiwasi na Elimu yako.. huwenda huufahamu Ukoloni ni nini.. na wala hujui Ukoloni mambo leo ni kitu gani..

Inasikitisha
Tulia basi unielemishe...maana ya beberu ni nini? Kwa jinsi linavyozungumzwa, ni kama tusi baya kabisa! La kutosha kabisa kuwashawishi wananchi wawachukie wafadhili na wahisani wao kabla ya kuweza kujitegemea?

Huo ubeberu wao na ukoloni mamboleo umeanza lini Tanzania? Niwekee mfano tafadhali.
 
Ni elimu yako ndogo tu ndio inakufanya uone neno beberu ni tusi ,malaumu babako kwa kushindwa kukupa elimu ya kutosha

Capitalism -ubapari
Capitalist -bepari
Imperialism -ubeberu
Imperialist -beberu
Socialism -ujamaa
Socialist -mjamaa

Kwa kuwa wao hutuita wajamaa nasi tunawaita mabeberu (imperialists -mabaeberu)

Imperialism is highest level of capitalism -ubeberu ni ubepari uliokomaa

USSR
Elimu yako kubwa ndiyo imekufanya uone siyo tusi? Hivi kama wewe siyo kilaza wahed, hapa sijui umlaumu mamako? Mkapiga risasi mnayesema anashirikiana na “siyo tusi”. Wewe akili yako inakutosha wewe peke yako tu. Hapa unaniwekea usiku tu.
 
Unajua maana ya BEBERU? why tusiwaite hivyo hali ya kuwa ni kwel Mabeberu? Nawasiwasi na Elimu yako.. huwenda huufahamu Ukoloni ni nini.. na wala hujui Ukoloni mambo leo ni kitu gani..

Inasikitisha
Sasa kama hilo ndiyo tatizo, si usubiri uweze kwanza kujitegemea ndo uanze kutukana? Wengine kina USSR , wanasema siyo tusi, si unaona akili zenu zilivyo?
 
China imeendelea sana
Ilipewa misaada?
Badilisha mtazamo
Umatonya ni fikra mgando
China hawakufanya ujinga huu. Walimweka karibu zaidi mzungu na kumuibia teknolojia ndiyo maaana wakafikia hapo walipo. China hawakufuata “isolationism”

Sikubaliana na umatonya, lakini huu ni ushamba ambao utaligharimu Taifa.
 
Wazungu sio mabeberu ila WALE wanaotaka kuinyonya NCHI ndio mabeberu ila wale ambao wanakuja kuwekeza nchini na kufuata taratibu za kunufaisha nchi bila kuinyonya hao ni MABEBERU TU.
Hata wanaofanya mambo hayo nchini mwetu dhidi yetu, tusiwaite mabeberu? Hao hao mafisadi wa ccm walio na akaunti zenye pesa ya kufuru nje ya nje sasa hivi mmewasahau kwasababu tumepata rais anayependa kula ugali samaki na asiyefahamu lolote kuhusiana na siasa za kimataifa?
 
Wabongo wanapenda kupetpet mambo.

Mfano neno zeruzeru lipo kwenye kamusi ya TUKI miaka yote ila kwa sasa wanasema ni unyanyapaa badala yake wanarukaruka tu mara,"albino" nalo wakaliacha,"ulemavu wa ngozi",wakaliacha,"wenye albinism" wakaliacha na sasa wanaita,"wenye upungufu wa melanin".

Kuukataa ukweli hakuufanyi uwe uongo bali ukweli uliokataliwa.

Wale jamaa ni mabeberu kwa matendo yao wala hawatukanwi ama kusingiziwa.
 
Mmeamua kupunguza mno uwezo wa kufikiri aisee!!

Nani kataja nchi na Kisha kusema nchi hizo ndio za mabeberu??
 
Mkuu yapo Mambo umeandika yamenigusa,mfano swala la mabeberu,asilimia KUBWA za hospital,mashule na majengo mengine yalikuwa yao, japo Kama serikali kwa Sasa asilimia KUBWA wanayatumia.

Hili jina beberu sio zuri linatuabisha watz ,kwa maana beberu kwa ni mbuzi dume, na hufika mahala Kama ni mbegu nzuri wenye mbuzi jike hupeleka kwa beberu ili apandwe Sasa ndugu Wana JF

Wale watusaidiao tunawaita mabeberu, na wamekupa msahada mkubwa tangu Uhuru na mh BASHIRU ni shaidi.
Swali
Je, watanzania wote bila kujali vyma,dini ,wadhifa wako katika jamii,baba au mama wa familia ,kijana tunapandwa na beberu? KWA maana nyingine sie ni mbuzi jike,maana mh jk aliwai sema ukutaka kula lazima uliwe!

Sasa miaka yote tumekula vingi vya hao muaitao mabeberu, Sasa maana yake ni Nini ,?

Ushauri
Turudishe kila kitu anzia tangu Uhuru then ndo tuwaite majina ya mahajabu vinginevyo kwa majina yenu hayo mnatuzalilisha watanzania, kwamba sie ni mbuzi jike na beberu yuko tiyari kwa kuja au kwenda wenyewe kupanda,STOP Mara moja huo msemo watanzania sio wa hivyo
 
Back
Top Bottom