Kuwafariji watu wa Chato sawa lakini si wale wa Kagera!

tulifanya makosa makubwa sana katika uchaguzi 2015, hatutakiwi kurudia makosa. kuna watu wameumbwa kuwa viongozi na wanaweza, ila kuna watu wengine wameumbwa kwa kazi nyingine tu ila si kuwa viongozi. wapo viongozi wengi tu serikalini ambao wameshika nyadhifa ambazo Mungu hakuwaumba nazo na wanalazimisha tu labda kwasababu imewadondokea kama ngekewa, kama wanafanyia majaribio kwenye maisha ya watu vile. hata hivyo, nampongeza magufuli, na ninamwombea Mungu afanye kazi kwa mapenzi ya Mungu.

Waliofanya makosa makubwa ni wale waliokubali kuzungusha mikono na kuimba jina la mtu lilete mabadiliko.Hawakuziamini akili zao,chama chao wala MUNGU wao,ila mmoja tu waliyemtukana usiku na mchana.Wakafagia na barabara ili mteule wao apite mahali safi,wana haki ya kulalamika.Walijitoa si haba kwa mtu si kwa nchi.

Watu hawa waliaminishwana bado wana amini kuwa ukiwa ndani ya CCM u mwovu sawasawa na shetani,ukihamia tu vyama wanavyoviamini kufumba na kufumbua unakuwa malaika.

Watu hawa hawakupimi kwa matendo yako bali hukupima kwa chama chako.Kwa habari ya Misiba sisi wote tunao changia humu naamini tu Watanzania ( kwa hoja inayojadiliwa sasa) nawataka kila mmoja ajitathmini mwenyewe amehudhuria misiba mingapi ya ndugu zake,jirani zake na hata asiowafahamu?

Nani kati yetu anaweza kumtembelea kila mwenye msiba . Waziri mkuu akienda si Serikali ? kama hata misiba ni mitaji ya siasa ,siasa na ife Tanzania.Tutafute biashara nyingine ya kufanya si maafa.
 
Back
Top Bottom