BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,124
Friday, December 30, 2016
Rais Magufuli awafariji majirani Chato
Kwa ufupi
Familia ya Manyama imefiwa na baba yao, Mbabe Manyama aliyekuwa maarufu eneo la Chato na familia ya Lufunga ambayo iliondokewa na baba yao, Mchele Lufunga.
By Baraka Rwesiga, Mwananchi brwesiga@mwananchi.co.tz
Chato. Rais John Magufuli, ametumia mapumziko yake ya mwisho nwa mwaka kuwatembelea na kuwafariji majirani zake waliofiwa na baba zao Desemba 27.

Rais Magufuli ambaye yuko nyumbani kwake Chato mkoani Geita, ametoa ubani wa Sh1 milioni na ng’ombe mmoja kwa kila familia.
Familia ya kwanza aliyoitembelea ni ya Lufunga ambaye ni jirani yake wanayetenganishwa na ukuta aliyefariki dunia katika Hospitali ya Wilaya ya Chato alikokuwa akipatiwa matibabu.
Pia, Rais Magufuli aliitembelea familia ya Manyama ambaye alifariki nyumbani kwake. Licha ya kuwa maarufu wilayani humo, Manyama pia alikuwa rafiki mkubwa wa baba mzazi wa Rais Magufuli.
“Msiba kama huu wa kufiwa na mzazi ambaye ni nguzo ya familia unapotokea, familia nyingi huanza kufarakana na kugawanyika. Naomba msifarakane ninyi wenyewe kwa wenyewe wala msifarakanishwe na watu,” amesema Rais Magufuli alipokuwa akiifariji familia ya Mbabe.
Akitoa shukrani kwa Rais, mdogo wa marehemu Lufunga, Charles Lufunga amesema familia imefarijika kutembelewa na kiongozi huyo na kuahidi kudumisha umoja na ushirikiano.
Mdogo wa Manyama, Theodatus Manyama amemhakikishia Rais Magufuli kuwa familia hiyo itazingatia ushauri wake kwa kuendeleza umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwao na kwa wote wanaowazunguka.