Kuwa ugenini mateso

Nashukuru Mungu yale yote niliyoyapitia kwa ndugu zangu yalikuwa somo kubwa mno katika maisha yangu ya sasa na ya baadaye, kwangu sasa imebaki kuwa historia na funzo kubwa ni kwamba, kaa na mtu yeyote vizuri kwa sababu hakuna aijuaye kesho yake!
 
wanawake sisi saa nyingine ni sumu kwenye familia za watu, nasema familia za watu maana wewe umeolewa ukaikuta. mwanamke unaoelewa unakuta watu wanaelewana kupita kiasi. wewe kidudu mtu unavuruga kuanzia mumeo na wazazi wake, mumeo na ndugu zake, mumeo na marafiki, halafu mnabaki wewe, yeye watoto wenu na ndugu zako!!! hivi hii inakuaje? na wako wengi wa aina hii. Jamani kama kuna wanawake walio hivi humu hebu tubadilike na waambie na wengine kua maisha haya ni ya kupita tu, vyakula hivi baada ya muda unaenda chooni kuvitoa. Kama unaishi na mtoto wa watu, wa ndugu yako au ndugu wa mumeo, ishi nae vizuri maana mara nyingi shida ndio inapelekea aje kukaa kwako. sidhani kama isingekua shida kuna mtu angetaka kupeleka mtoto wake alelewe kwingine. Kwani ukimpenda na kumthamini, utapungua wapi. akila chakula chenu, utafirisika? ikiwa huna roho ya imani, basi bora ukatae, kuliko kuishi na mtoto wa watu na umfanye mtumwa.
 
Mm nlikuwa nkibakiza ugali wanasema kula wote mjini hamna mashamba,unasaza sababu hujui bei ya unga!

Duh, .......... kweli hamjui mwenye njaaaa..

Nilikuwa nakaa kwa mamamdogo wakati na soma o-level day! Baada ya kugundua weakness yangu kwamba siwezi kula chakula chenye pilipili ilikuwa inasagwa kwa wingi na wakati wa kula inamwagwa kwenye mboga! Nilishindwa kuishi nikapata msamalia mwema mama mshiriki wa kanisa nilipokuwa nasali alinihost mpaka nikamaliza shule! MUNGU AMBARIKI TENA NA TENA na AMWONGEZEE UHAI MARADUFU NA MAFANIKIO ZAIDI

Ebana hiyo kali, yaani alikuwa analenga kwenye kidonda kabisa. Kuna watu wana roho mbaya zaidi hata wauza sumu

Mama mdogo au msamalia mwema

Wote.., Msamalia mwema ili one day na yeye atolewe, na Mama mdogo ili aone jinsi navyoneemeka (Ombea adui yako aishi miaka mingi...:violin:)
 
me nakumbuka niliwekewa maji ya kunywa kwenye chupa ya chai badala ya kwene jagi usipime mkuu
 
Jamani mnanikumbusha mbali. Nikakaa kwa ndugu fulani sabuni kila mtoto anayo yake akioga anaficha anakojua yeye - Naogaje? Dawa ya mswaki kila mtoto ana yake, napigaje mswaki? - Chumvi. Na ukichelewa kurudi mchana au usiku home unakuta chakula hakuna. Nilitia akili nakwambia.

Ila kukaa na wageni udhia na inakera mara nyingi sana. Wengine ndiyo wanakulaaa hawashibi wanamalizia watoto share, wengine wezi, wengine wabakaji, wengine wanakuchapia wanao. Ali mradi tu haujui nini unakaribisha nyumbani kwako.
 
wanawake sisi saa nyingine ni sumu kwenye familia za watu, nasema familia za watu maana wewe umeolewa ukaikuta. mwanamke unaoelewa unakuta watu wanaelewana kupita kiasi. wewe kidudu mtu unavuruga kuanzia mumeo na wazazi wake, mumeo na ndugu zake, mumeo na marafiki, halafu mnabaki wewe, yeye watoto wenu na ndugu zako!!! hivi hii inakuaje? na wako wengi wa aina hii. Jamani kama kuna wanawake walio hivi humu hebu tubadilike na waambie na wengine kua maisha haya ni ya kupita tu, vyakula hivi baada ya muda unaenda chooni kuvitoa. Kama unaishi na mtoto wa watu, wa ndugu yako au ndugu wa mumeo, ishi nae vizuri maana mara nyingi shida ndio inapelekea aje kukaa kwako. sidhani kama isingekua shida kuna mtu angetaka kupeleka mtoto wake alelewe kwingine. Kwani ukimpenda na kumthamini, utapungua wapi. akila chakula chenu, utafirisika? ikiwa huna roho ya imani, basi bora ukatae, kuliko kuishi na mtoto wa watu na umfanye mtumwa.

wanawake roho zenu mnazijua wenyewe, unaondoka kwa mtu unabaki kumkumbuka kwa mabaya tu!!
 
Nilikuwa nakaa kwa mamamdogo wakati na soma o-level day! Baada ya kugundua weakness yangu kwamba siwezi kula chakula chenye pilipili ilikuwa inasagwa kwa wingi na wakati wa kula inamwagwa kwenye mboga! Nilishindwa kuishi nikapata msamalia mwema mama mshiriki wa kanisa nilipokuwa nasali alinihost mpaka nikamaliza shule! MUNGU AMBARIKI TENA NA TENA na AMWONGEZEE UHAI MARADUFU NA MAFANIKIO ZAIDI

Aaamen
 
....ni roho mbaya tu za binadamu....nashukuru me sijapitia hayo ila nimeona wengi......kuna dogo mmoja zamani mtaani alikuwa anawekewa chakula pamoja na mbwa wale pamoja....imagine?sijui hata yuko wapi sasa najua atakuwa amekuwa mtu mzima

Mhh..hii dunia hii
 
Mie shem alininyanyasa kwa chinichini sn kwa kaka yangu wa tumbo moja.Bila kuwa mwenye sifa ya kuwa mkali ktk familia yetu ningeona chamoto.Ila ukali nilionao kwa wapuu ndio uliniokoa kwani najua hata bro alikuwa anamwambia ukimchezea huyo umeumia.Alishia kuniimbia tunyimbo tu.
 
Hicho ndicho kilichonifanya nisiende kukaa kwa watu maishani mwangu. Naelewa kuwa kuna wengi situation zinawalazimu kufanya hivyo. Ila kama ni kuchagua kwa kweli kukaa kwa watu tabu. Nakumbuka nilienda kumtembelea ndugu yangu Arusha, yani I had to pretend being a good girl. Kuamka saa kumi na mbili, wakati home kama siendi school nalala nitakavyo.

Kwa watu napiga kazi kweli kweli. Yani mpaka mtu unaaga wanakwambia njoo tena next holiday. Maana wanaona wamepata housegirl wa bure. Wengi hawalijuhi hilo kuwa huwezi kuishi maisha kama ya nyumbani kwenu ukiwa ugenini.

Kumbe ugenini kuna darasa na hakuna kudeka aisee.
 
sio wewe tu
wengi tumejifunza mengi ugenini...

Mimi kuna vyakula nilipokuwa mdogo nilikuwa sili
na home kwetu hatukuwahi kushinda bila kula

but kwa ndugu nilijifunza kula kitu na kushinda na njaa pia....

Siku moja kwa baba mdogo tumekaa siku nzima bila kula
ikawasili mihogo saa sita usiku.....tulii ilamba kama asali...

umenikumbusha mbali nilienda kuishi kwa ndugu hapa hapa dar familia yangu ilisafiri na sikuweza kuambatana nayo kwa sababu ya shule sasa kule kwa mama yangu mkubwa wanakula pamoja kwa sinia mi nilikuwa mdogo kama miaka 10 nikawaambia saa ya kula wanipakulie cha kwangu nimezoea kila mtu na sahani yake mama yangu mkubwa akasema kwenu mnakula kila mtu na plate yake kwasababu ni wachoyo siku ya kwanza nililala njaa ya pili ikabidi nile ila tonge mbili mara sinia nyeupe dah nilikonda
 
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.

Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.

kabisa. nakubaliana na wewe. wengi wao hapa wanaolalama ni sawa na hao unaowasema. wanakuja na kuleta amri zao kwenye nyumba za watu, wakionywa au kuwekwa sawa kuwa ishi maisha uliyoyakuta sehemu wanaona manyanyaso, muwe na shukrani msipende kupeleka sheria zenu kwa watu na hiyo mitizamo yenu itakuwa vinginevyo
 
Haya mambo yako pande zote zote. Sisi mama yetu alikuwa anatuambia tulale kwenye makochi wageni wakija nyumbani ambao most of them ni ndugu upande wa baba. Kuna waliokuwa wanakuja bila hata malengo; si wa kuondoka leo au kesho lakini tulikuwa tunabanana tu. Wengine wakaja ku win maisha tukawa tunawasikia bombani wala shukurani hawana.

Wengine ni ndugu wa mbali. Wanatangaziana tu huko kijijini; ukienda dar fikia kwa mzee fulani ana nyumba kubwa. Tena wanakuja kwa kushtukiza maana those days hakukuwa na simu za viganjani ni za kukoroga tu. Mnashtukia mtu katia timu. Sisi tulikuwa tuna mind kweli maana tulikuwa hatuko comfortable lakini mama alikuwa mkali kweli yani priority kwake ni wageni. Mama alipoachana na baba walikuwa wa kwanza kushangilia wala hawakuwa wanakumbuka fadhila zake. Binadamu ni wagumu sana kuishi nao.

hongera sana, ni wachache sana wenye moyo kama wako. Wazazi wangu walikuwa na roho nzuri sana, wageni walikuwa hawakauki nyumbani, walisoma na kupatia kazi nyumbani. Ila toka wazazi wafariki hatukuwa na thaman yeyote kwao.

ndivyo wengi wao/wote walivyo... si walichokitaka walshakipata wawakumbuke wa nini hasa mkiwa choka mbaya
 
duh poleni wote mlioteseka kwa kukaa kwa ndugu....mie namshukuru Mungu mpaka nakuwa kwa ndugu tunaenda likizo tu za juu kwa juu......ingawa sie tuliishi na ndugu wazazi walijitahidi kuwafanya kama watoto wao ingawa mwisho wa siku waliambulia matusi......baadhi ya ndugu ni lawama na hawana shukrani......
 
asilimia kubwa ya wanaolalama hapa ni dizaini hiyo...lawama,hawana shukrani
 
Imekuwa ikisemwa hivyo mara kwa mara. Mimi niliamini huu usemi mwaka 2002., nakumbuka nilikuja Dar kufatilia uhamisho wangu wa shule, nilikaa kwa baba yangu mdogo kwa takribani wiki moja. Huyo mama niliyemkuta hapo alikuwa hapiki mpaka mumewe awepo. Wiki niliiona kama mwaka, hata nilipoaga nilipewa nauli kimanati. Najua wengi tumepitia kwa ndugu kutokana na sababu mbalimbali, kuna walioishi vizuri lakini wengi wanalalamika. Je tatizo hasa nini? Ukiwa ni miongoni mwa uliyetendewa mabaya, umejifunza nini?

nilikwenda kuwatembelea kwa mjomba enzi Niko chuo
nikiwa peke yangu sebulen naangalia TV enzi za TVT nkaamua kuweka Chanel 5
mjomba aliporudi alinifokea sana eti siruhusiwi kubadiri channel ntamuharibia TV wakati sijui hata bei yake!
pia niliwahi kuishi kwa mamdogo namsaidia kazi za biasha zake lakn kila siku Mimi na house girl tunaamshwa usiku SAA 10 kufanya usafi na kusomba maji huku watoto wake wamelala!
nilikuwa napewa kufua nguo za familia nzima mpaka za ndani za mamdogo(hapo nshamaliza o level)
nikuchelewa kutoka kwenye biashara nkachelewa nakuta wamemaliza chakula!
nililazimishwa kufanya kazi hata naumwa!
ni mengi nkikumbuka naumia ila namshukuru Mungu Leo nina maisha yangu!
 
asilimia kubwa ya wanaolalama hapa ni dizaini hiyo...lawama,hawana shukrani

kuna watu kweli waliteseka .....hata baba yangu alishawahi kukaa kwa watu tena kwa mjomba wake....mateso aliyoyapata kwa yule mama....acha tu....alikuwa anafua hadi nguo za ndani za yule mama........kwa mateso yale baba yangu hakutaka kamwe tukaishi kwa ndugu....na yeye binafsi hataki kumfanyia ndugu hivyo.....

ingawa sasa ndugu tulioishi nao baadhi kiukweli wazee waliambulia lawama na matusi......
 
Back
Top Bottom