Kuwa na mtoto wa kiume ndio uanaume

Kuwa na mtoto wa kiume ndio uanaume

Mambo ya zamani hayo siku hizi mtoto ni mtoto tena afadhali upate mtoto wa kike, watoto wa kizazi hiki wa kiume watakuvalia hereni, cheni, mlegezo na wanatembea wakikatika viuno, ni headache aisee vitoto vya kiume vya sasa.
Sikatai mtoto ni mtoto lakini wa kiume akiwepo nyumbani baba huwa anajiamini zaidi, achana na hao wavaa hereni, mashoga nk
 
Sio sawa ... Acheni utumwa wa fikira....watoto wa kike nao ni mpango mzima. Ref: Obama, Bush, Clinton na pia kwa mtazamo wa haraka tu mabinti ndo huwa wanalea wazazi.
 
Na jumba bovu wanaangushiwa wanawake kwamba unanizalia ke kwahiyo Baba anatafuta mwanamke mwingine watu wanamna hii nikufyekelea mbali
 
Ngoja niwasaidie kitu wanajamvi
Ukio a umezaa watoto wengi wakike kuliko wakiume ndio kifo cha ukoo wenu kinakuja. Kinakujaje? Mwanamke anapoolewa anakwenda kwa mwanaume na kupata ubin wa mumewe yeye na watoto atakao wazaa, kuwa makini sana katika uzao wako ni mara 1000 uzae madume yote na kwa hali iliyopo sasa kupata mtoto wakiume imekuwa kama ubashiri wa sportpesa ila wanawake ni kugusa tu
 
Ngoja niwasaidie kitu wanajamvi
Ukio a umezaa watoto wengi wakike kuliko wakiume ndio kifo cha ukoo wenu kinakuja. Kinakujaje? Mwanamke anapoolewa anakwenda kwa mwanaume na kupata ubin wa mumewe yeye na watoto atakao wazaa, kuwa makini sana katika uzao wako ni mara 1000 uzae madume yote na kwa hali iliyopo sasa kupata mtoto wakiume imekuwa kama ubashiri wa sportpesa ila wanawake ni kugusa tu
Watu watapingana na ukweli tu lkn ukweli utabaki palepale hata tafiti zinaonesha ndoa nyingi hufa kifo cha mende kama jinsia ya kiume haipatikani
 
Babu yangu mzaa mama alimfukuza bibi eti kwasababu tu alizaa watoto wawili wakiume kati ya nane,alipooa mwanamke wapili akazaa watoto kumi wote wakike watoto wote ni sawa anaepanga ni mungu tu nasivinginevo
 
Ni rahisi kwa mtoto wa kiume wa rais kufikiriwa kuwa rais wa baadae kuliko mtoto wa kike wa rais angalieni hata hapa nyumbani, jiulize kwa akina Uhuru hakuna wa kike? Kwa akina karume, jk nk
 
Kuna siku niko namzalisha mama labour room basi ile namwonesha mama kuwa mtoto ni jinsia gani anasema me nasema angalia vzur ni jinsia gani kaona vzuri kasema ni ke alafu karusha shingo pembeni kama vile yuko so disappointed.
Nikamwambia sio vzur mama mtoto kumfanyia hvo day 1. Yaani alikuwa na hamu sana na dume .
Wakwe zake nao walivokuja basi kuulizia nikawaambia mtu flan kajifungua tayar na mtoto ni ke. Wakaanza wa kiume au wa kike nawaambia ni ke. Nao wakawa very disappointed.
Kimsingi ukiwa na mixer n nzuri zaid though siwezi mchukia mtoto yoyote mungu ananiletea.
Ila ofcourse kia africa jinsia me ni must ndan ya nyumba.
 
Back
Top Bottom