Kuwa na akili nyingi kama Mzee Bishanga sio kuwa tajiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa na akili nyingi kama Mzee Bishanga sio kuwa tajiri!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 28, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hata mimi nilikuwa nikiamini katika jambo hili, kwamba watu wenye uwezo mkubwa kiakili huwa na mafanikio katika maisha. Nilikuwa nikiamini hivyo kwa sababu nilikuwa nikijua kwamba ni wale wenye uwezo mkubwa darasani ndio pekee wenye uwezo wa kufanikiwa katika maisha, lakini hivi karibuni baada ya kusoma tafiti kadhaa na kuangalia maisha ya wale niliosoma nao ambao darasani walikuwa wakituburuza kwa kupata maksi za juu na kufaulu sasa hivi maisha yao ni ya kawaida kabisa na wengine wameshindwa kabisa katika maisha wamebaki kubaingaiza tu mitaani.

  Wale ambao tulikuwa tukiwaita mbumbumbu, ambao hawakuwa na uwezo kabisa darasani na wengine walishindwa kabisa kuendelea na masomo wakiwa hata hawajafika darasa la tano, ndio ambao wamefanikiwa na kumudu kuwa na kipato cha kuridhisha na wengine wakiwa wanamiliki biashara kubwa kubwa. Na ndio maana kuna wakati unashangaa sana kusikia watu wakisema, ‘fulani alikuwa bomu kabisa darasani, hata la nne hakumudu kumaliza, lakini sasa ana fedha kama nini!' Kwa nini kauli kama hizi zimebeba mshangao mkubwa? Ni kwa sababu, tumefanywa kuamini kwamba, uwezo wa kiakili, ndiyo unaoamua mtu apate fedha kiasi gani maishani mwake.
  [​IMG]
  Ninavyojua mimi ni kwamba, kuna watu kwa mamilioni ambao wana akili sana, kuanzia za darasani na zile za nje ya darasa. Lakini, ukiangalia kipato chao, kila siku ni kile cha kubangaiza. Ukweli ni kwamba, hakuna uhusiano kati ya akili nyingi na upataji wa fedha. Watu wenye uwezo wa kawaida kiakili wanaweza kuwa na mali sawa na wenye uwezo mkubwa. Haijalishi uwezo wako wa kiakili linapokuja suala la mafanikio ya kiuchumi. Kama una mtazamo chanya na unahitaji mafanikio kiuchumi, haihitaji uwezo mkubwa kiakili kuvipata hivyo.

  Hata hivyo imebainika kwamba watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili pia wana matatizo kiuchumi kiasi cha kushindwa kabisa kulipia bili na za vitu kama umeme, maji, simu na vingine hata vidogo zaidi. Matatizo kiuchumi yanaweza kuhusishwa na uwezo mdogo wa kutunza pesa. Tafiti za nyuma zilionesha kwamba, uwezo wa kiakili huathiri pato au pesa ambayo mtu hutengeneza kwa mwaka. Watu wenye uwezo mkubwa kiakili huwa na mafanikio ya juu kielimu, kicheo na hii hutokea mara nyingi. Hata Ruth Spinks, mwanasayansi wa neva (neuroscientist) anathibitisha jambo hilo na kusema, halina majadala. Na anasema, kwenye pato la kifedha, akili kubwa haina nafasi kubwa.
  [​IMG]
  Lakini pia mtu kuwa na kazi inayomlipa vizuri haimaanishi kuwa ni tajiri. Mtu anaweza kuwa na mshahara mzuri sana kwa sababu ya elimu na cheo chake, lakini je, umeshawahi kujiuliza kuhusu namna watu hawa wanavyodaiwa? Wanadaiwa sana, kwa sababu hata kutunza fedha, kwao ni shughuli pevu.
  Kwa mfano,, ingawa wanasayansi waliogundua roketi walikuwa wakipata mapato makubwa haikumaanisha kwamba wao ni matajiri kwani hawakuwa na akiba ya kutosha kulidhihirisha hilo.

  Utafiti mpya wa Zagorsky unaonesha kwamba watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili huwa hawana tabia ya kutunza pesa nyingi. Wengi wanaonekana kujali zaidi sifa za kiakili kuliko zile za kifedha. Ndiyo maana, ni vigumu kukuta wanataaluma wakiwa ndiyo matajiri katika jamii.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Bishanga nakuomba sana usichangie huu uzi.
  Lakini unaweza kuchungulia na kusalimia ukipenda.......................LOL
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Najua kuna watu watakuja humu na kutoa povu mdomoni wakinibishia......
  Natabiri mwanangu mwenyewe tena wa kumzaa King'asti atakuwa wa kwanza....................LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. EARPHONE

  EARPHONE JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 357
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwenda bure si sawa na mkaa bure...leo nimeokota kitu hapa
   
 5. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mimi pia hili jambo nimeliona wale waliokuwa wanaongoza darasani wengi wao wanaishia kuwa just employees for the rest of their life ikizidi sana kipato cha kujitosheleza. Nafikiri ni kuwa wengi wasiokuwa na elimu ya zaidi huwa ni risk takers, they don't real take into account what if......haya mambo ya wasomi ya kufanya toooooo many planning ndio yanaishia kuwarudisha nyuma.
   
 6. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ray 'the greatest' anawaza nini jamani?
   
 7. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  Mhh mtambuzi unatukatisha tamaa ss tunaotegemea makaratasi tuu
   
 8. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 997
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  I beg to differ with this analysis. Mbona watu wanaotumia sana pesa ndo wanazipata zaidi???sisi wabahili wala hatupati zaidi???
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Bishanga ni babu jinga. Ana mipesa lakini akili hana! Kila siku analiwa mihela yake na vibinti vi tinieja.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,740
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Naam mkuu Mtambuzi umenena vyema maana yote uliyoandika ni ukweli mtupu usiopingika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,326
  Likes Received: 13,032
  Trophy Points: 280
  Naamini na wengi wanaamini kuwa wafanyabiashara wengi elimu yao si kivile na hao hao wamewapita wengi wenye masters au wenye akili sana mfano fanya research kwa wafanyabiashara wengi wa Kariakoo,Dar yote,Mwanza,Mbeya utagundua wengi elimu si kubwa sana ila income,assets huwagusi
   
 12. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mkuu haya uliyonena.
   
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  wenye akili wengi sio marisk takers,kila kitu wanakifanyia analysis weeeeeeeeeeeh! mwishowe wanaamua kukiacha !
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  Mwisho utasema 'sisi ma risk taker' hatuna akili.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya bwana. Pesa watazipataje wakati wanatumia muda wao na akili yao kwenye makaratasi + JF?
   
 16. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Wacha nimwage povu langu. Hiyo analysis ya Mtambuzi ina kasoro. Kushinda mitihani siyo sifa pekee ya kusema mtu ana akili nyingi. Akili nyingi ziko katika nyanja mbali mbali. Michael Jackson alikuwa na akili nyingi katika muziki wa pop. Albert Einstein alikuwa na akili nyingi katika hesabu na fizikia. Julius Nyerere alikuwa na akili nyingi katika siasa. Usain Bolt ana akili nyingi katika riadha hasa mbio fupi. Wapo na wengine wengi. Je watu hao niliowataja unaweza kuwaita watu ambao hawakufanikiwa? Mafanikio siyo kuwa na pesa nyingi. Kuna watu ambao kwa nature zao pesa kwao siyo "motivator". Motivators kwao zinaweza kuwa ni vitu kama kushinda Nobel Prize, Kushinda Grammy, kupewa sifa kama 'Sir' kwa Waingereza, n.k.. Lakini kwa misingi ya nadharia ya mtaalam Maslow inayoitwa "Hierarchy of Needs" siyo ajabu kwa watu wa dunia ya tatu (maskini wa kutupwa) kupima mafanikio kwa kigezo cha pesa tu. Bado mahitaji yetu ni yale ya chini (ya msingi).
   
 17. mito

  mito JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,659
  Likes Received: 2,042
  Trophy Points: 280
  Exactly MadameX, this is what i wanted to say
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Naandaa uzi kukujibu very soon...............
   
 19. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,355
  Likes Received: 2,361
  Trophy Points: 280
  Mmm sijui nimkataze mwanangu asisome?
   
Loading...