Kuwa muafrika halisi kwa kutunza nywele zako na ngozi yako kwa mafuta asilia.

Nzallacado oil

New Member
Aug 18, 2017
2
1
Habari zenu ndugu zangu. Kwa jina naitwa mr aziz . Mimi ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya NZALLACADO OIL COMPANY LIMITED. Kampuni yetu inajihusisha na uzalishaji wa mafuta asilia ya parachichi (pure avocado oil) pamoja na mafuta asilia ya nyonyo au mbalika (pure castor oil). Lengo la kuwashirikisha kwa kuleta suala hili kwenu ni kuwahamasisha ndugu zangu kuachana na matumizi ya mafuta ya viwandani yanayotengenezwa kwa kemikali ambayo huaribu muonekano wetu wa asili na mara nyingine kutusababishia matatizo makubwa kama kansa. Utakutana na kijana mdogo anamuonekano wa kizee au mwingine anarangi mbili mbili katika ngozi yake, au mwingine utakuta kutwa kucha anahangaika kurefusha na kujaza nywele zake lakini mwisho wa siku matokeo anayopata ni kuendelea kukatika na kupungua kwa nywele zake. Haya yote yanatokana na athari za matumizi ya mafuta ya viwandani yenye kemikali zinazo tuathiri. Hivyo kwa kuwajali NZALLACADO OIL CO LTD ndio mkombozi wa matatizo haya kwani tumeamua kuhakikisha watoto ,vijana na wazee wa kiafrika wanabaki katika muonekano wao wa asili kwa kuwaletea mafuta asilia ya parachichi(pure avocado oil) pamoja na mafuta asilia ya nyonyo (pure castor oil) kwa ajili ya matunzo na uboreshaji wa ngozi zetu na nywele zetu za asili. Zifuatazo ni sifa na faida za matumizi ya mafuta haya.

MAFUTA YA PARACHICHI (AVOCADO OIL)

Mafuta haya ni mafuta ambayo hutumika kuzipa afya na nguvu nywele zilizokosa rutuba, yaani kujaza nywele kichwani, kuboresha nywele na kuzifanya kuwa na mng’aro mzuri, pia kuondoa tatizo la nywele zenye kipilipili (nywele zilizojiviringisha na kudumaa) pia huondoa vipara.


Mafuta ya parachichi pia hutumika kupakaa kwemye ngozi,mafuta ya parachichi yanapenya kwa haraka kwenye ngozi yanapopenya ndani ya ngozi huenda kuongeza nguvu na kasi ya uzalishaji wa protini iitwayo Colagen. Kazi ya Colagen mwilini ni kuifufua na kuirekebisha ngozi yenye matatizo na kuirudisha ngozi yako katika ubora na uhalisia wake.


Kwahiyo unapopakaa mafuta ya parachichi kwenye ngozi husaidia kuondoa madoa meusi (black spots) kwenye uso na ngozi kwa ujumla. Madoa haya ni yale yaliyosababishwa na kukamua chunusi au utumiaji mafuta makali (mkorogo) mafuta ya parachichi huondoa haya madoa yote na mabaka na kurudisha ngozi yako kama awali


Unapopakaa mafuta ya parachichi kwenye ngozi hulainisha ngozi kwa haraka sana, huongeza unyevu kwenye ngozi (moisturize), pia mafuta haya huhuisha chembechembe hai za ngozi zilizokufa na kufanya ngozi yako kuwa mpya kwani mafuta ya parachichi ndiyo mafuta yenye vitamin E nyingi kuliko mafuta yoyote. .


Mafuta ya parachichi huondoa makunyanzi usoni hata sehemu nyingine kwenye ngozi.mafuta haya husaidia kuponya vidonda na pia hutumika kama aftershave baada ya kunyoa, kuzuia vipele vinavyotokea baada ya kunyoa.


MAFUTA YA NYONYO (CASTOR OIL)

Haya ni mafuta ambayo kwanza hutumika kwaajili ya kurefusha na kukuza nywele kwa haraka sana kuliko mafuta yoyote, mafuta haya huondoa tatizo la mba kwenye nywele (kichwani).

Mafuta ya Nyonyo huondoa mba za kwenye ngozi (utangotango), huponya mapunye na magonjwa ya ngozi kwa ujumla.

Mafuta ya nyonyo huondoa michirizi (stretch marks) ambayo hutokea kwenye ngozi kutokana na unene au matatizo mengine, mafuta ya Nyonyo huondoa chunusi usoni na sehemu nyingine kwenye ngozi.


Pia mafuta ya Nyonyo ni tiba kwa kuponya na kupoza maumivu ya viungo mbalimbali kama vile:-

Maumivu ya miguu, mgongo, nyonga, mgongo na viungo vingine vya mwili kwa kuchua viungo hivyo na mafuta ya Nyonyo (Castor Oil) maumivu hupoa na tatizo huisha kabisa. Pia watu waliopooza huchuliwa na mafuta ya nyonyo ili kuwezesha damu kutiririka vizuri kwenye maeneo yaliyopooza na kumpa mgonjwa nafuu kwa haraka.

Tiba hii hufanyika kwa kuyapasha mafuta kidogo na kumchua mgonjwa kwenye kiungo kilichopooza au chenye maumivu.

Na mafuta haya yasipashwe kwenye moto, maji yachemshwe na bakuri ya bati iwekwe juu ya maji ya moto kisha mafuta yamiminwe ndani ya bakuri ya bati yakishapata joto kidogo ndiyo yatumike kumchua mgonjwa.

Kwa mahitaji na mawasiliano tupigie au tutumie ujumbe wa whatsapp kupitia namba 0716929475 / 0745295030.
0cf3c9d366055611d54ce5f602335974.jpg
 
Back
Top Bottom