Kuwa makini na bodaboda hawa!!1

Kuwa makini na bodaboda hawa!!1

Kozo Okamoto

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2013
Posts
3,391
Reaction score
1,546
Kwa uchunguzi mfupi nilioufanya kuhusu boda boda ambao ni hatarishi zaidi katika usalama wa barabarani na abiria wao pia ni wa aina hii:

1.kanyoa kiduku na mavazi yake ni ya kihunihuni bila kusahau ki tshirt au vest,kikaptura,sendo na kachomeka kitambaa aina ya bandana kwenye mfuko wake wa nyuma

2.Muda wote ni full singeli au anapiga muziki kwa sauti kubwa sana.Na mara nyingi utakuta kajilaza kwenye piki piki yake au muda mwingine anafanya manjonjo ya kucheza na piki piki muda wote.

3.Muda wote umuonapo huwezi kutambua mara ya mwisho alioga lini,yaani umuone mchana kapauka,umuone usiku wa manane kapauka,hujui kalala saa ngapi au kaamka saa ngapi au kauga saa ngapi.

Mara nyingi kundi tajwa hapo juu huwa wanatafuta hela ya kufanyia matanuzi tu na hawako kimajukumu zaidi tofauti na wale wanaoonekana watu wazima wenye majukumu ya kifamilia.

NB: Ushauri wangu ni kuwa kabla ya kukodi bodaboda ni vizuri utumiae dk mbili tatu ukiwachunguza hapo kituoni kwao then angalia mwenye unafuu.
 
Safi kabisa hizi ndio mada za kujadili.
Maana hapo umesaidia kuokoa maisha ya watu.
Kweli hawa bodaboda wenye hizo tabia ndio chanzo kikubwa cha ajali.

Ni kweli kabisa mkuu Bro Santana,hatuwezi kuepuka yote lakini kuna baadhi yanaweza kuepukika kama utazingatia na kuepuka wenye tabia hizi
 
Boda boda at your own risk
18c2f452ca124cc357ed80046c3dd1d7.jpg
 
Bila kusahau wale wanaoendesha bila kuwa na kofia ngumu...
Hao ndio hatari zaidi, jali usalama wako!
 
Back
Top Bottom