Kuwa makini na bodaboda hawa!!1

Kuwa makini na bodaboda hawa!!1

Kwa uchunguzi mfupi nilioufanya kuhusu boda boda ambao ni hatarishi zaidi katika usalama wa barabarani na abiria wao pia ni wa aina hii:

1.kanyoa kiduku na mavazi yake ni ya kihunihuni bila kusahau ki tshirt au vest,kikaptura,sendo na kachomeka kitambaa aina ya bandana kwenye mfuko wake wa nyuma

2.Muda wote ni full singeli au anapiga muziki kwa sauti kubwa sana.Na mara nyingi utakuta kajilaza kwenye piki piki yake au muda mwingine anafanya manjonjo ya kucheza na piki piki muda wote.

3.Muda wote umuonapo huwezi kutambua mara ya mwisho alioga lini,yaani umuone mchana kapauka,umuone usiku wa manane kapauka,hujui kalala saa ngapi au kaamka saa ngapi au kauga saa ngapi.

Mara nyingi kundi tajwa hapo juu huwa wanatafuta hela ya kufanyia matanuzi tu na hawako kimajukumu zaidi tofauti na wale wanaoonekana watu wazima wenye majukumu ya kifamilia.

NB: Ushauri wangu ni kuwa kabla ya kukodi bodaboda ni vizuri utumiae dk mbili tatu ukiwachunguza hapo kituoni kwao then angalia mwenye unafuu.
...Yani kama vile ulikuwa kichwani kwangu...
Huwa sithubutu kabisa kukodi boda boda yenye mtu wa dizain kama hizo
 
Kwa uchunguzi mfupi nilioufanya kuhusu boda boda ambao ni hatarishi zaidi katika usalama wa barabarani na abiria wao pia ni wa aina hii:

1.kanyoa kiduku na mavazi yake ni ya kihunihuni bila kusahau ki tshirt au vest,kikaptura,sendo na kachomeka kitambaa aina ya bandana kwenye mfuko wake wa nyuma

2.Muda wote ni full singeli au anapiga muziki kwa sauti kubwa sana.Na mara nyingi utakuta kajilaza kwenye piki piki yake au muda mwingine anafanya manjonjo ya kucheza na piki piki muda wote.

3.Muda wote umuonapo huwezi kutambua mara ya mwisho alioga lini,yaani umuone mchana kapauka,umuone usiku wa manane kapauka,hujui kalala saa ngapi au kaamka saa ngapi au kauga saa ngapi.

Mara nyingi kundi tajwa hapo juu huwa wanatafuta hela ya kufanyia matanuzi tu na hawako kimajukumu zaidi tofauti na wale wanaoonekana watu wazima wenye majukumu ya kifamilia.

NB: Ushauri wangu ni kuwa kabla ya kukodi bodaboda ni vizuri utumiae dk mbili tatu ukiwachunguza hapo kituoni kwao then angalia mwenye unafuu.
Asante kwa angalizo.Naunga mkono mawazo yako!
 
Dude, ur right on the money! Mimi huwa nafanya hiyo summary vetting subconciously, najikuta tunimemchagua mwenye nafuu
 
Angalia umri wa muhusika, akiwa mtu mzima kidogo, atakuwa na familia hata uendeshaji wake ni wa kinidhamu, lakini hawa vijana wadogo wenye vipanki ..ni balaa.
 
Kumbe inawezekana kuijua tabia ya mtu kwa muonekano wake tu?!
Hao ndio wale WADADA ama WAKAKA walio jaaliwa kupata Vigari vya mkopo, baada ya muda mfupi tu kuanza KAZI...!!

Na hoa watajwa hapo katika Thread, (Bodaboda wa hovyo) ndio wale waliokuwa wanawabeba kuwapeleka sehemu mbalimbali katika mishe zao..!!

Sifa kubwa ya AJIRA, Kwanza ni kumfanya muajiriwa kujitofautisha na JAMII inayo mfahamu VIZURI...Lengo likiwa kujiweka MATAWI ya juu...

Msidharau kazi/shughuli za watu baada ya kupata hivyo Vi-IST, SPACIO kwa njia ya MKOPO...
 
Ingekuwa amri yangu ningepiga marufuku hii biashara kama Zanzibar,kule ujinga wa ajali ajali katikati ya mji ni nadra, hii biashara iangaliwe upya irekebishwe ama laah ifutwe kabisa zibaki taxi na bajaj,tatizo hawaambiliki wanaojitambua wachache mno
 
Ifutwe watakula wapi au ndo wazidi kututobolea madirisha
 
Back
Top Bottom