Kuvunja poverty circle sio kitu rahisi

Kuvunja poverty circle sio kitu rahisi

Mimi sikubaliani na TIBIM kuwa eti mtu ukipanda miti ekari100 baada ya miaka15 mkivuna miti mnakuwa matajiri kuliko kupoteza miaka yako 15 ukisoma.Ataniwia radhi ni maoni tu.Elimu ni ufunguo wa maisha.Hakuna kitu kibaya ukiwa masikini halafu tena na elimu uwe huna.Hiyo habari ya kupanda miti ni mawazo tu unaweza kuta hata hiyo ekari100 huna na au ukapanda miti yote ikafa.Namnukuu mhe Flani raisi wetu awamu ya flani alipataga kusema ''Wazazi wa Maradhi ni Ujinga na Umasiki,Ujinga ni baba yao na Umasikini ni mama yao''(Mwisho wa kunukuu).

Ukiwa huna elimu kabisa kila kitu unafikiria umelogwa na unaendesha mambo yako kama meli isiyo na usukani matokeo yake maradhi na umasikini juu.Hivi unafikiri matajiri tulio nao Mfano Mzee wa IPP na kijana MOD hawana elimu?.Mzee wa IPP ana shahada ya udakitari na ni moja ya watu wachache wenye cheti cha charter cha wingereza hapa nchini.Kijana MODi ana shahada ya pili ya uchumi amesomea Marekani,Mzee wa watu wa Juice,Unga n.k anaweza kuwa hana elimu kubwa lakini amesomesha wanawe kwa elimu za juu sana kwa kuona umri wake mkubwa na wanawe wanamsaidia kupanua biashara na nyie mnaona.

Ni kweli wako matajiri walio na utajiri bila elimu ila ukiona wanavyoendesha mambo yao utasikitika sana.Unakuta mtu anaungulia ndani na pese kwenye magunia.Eleweni kuwa hata matajiri wakubwa wasio na elimu kuendesha mambo yao wanatafuta wasomi.Na walio wajanja wanaanza kusoma baada ya kugundua walichokosa maishani na wengine siwataji wameshafikia hata ngazi ya udaktari wa falsafa.Unakuta mtu ana ng'ombe 5000 lakini analala kwenye ngozi ya ngombe na hali nyama anachinja siku ngombe akifa au kukiwa na msiba.

Eleweni haiwezekani watu wote tukawa matajiri nani atamtuma mwenzake na nani atamuajiri mwenzake?.Matajiri mnao waona Marekani msije dhani hawana Elimu kama kina Trump na huyu tajiri wa Africa Aliko Dangote.Niwieni radhi kidogo nitataja mikoa yenye maendeleo mkoa flani wa kaskazini,mkoa flani wa kusini magharibe na na mkoa flani wa magharibi maendeleo yao japo hawana rasilimali yeyote ya kuwekeza au ardhi kubwa sana lakini wameendelea kutokana na Elimu sio maisha ya kubahatisha bahatisha.

Ili kuvunja CIRCLE ya umasikini kitu cha kwanza kabisa ni kutoa UJINGA kwa elimu mambo ya bahati yatafuatia hiyo ni mipango ya mungu sio kusema mbona fulani hajasoma lakini ana mali ni kujidanganya bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi.

Kinachosababisha CIRCLE ya umasikini isikatike ni UJINGA(kukosa elimu) baba akiwa hajasoma kabisa akizaa mtoto naye anajiwa na ujinga wakusema mbona baba hajasoma mimi nisome nini sasa.Mtoto ana pass ujinga huo kwa wanawe na wanawe kisa mtasingizia laana au shetani SHETANI wetu ni ujinga wa kukosa elimu.Kwa ujinga mtu alio nao mtu anaoa wake wanne huku akijua ni masikini unategemea nini watoto wanazaliwa kwenye lindi la umasikini.Bahati mbaya baba akiondoka bado anaacha watoto kwenye lindi la umasikini kizazi na kizazi wanapasiana ujinga.

ELIMU inamkomboa mtu kutokuwa masikini wa kutupwa(ABJECT POVERTY) pia inamfanya mtu awe na uwezo wa kati sio chini sana wala juu sana.Sasa usiende shule kabisa utegee utakua kama flani utasubiri mpaka jua linazama.

Kitu kingine niwaase watanzania wenzangu.Kuna dhana imejengeka kuwa mtu anasoma ili aajiriwe.Hii pia ndio inachangia kuwafanya wasomi wasipige hatua kimaendele.Mtu unasoma ili uelimike upambane na hali yako serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu wa kila sekta na hata sekta binafsi imefikia hapo.Hiyvo chonde msikate tamaa kutokusoma kisa sitaajariwa afterall kuajiriwa ni utumwa.Tumia elimu na maarifa uliyopata kujiajiri mwenyewe.

Naomba kutoa hoja
 
Last edited by a moderator:
Kwangu mimi nacho amin kipaji pekee alicho nacho mwanangu ndo kitamfanya atoboe maisha, jukumu langu ni kumuendeleza tu. na kumfanya aishi kwenye ndoto zake.
Hakikisha unainvest sana ktk hilo maana vipaji kwa Tanzania bado sana, miundombinu si rafiki, bila kusahau elimu pia maana kipaji bila elimu in changamoto!
 
Hii iko applicable sana katika dunia ya tatu ambapo fursa kwa mtoto wa masikini zimebanwa mno lkn kwa dunia ya kwanza opportunities za kujikwamua hata kwa mtoto wa masikini ni nyingi tu.
Noted
 
Ni kweli wengi utegemea elimu,then wapate kazi ya kuajiriwa, kitu ambacho ni kosa kwa hali ya sasa.MAARIFA ni kitu muhimu sana cha kuvunja chain ya umasikini, mkipata mentor wa kuwaongoza vizuri, mnaweza mkaleta mabadiliko makubwa katika jamii yako.Mimi naamini katika ardhi ukiwekeza vya kutosha na kwa bidii,mfano wengi vijijini bado mapori ni mengi tumshuru Nyerere mzalendo halisi wa vitendo sio wengine wa maneno,kutokuruhusu ardhi kuwa mali binafsi wengi tungekuwa manamba vizazi na vizazi, yaani wapangaji kama Kenya. Sasa huko vijijini familia nzima ikijikita kwenye upandaji wa miti mfano heka 100,baada ya miaka 15 ambayo mtu atapoteza kusoma aje apate ajira familia hio inaweza kupata mapato makubwa sana ambayo yataweza kuibadilisha,jamii husika.Pia ukiweza wapeleke kozi ndogo ndogo wajifunze ujuzi mfano useremala,ufundi, udereva, ushonaji,nk,ujuzi ambao sio lazima ukae darasani mda mwingi,mfano kumuombea kwa wenye ujuzi wajifunze pia ni tools ya kukata chain ya poverty. Sababu poverty ni suala la kwenye akili zaidi kuliko hali halisi.MAARIFA ndo njia pekee ya kuondoa umasikini kupitia smartphone utapata kila aina ya MAARIFA.
Thanks for visionary thought
 
Inasikitisha sana, unakuta kila ukijitahidi kuna kitu km kinakuvuta nyuma ndio maana mara nyingi masikini tunasingiziaga uchawi kumbe tayari ni poor circle inatusumbua, unakuta kijana anaendelea vizuri kwenye masomo yake anafika mpaka university kinatokea tu kikwazo kinamrudisha nyuma
Tuendelee tu kupambana tu mkuu
 
Kwangu mimi nacho amin kipaji pekee alicho nacho mwanangu ndo kitamfanya atoboe maisha, jukumu langu ni kumuendeleza tu. na kumfanya aishi kwenye ndoto zake.
Endelea kumuandaa dogo
 
Capitalism ni nzuri kuliko ujamaa maana ya capitalism ni Kazi juu ya Kazi hakuna mjomba kama ujamaa, ni jinsi ya kutap kupata MAARIFA na kuyafanyia Kazi,capitalism usababisha mzunguko Mkubwa sana wa noti,mtaani kuliko ujamaa hivo ni bidii yako tu kwenda spidi.Tusingekumbatia ujamaa tungekuwa mbali sana,ila ardhi tuombe iendelee kuwa ni Mali ya serikali kamwe asiruhusiwe mtu kubinafisha ardhi awe mpangaji tu.
Of coarse, watu husema ukitaka kuwahi kimbia mwenyewe
 
Mimi sikubaliani na TIBIM kuwa eti mtu ukipanda miti ekari100 baada ya miaka15 mkivuna miti mnakuwa matajiri kuliko kupoteza miaka yako 15 ukisoma.Ataniwia radhi ni maoni tu.Elimu ni ufunguo wa maisha.Hakuna kitu kibaya ukiwa masikini halafu tena na elimu uwe huna.Hiyo habari ya kupanda miti ni mawazo tu unaweza kuta hata hiyo ekari100 huna na au ukapanda miti yote ikafa.Namnukuu mhe Mkapa alipataga kusema ''Wazazi wa Maradhi ni Ujinga na Umasiki,Ujinga ni baba yao na Umasikini ni mama yao''(Mwisho wa kunukuu).
Ukiwa huna elimu kabisa kila kitu unafikiria umelogwa na unaendesha mambo yako kama meli isiyo na usukani matokeo yake maradhi na umasikini juu.Hivi unafikiri matajiri tulio nao Mfano Mengi na Dewji hawana elimu?.Mengi ana shahada ya udakitari na ni moja ya watu wachache wenye cheti cha charter cha wingereza hapa nchini.Dewji ana shahada ya pili ya uchumi amesomea Marekani,Bakhresa mzee wa watu anaweza kuwa hana elimu kubwa lakini amesomesha wanawe kwa elimu za juu sana kwa kuona umri wake mkubwa na wanawe wanamsaidia kupanua biashara na nyie mnaona.
Ni kweli wako matajiri walio na utajiri bila elimu ila ukiona wanavyoendesha mambo yao utasikitika sana.Unakuta mtu anaungulia ndani na pese kwenye magunia.Eleweni kuwa hata matajiri wakubwa wasio na elimu kuendesha mambo yao wanatafuta wasomi.Na walio wajanja wanaanza kusoma baada ya kugundua walichokosa maishani na wengine siwataji wameshafikia hata ngazi ya udaktari wa falsafa.Unakuta mtu ana ng'ombe 5000 lakini analala kwenye ngozi ya ngombe na hali nyama anachinja siku ngombe akifa au kukiwa na msiba.
Eleweni haiwezekani watu wote tukawa matajiri nani atamtuma mwenzake na nani atamuajiri mwenzake?.Matajiri mnao waona Marekani msije dhani hawana Elimu kama kina Trump na huyu tajiri wa Africa Aliko Dangote.Niwieni radhi kidogo nitataja mikoa yenye maendeleo Kilimanjaro,Mbeya na Kagera maendeleo yao japo hawana rasilimali yeyote ya kuwekeza au ardhi kubwa sana lakini wameendelea kutokana na Elimu sio maisha ya kubahatisha bahatisha..
Ili kuvunja CIRCLE ya umasikini kitu cha kwanza kabisa ni kutoa UJINGA kwa elimu mambo ya bahati yatafuatia hiyo ni mipango ya mungu sio kusema mbona fulani hajasoma lakini ana mali ni kujidanganya bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi.
Kinachosababisha CIRCLE ya umasikini isikatike ni UJINGA(kukosa elimu) baba akiwa hajasoma kabisa akizaa mtoto naye anajiwa na ujinga wakusema mbona baba hajasoma mimi nisome nini sasa.Mtoto ana pass ujinga huo kwa wanawe na wanawe kisa mtasingizia laana au shetani SHETANI wetu ni ujinga wa kukosa elimu.Kwa ujinga mtu alio nao mtu anaoa wake wanne huku akijua ni masikini unategemea nini watoto wanazaliwa kwenye lindi la umasikini.Bahati mbaya baba akiondoka bado anaacha watoto kwenye lindi la umasikini kizazi na kizazi wanapasiana ujinga.
ELIMU inamkomboa mtu kutokuwa masikini wa kutupwa(ABJECT POVERTY) pia inamfanya mtu awe na uwezo wa kati sio chini sana wala juu sana.Sasa usiende shule kabisa utegee utakua kama flani utasubiri mpaka jua linazama.
Kitu kingine niwaase watanzania wenzangu.Kuna dhana imejengeka kuwa mtu anasoma ili aajiriwe.Hii pia ndio inachangia kuwafanya wasomi wasipige hatua kimaendele.Mtu unasoma ili uelimike upambane na hali yako serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu wa kila sekta na hata sekta binafsi imefikia hapo.Hiyvo chonde msikate tamaa kutokusoma kisa sitaajariwa afterall kuajiriwa ni utumwa.Tumia elimu na maarifa uliyopata kujiajiri mwenyewe.

Naomba kutoa hoja
True lkn kusoma ni Pesa,elimu sio bure ni ghali,nachomaanisha kwamba upate MAARIFA ya kuzalisha kwamba,then ukipata kipato ndo uwekeze kizazi kwenye elimu,ukipata kipato watoto watasoma vizuri. Tungekuwa na mfumo wa elimu bure kama wenzetu,ingeaaidia kupunguza umasikini.
 
Kuvunja mfumo huu wa kijamaa ni maamuzi magumu, kwani itakulazimu uonekane kichaa Kwanzaa kwa ndg na jamaa.
True hio nayo ni mbinu, unaweza ukajinyima na kuonekana mbaya kwa ndugu Kuwa utoi msaada, then mbeleni ukishasimama ndo uanze kuwasidia
 
MAARIFA yapo mengi sana ya kujikwamua na umasikini, shida unaweza ukawa na MAARIFA ukakosa Pesa ya kuligeuza Wazo kuwa Pesa. Mfano Kilimo kinataka zana na vitendea kazi ambavo lazima uwe na Pesa ili uvipate.
 
Sure
 
Familia nzima ikiwa inamtegemea mtu 1, ikitokea huyo mtu akadondoka, basi familia nzima inadondoka.... Distribution of wealth ni nzuri katika familia na capitalism ni nzuri kwenye familia kuliko socialism
 
True lkn kusoma ni Pesa,elimu sio bure ni ghali,nachomaanisha kwamba upate MAARIFA ya kuzalisha kwamba,then ukipata kipato ndo uwekeze kizazi kwenye elimu,ukipata kipato watoto watasoma vizuri. Tungekuwa na mfumo wa elimu bure kama wenzetu,ingeaaidia kupunguza umasikini.
Sasa nimekupata TIBM wazo lako zuri tuendelee tu kuelimishana kiungwana
 
Hello JF comrades
Ni matumaini yangu mko poa pande zote of this planet Earth.
Kuna jambo moja limenicost na ninaelewa ni changamoto kwa wengi pia. So kupitia platform hii naomba kufungua mjadala ili tushare uzoefu.

Piga ua, inama inuka kuvunja poverty circle sio kitu rahisi.

Poor daddy leads to poor sons and daughters and then poor daughters and sons leads to poor family and then poor sons and daughters. And the circle goes on.

Namkumbuka jamaa mmoja rafiki yangu tuliotokea kijiji kimoja wilaya X mkoani Geita. Alikua wa Kwanzaa katika familia ya watoto 12. Wazazi wake walikua masikini sana hivyo walijikuta wakiwa trapped in poverty circle.

Jamaa aliishia form four baada ya kusoma kwa kuunga unga sana. Baada ya kumaliza shule alijikita na biashara ya mitumba, akichukua mzigo wa tajiri na kuuzungusha kwenye minada na kile cha juu ndo inakua faida yake.

Katika umri wa miaka 35 alijikuta anageuka kuwa Baba wa familia mbili kufuatia kifo cha baba yake, huku akiachiwa familia ya baba yake, amtunze mama na wadogo zake. Wakati huo tayari yeye pia alikua amekwisha kuoa na ana watoto wawili.

Kwa mazingira ya maisha hayo uku akiwa na kipato duni, familia zote mbili zilijikuta kwenye dimbwi kubwa la umasikini. Wadogo zake wengi tu walilazimika kukatiza masomo na kuanza kuwa wabangaizaji, wale wa kike waliishia kupewa mimba na kuzalia nyumbani.

Familia iliongezeka na hakukuwa na mtu wa kuleta tumaini tena katika familia yao. Mama yao mzazi kutokana na kufanya kazi nzito na misoto ya maisha, kadri siku zilivyosonga afya yake ilianza kuzoofu.
Mwishoni ilikuja kujulikana alikua na ugonjwa wa kifua kikuu na alichelewa kupata matibabu na umauti ulimkuta. Hapa ilikua ni Kama miaka nane baada ya mmewe kufariki.

Baada ya mama yao kufariki, uhalisia wa maisha ujidhihirisha kuwa ubaki home ufe kwa njaa au ujitose duniani kupambana na hali yako, chaguo la pili ndilo lilkua chaguo la wengi na familia ilisambaratika kila mmoja na maisha yake.

My take :
Nimerejea uzoefu huo amabo ni mkasa halisi nilioushuudia katika maisha haya ila lengo langu nilitaka kuonyesha ikiwa wazazi hawatajenga msingi wa familia inakua ngumu sana kuuvunja mzunguko wa umasikini.

Leo ni zaili hata kwa maisha yetu
Unajikuta wewe ndo msomi kwenye familia
Umepata kikazi chako kwa mishahara hii ya kaizari ambayo huishia week ya pili baada y'a kupata monthly salary.

Lakini unajikuta unalazimika kusomesha wadogo zako watatu, uwatunze wazazi wako na wajomba.

Omba Mungu uwe umeo mke ambaye upande wake kuna unafuu, lakini maisha yasivyo na huruma
Mara nyingi ndege wanaofanana huruka pamoja, this means mtu mwenye kipato kidogo uoa wake wanaotoka familia kama yake, hivyo umasikini uzaa umasikini.

Omba Mungu usiwe unaishi kwa sifa uanze kuchukua mikopo ili ukanunue gari tena ya kutembelea amabayo haiingizi kipato chochote ili uonekane unaunafuu kwa maisha ya kitaa.

Tena shukuru Mungu ukiwa umeshamaliza mkopo wa Loan bord, vinginevyo hadi unastafu maisha ni ya kuunga unga tu na full stress.

Point to note :

Bila kujimakinisha kujenga misingi ya familia yako hesabu maumivu kwa kizazi chako pia.

Leo tunasumbuka sana kuvunja our poverty circle kutokana na makosa ya wazazi wetu , we're living the poverty legacy of our poor daddy

Mafanikio makubwa sana kwetu ni ikiwa tutaweza kufanikiwa kuandaa misingi ya watoto wetu ili at least wakue katika misingi huru nje ya umasikini.

Naomba kuwasilisha, karibuni wadau tushirikishane uzoefu na kupendekeza namna bora kabisa za kuvunja poverty cycle.
Hua siamin sana kwamba elimu yaweza kuvunja poverty cycle,binafsi nimewai kujikuta kwenye hilo janga tena nikiwa na umri Mdogo (sio kama uliemtolea mfano maana yangu hayakua makubwa ivyo)
mm nilikataa shule tena kwa herufi kubwa baada tu ya elimu ya msingi na kuamua kuzamia dunian kukombua kile kilichokua kinaangamua..ya Mungu ni mengi kwa msaada wake nimefanikiwa kuvunja hyo poverty cycle

Sio kazi rais kabisa kuvunja mkataba na umasikin unaitaji kuagana na nafsi, kupamba na umasikini ni sawa kabisa na kupambana na shetani unatakiwa kupambana kiroho(kumuomba MUNGU) na kimwili!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom