Kuvuja siri & kauli ya Msajili vyathibitisha ukweli wa mtonyaji serikalini kuhusu vifo mikutanoni

Mtu mshamba anapojaribu kufanya jambo flani ili aonekane mjanja hujikuta anakosea na kuzidi kuonekana mshamba maradufu.
Ccm kila wanapojaribu kufanya jambo flani ili waonekane ni chama safi, wanajikuta wanakosea na kuzidi kukichafua chama chao na kuonekana ni adui mbele ya watanzania.
Viongozi wa ccm na vibaraka wao wamekua kama wajenzi wa mnara wa babeli,
Nape akiomba nyundo nchemba analeta msumeno,
shingela akiomba msumari wassira analeta koleo,
Nchimbi akiomba kobiro tendwa analeta bawaba.
CCM imelaanika kiwango ambacho kila maovu wanayofanya yanadhihirika mbele ya watanzania.
Ccm is in grave condition.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
CDM wameridhika na yote yanayotokea ndio maana hawataki kufanya maamuzi magumu kwa Imani kuwa wataitoa ccm 2015 Mimi sio mtabiri lakini nawaapia CDM hamtoweza kamwe kuitoa ccm madarakani kwa kipande cha karatasi au kura sahauni ccm imeshika mpini Na wako tayari kumuua Hata yesu Angekuweko ili mradi wabaki madarakani......viongozi wa juu CDM chukueni maamuzi magumu na muache kuimba taarabu Kama Nape

Mkuu kuna kitu sijakuelewa,
Zaidi ya kwamba wako porini kila siku wakijenga chama hebu ni mbinu gani mkuu unayowapendekezea zaidi ya sanduku la kura? kwa maoni yangu viongozi wetu wametimiza majukumu yao to the maximum.
 
Hakuna mtu yeyote aliyemtegemea Mungu wa Israeli akashindwa. Fuatilieni historia hata ukisoma vitabu vitakatifu Korani na Biblia vinashuhudia hayo.

CDM wanamtegemea Mungu wa Israel na wao wanamtegemea shetani kwa matendo yao.Nawahakikishia kamwe shetani hataachwa atambe mbele ya Mwenyezi Mungu.Yanayowakuta CDM kwa sasa ni majaribu tu ili Mungu azidi kutukuzwa.CDM watapata sana shida lakini mwishoni watashinda.

Mafedhuli watashindana lakini kamwe hawatashinda.Ninachoweza kusema ni Dr Slaa na Mbowe jipeni moyo Mungu wa Israel atawainua na mtashinda.
 
Yana mwisho haya. Kwa aliyesoma kitabu cha KULI anaikumbuka kauli hii dhahiri
 
Ukereketwa tu umekuzidi hadi unaandika habari kulingana na fikra zako. Hakuna ulazima wa mtumishi anaposafiri kikazi lazima kiongozi wake apate ridhaa kwa watumishi wengine. Hatutaki udaku hapa.
 
CCM na serikali kwa ujumla wamekosa kitengo kizuri cha Public Relation. Kabla ya kuongea jambo lazima upime watu wana mtazamo gani kuhusu hilo jambo. Na muhimu zaidi, ukijaribu kudanganya, kuwa makini kwa sababu uongo ili uaminike unapaswa kuwa karibu sana na ukweli, la sivyo utadharauliwa kwa kujaribu kudharau wengine.
 
Msajli wa vyama alichemka..alichukua desa lile lile la kabla picha hazijarushwa..Lakini aliyeumbuka zaidi ni kamanda aliyesema chuma kizito. Lakini zaidi hata Dr Nchimbi anaumbuka kwa kusema ni bomu la machozi limelipuka vibaya na kumwua mwandishi.

Yaani ukijaribu kuunganisha haya yote unaona kabisa ni dili kubwa sana walikuwa wamepanga lakini kwa bahati mbaya sana wakachemka kwenye umaliziaji..

Sijui kwa nini serikali inatumia nguvu ya kupita kiasi hasa kwenye M4C..why hata CCM inaonekana hawapati usingizi kwenye hili kiasi cha kuanza kutumia siasa za kibabe badala ya hoja..
 
Hakuna mtu yeyote aliyemtegemea Mungu wa Israeli akashindwa.Fuatilieni historia hata ukisoma vitabu vitakatifu Korani na Biblia vinashuhudia hayo.CDM wanamtegemea Mungu wa Israel na wao wanamtegemea shetani kwa matendo yao.Nawahakikishia kamwe shetani hataachwa atambe mbele ya Mwenyezi Mungu.Yanayowakuta CDM kwa sasa ni majaribu tu ili Mungu azidi kutukuzwa.CDM watapata sana shida lakini mwishoni watashinda.Mafedhuli watashindana lakini kamwe hawatashinda.Ninachoweza kusema ni Dr Slaa na Mbowe jipeni moyo Mungu wa Israel atawainua na mtashinda.

Ameeeeeen.......
 
Mi nilishasema "nachukia kazi inayofanywa bila kushirikisha ubongo". Hawa wawili Zelote Stephen na Kamhanda ni wahusika wakubwa na damu hizi zitawarudia tu.
N.B: Tanzania ijiandae kwa kizazi cha visasi maana watoto wa ndugu zetu wanaouwawa pasi na hatia lazima watakuja lipiza vifo vya wazazi wao. Take my words
mimi nimeshaanza kuwaambia wanangu wawaogope na kuwaepuka sana mapolisi na wasije kabisa kuwaamini nikaongezea kwamba wakati mwingine majambazi huwa wema kuliko polisi pindi tu ukiwapatia wanachokitaka.kwa kweli polisi wana laana na ndio maana maisha yao hayajawahi kuwa mazuri hata siku moja.
 
Kwa namna hii Tendwa asitegemee kuaminika katika maamuzi yake. Yaani yeye amekuwa refa mchezaji kitu ambacho hakiwezi kumpa uwezo wa kufanya maamuzi mazuri.. Namwonea huruma sana huyu mzee!!!
 
Msajli wa vyama alichemka..alichukua desa lile lile la kabla picha hazijarushwa..Lakini aliyeumbuka zaidi ni kamanda aliyesema chuma kizito. Lakini zaidi hata Dr Nchimbi anaumbuka kwa kusema ni bomu la machozi limelipuka vibaya na kumwua mwandishi. Yaani ukijaribu kuunganisha haya yote unaona kabisa ni dili kubwa sana walikuwa wamepanga lakini kwa bahati mbaya sana wakachemka kwenye umaliziaji..
Sijui kwa nini serikali inatumia nguvu ya kupita kiasi hasa kwenye M4C..why hata CCM inaonekana hawapati usingizi kwenye hili kiasi cha kuanza kutumia siasa za kibabe badala ya hoja..
bado tu kuanza kuyalipua masaburi yao hii nchi iko karibu kuvurugwa maana hata kwa hila wakiiua cdm bado wao kwa wao hawakubali kuukosa uraisi kila mtu kwa muda wake nchi haipo salama hii.
 
Policeccm, CCM na serikali yake wameingia studio kurekodi/kucheza movie ili watanzania tukiona tuwasifu kuwa movie yao ni kali lkn walipoitoa movie yao ukiangalia unaona chengachenga hakuna picha. Hii ya Nyololo Iringa haina tofauti na movie ya Dr. Ulimboka ambayo ilichezwa hatukuielewa matokeo yake hata mchungaji Gwajima kawageuka akawa upande wa umma. Sasa hivi kwa taarifa Dr. Ulimboka wamebana kiasi kwamba hakutani na chombo chochote cha habari ndio maana unaona kimya. mm sio mwana cdm lkini nawashauri cdm yafuatayo:-

1. kila mnapokubaliana na polisi namna ya kufanya mikutano na maandamano, mpatiwe makubaliano hayo kimaandishi;picha za aina zote ikiwezekana ziwepo kama kumbukumbu ya kikao

2. kila mnapokubaliana, mhakikishe mnaweka kifungu cha bayana kuwa kusiwepo usitishwaji wa shughuli za siasa za cdm kwasababu yoyote ispokuwa tu kama cdm kwa busara zao wataona inafaa

3. jitahidini kufuatilia matumizi ya simu za viongozi wenu wakuu ili mtambo wa kutumia simu za watu ulioingizwa nchini ukijaribu tu kuingilia au kuandika sms kutumia namba hizo kwenda kwa mtu yeyote muanike hadharani mbele ya vyombo vya habari

4. tafuteni teknolojia mbadala israel, ya kulinda simu za viongozi wakuu wa cdm zisiingiliwe na mtambo huo. Israeli hawashindwi kuwapatia vitu hivyo

5. hakikisheni mnakuwa na waandishi wenu ambao ni wanachama wa CDM katika kazi zenu wasiopungua 3, ambao watakuwa wanapiga picha, kurekodi video na kufuatilia kila kinachotokea ktk eneo husika

6. imarisheni kikosi chenu cha upelelezi na hakikisheni chochote kinachopangwa na ccm, police ccm na serikali yake, mnakipata kimaandishi(minutes) au tape/video. hili linawezekana endapo mtapanda watu wenu kwenye system zima ya utawala wa ccm. hili litasaidia cdm kujiandaa kisaikolojia na wakati mwingine kubadilisha utekelezaji wa kazi za siasa. kwa mfano mmegundua policeccm wamepewa agizo kuwapiga mabomu ikibidi kuua mtu Nyololo Iringa, nyie mnaenda kufanya mkutano sehemu tofauti nna hiyo, labda Ihowanza/itengule ambako ni mbali sana na nyololo.

7.kadri inavyowezekana epukeni kuwatumia sms policeccm, ccm na serikali yake, katika mazungumzo yoyote sisitizeni kukutana uso kwa uso na hakikisheni mnarekodi vikao vyote ikibidi hata bila wao kujua, ili kuweka ushahidi kamili.

8. Chunguzeni mienendo ya baadhi ya watu wa cdm bila wao kujua hususani wale ambao hata jamii inawatuhumu kushirikiana na ccm sirini hata wale wasiotuhumiwa. lengo likiwa ikifika 2015 wakati wa kuteua wagombea tusiweke watu wa aina ya Shibuda kwani anatukera sana kuwemo ndani ya cdm wakati roho yake iko ccm

9. Nawashauri viongozi wote mkapate mafunzo ya negotiation skills, conflict management and fraud management. kimsingi training iwe comprehensive. mkiweza mnaweza kuwapata Waisraeli ambao wanaweza kuwapa ifano hai jinsi walivyojikusanya kisha kuanzisha utawala ndani ya ardhi ya Babu zao bila hata wapalestina kujua. mafunzo haya yataboresha utendaji kazi wenu na taasisi zinazoongozwa kwa sera za ccm.

10. Anzisheni TV yenu ambayo itakuwa inarusha matangazo ya mikutano yenu moja kwa moja, hii itasaidia kufrastate system ya ccm kwani watu wataona kila kinachooendelea na kinachofanyika, kwao itakuwa vigumu kutoa uongo wa sasa au kufanya vurugu kwani watahofia kujulikana mapema. hakuna mtu anayependa matendo yake ya giza yaonekane nchi nzima.

11. Tuulizeni wananchi tutawaambia maeneo gani kumeiva hamuhitaji kufanya mkutano zaidi ya kwenda kufungua matawi, kugawa kadi, bendera na mavazi ya cdm

12. Fanyeni tafiti kujua je endapo ccm na serikali yake watatunga sheria kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, je mtaendesha vipi shughuli zenu na kuendelea kupata matokeo

13.Mwombeni Mungu awasaidie, msiwe watu wa kukata tamaa, kwani watanzania wengi tunaona cdm ndio chama mbadala wa ccm.


Tena narudia kusema saa ya ukombozi ni sasa, tusiache ccm waendelee kuuza nchi, utu wetu, uridhi wetu, maliasili yetu na kuongeza pengo kati ya maskini na walionacho

nadhani mmenisikia mkereketwa wenu

mm nawatakia mafanikio, huenda hapo mbeleni nitakuwa mwanacdm
 
Imekuwa ni kawaida kabisa Polisi kusafirishwa kutoka eneo moja kwenda lingine kuwadhibiti CDM tumeona kwenye mikutano na chaguzi mbali mbali. Hii inaashiria kuwa Polisi sampuli ya kina SABA SITA Wapo wengi ambao wameshajipatia umaarufu ndani ya jeshi la polisi na hii ndiyo shughuli zao.Kwahiyo hata hao waliotoka dom usikute ndiyo waliotekeleza maagizo Moro.
 
CDM wameridhika na yote yanayotokea ndio maana hawataki kufanya maamuzi magumu kwa Imani kuwa wataitoa ccm 2015 Mimi sio mtabiri lakini nawaapia CDM hamtoweza kamwe kuitoa ccm madarakani kwa kipande cha karatasi au kura sahauni ccm imeshika mpini Na wako tayari kumuua Hata yesu Angekuweko ili mradi wabaki madarakani......viongozi wa juu CDM chukueni maamuzi magumu na muache kuimba taarabu Kama Nape.

Mkuu kuna kitu sijakuelewa,
Zaidi ya kwamba wako porini kila siku wakijenga chama hebu ni mbinu gani mkuu unayowapendekezea zaidi ya sanduku la kura? kwa maoni yangu viongozi wetu wametimiza majukumu yao to the maximum.
mimi nimemuelewa kwamba wanatakiwa kutumia mbinu pekee ambayo mwanaume huitumia pindi majadiliano na hekima inaposhindikana.anamaanisha ngumi au nguvu.
 
Back
Top Bottom