Kuvuja siri & kauli ya Msajili vyathibitisha ukweli wa mtonyaji serikalini kuhusu vifo mikutanoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuvuja siri & kauli ya Msajili vyathibitisha ukweli wa mtonyaji serikalini kuhusu vifo mikutanoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Sep 6, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Jumatatu niliweka uzi hapa kuhusu nini hasa kinachoweza kuwa nyuma ya pazia la vifo vyenye utata ktk mikutano ya Chadema. Mtumishi wa idara muhimu ya serikali alniambia kuwa kuna mkakati wa kujaribu kudhoofisha chama chenu serikalini.
  Kwamba mkakati wa serikali ni kutunga sheria ya kuthibiti vyama vya upinzani hususani Chadema mbele ya safari.
  Kwamba hofu yao ni kama sheria hiyo itakukubalika kwa wananchi na wahisani. Na kwamba kuna maofisa wanaodhani kuwa sheria hiyo italeta vurugu.
  Na hoja yake ni kwamba inawezekana vifo hivyo vimepangwa ili kuwalainisha wahisani, na kuwaandaa wananchi kuikubali sheria husika pamoja na kuwapa hoja wakubwa serikalini wanaoipigia chapuo sheria hiyo. Pili, sheria ikikwama basi mbinu za kuwachafua zinaweza kutumika. Utunzi wa sheria hii ulishadokezwa hadharani Bungeni na Mwanasheria mkuu.
  Leo naomba nitoe hoja 2 zinazoonesha kwamba mtonyaji wangu kutoka serikalini alikuwa mkweli na yuko sahihi.

  Mosi, kuvuja kwa siri ya Askari kutolewa nje ya Mkoa wa Iringa kinyemela kama lilivyonukuliwa na gazeti la mwananchi hapa chini

  Chanzo hicho kilisema kwamba awali, hawakuwa wakifahamu kama baadhi ya wenzao walichukuliwa na kupelekwa Iringa. "Tulikuja kuona kwenye gazeti picha na tulipofuatilia tukaelezwa kuwa ni kweli Dodoma ilitoa askari kwenda Iringa."

  Askari mwingine aliyekuwa katika operesheni hiyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma, alikiri kuwa hadi jana baadhi yao walikuwa bado wako Iringa na kwamba walikwenda kwa agizo la wakubwa wake wa kazi.
  "Sisi ni Watanzania, lakini tumelazimika kuyafanya hayo kwa sababu ya mkate (malipo). Kwa kweli haikuwa haki, kuwatoa askari na silaha kutoka mikoa mitatu kana kwamba wanakwenda kupigana vita!"

  Alidokeza kwamba, askari wote waliotoka Dodoma walikuwa njiani kurudi mkoani humo, jana lakini gari la maji ya kuwasha liliendelea kubaki huko Iringa likiwa na dereva wake na askari mmoja mwenye cheo cha inspekta. Askari huyo alisema kwamba gari hilo lililazimika kubaki kutokana na hitilafu.

  "Wengine wamerudi lakini, kuna wengine wenye gari la kuwasha bado walikuwa Iringa, gari lao limepata hitilafu kidogo," kilisema chanzo hicho kutoka mjini Dodoma.

  Mmoja wa askari hao alidaiwa kwamba hiyo inaweza kuwa moja ya sababu ya askari hao kumshambulia marehemu Mwangosi wakati mwenzao anayemfahamu akijaribu kuwazuia. "Hii inaonyesha kuwa askari hao waliompiga walikuwa hawamjui na huyu aliyekuwa akiwazuia, alimjua."

  Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen hakukubali wala kukanusha na badala yake alisema: "Mambo yote hayo yanatakiwa kujibiwa na Kamanda wa Iringa."
  Aidha, alisema sakata la kifo cha mwandishi huyo kwa sasa liko katika vyombo vya uchunguzi hivyo asingekuwa tayari kulizungumzia.

  "Siwezi kusema kama askari wangu walikwenda huko au hawakwenda, isipokuwa ninachoweza kusema ni kwamba suala hilo lipo katika vyombo husika hivyo waachiwe wao au Kamanda wa Iringa ndiye mwenye majibu."
  Alipotajiwa jina la mmoja wa askari aliyeonekana katika picha za video na magazeti za tukio hilo kwamba anatokea katika moja ya vituo vyake, kamanda huyo alisema: "Mimi yakitokea Dodoma nitazungumza wala siyo mtu mwingine kwa hiyo, mambo ya Iringa siwezi kuyazungumza na kama tutaanza kila Kamanda kuzungumza jambo hilo hamuoni kuwa itakuwa ni kama vurugu?"


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani alikanusha pia kuwapeleka askari wake Iringa akisema: "Hizo taarifa siyo za kweli. Hakuna askari yeyote aliyekwenda Iringa wakati wa vurugu zile."

  Maswali ya kujiuliza
  Kwa nini askari waliochukuliwa kwa siri hata bila wenzao kujua?
  Kwanini makamanda wa mikoa walipoulizwa na mwananchi kuhusu sakata hili wamekuwa waoga kusema ndio au hapana kama ni utaratibu wa kawaida kupeleka askari wa ziada Iringa. Na je, mbona haikutangazwa? Kwani siri? Kwa nini Kamanda wa Mkoa wa Mbeya alidanganya kwa kusema hapana wakati jibu ni kweli askari wake walienda Iringa? Je, askari kutoka Mbeya walitoroka? Nini malengo yao.
  Sasa mimi nikihitimisha kwamba askari hawa walikuwa na lengo maalum, ninakosea?
  NB; Ifahamike kuwa askari hao wanaletwa Iringa wakati Chadema walishakubali kuendelea na mikutano ya ndani kupisha sensa badala hadhara na hakukuwa na mvutano mkubwa baina yao uliohitaji nguvu kubwa kiasi hicho.

  Hoja ya pili ni kauli za viongozi hasa J. Tendwa na Waziri Nchimbi.
  Msajili wa vyama John Tendwa na Waziri Nchimbi kwa nyakati tofauti wanatoa hoja za kuilaumu zaidi Chadema, huku Tendwa akitishia kufuta Chadema. Wote hawa, wanajua kwamba ktk vifo vyote hivyo, hakuna kosa la dhahiri lililofanywa na viongozi au wanachama wa kawaida. Badala yake wao wamekuja kudhihirisha kile ambacho mtonyaji wangu aliniambia kuwa lengo ni kupunguza nguvu ya Chadema kwa kuitungia sheria mbovu, kuichafua, kuwatisha wananchi ili wasusie chama hicho na ikiwezekana waifute, japo ktk kuifuta hawakoserious.
  Hii taarifa ya Molemo nayo inatisha.

  NB;Wakati huo huo, usisahau kwamba mrithi wa Shehe Yahaya Nape Nnauye alitabiri kifo cha Ali Zona pale alipowatahadharisha wananchi wa Morogoro redioni siku mmoja kabla kuwa wasiende ktk mikutano ya Chadema Morogoro kwa sababu vurugu zitatokea. Mtabiri Nnauye alipatia na mtu akafa. Je, yeye ni mtabiri mzuri au alijua kitakachokea? alijuaje?


  Mwisho ni je, jitihada zao zimefika mwisho? Muda utatuambia. tafakari.

   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mungu kama ameshafuta CCM hata waseme kwa mbinu zote itafikia mwisho tu!!!
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  walipanga kuua sasa wameumbuka, maneno ya msajili aloitakiwa kuyatoa baada ya kifo kaedit kidogo... badara ya kukifuta CDM, tutafua vyama vitakavyo sababisha vifo....
   
 4. P

  Paul J Senior Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ufisadi na wizi wa rasilimali za nchi hauwezi kuendelea kuiweka ccm madarakani na haya mapolisi yasipotumia akili kama makada wa ccm raia tukiamua tunauwezo wa kuwathibiti in a calm manner!
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Nilimsikia jana kwenye taarifa anasema, vyama vyenye vurugu vitafutiwa usajili

  Nikawaza, anayo malaka hayo kisheria?? na vurugu za kusababisha chama kuvutwa zutapimwaje??

  Kumbe ndio mswada unaandaliwa??

  Kila kitu kinakuja na kupita, ilianguka Rumi miaka hivyo sembuse hawa.

   
 6. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Hata Farao, ilifika mwisho akasalimu amri...akawaacha waende zao Kanani!!!
   
 7. m

  malaka JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hawa hata wakiua watu 100 hawawezi kuepuka kifo chao 2015. Jiulize, ni mtu gani atakayekuwa na uwezo wa kusimama na kuomba kura kwa watu akipeperusha vilivyo bendera ya CCM leo? Labda maeneo ya Pwani, Je Mbeya? Arusha? Iringa? Songea? na kwengineko?
   
 8. masatujr1985

  masatujr1985 JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 1,933
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mi nilishasema "nachukia kazi inayofanywa bila kushirikisha ubongo". Hawa wawili Zelote Stephen na Kamhanda ni wahusika wakubwa na damu hizi zitawarudia tu.
  N.B: Tanzania ijiandae kwa kizazi cha visasi maana watoto wa ndugu zetu wanaouwawa pasi na hatia lazima watakuja lipiza vifo vya wazazi wao. Take my words
   
 9. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #9
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu wimbo wa TAIFA mi naona tuubadilishe na kuimba nyimbo za mashujaa alfajiri na umande wa wakati huo hali ilipokua shwari, si shwari tena na hali ya hewa imebadilika. Tunahitaji kubadilika pia kwani enzi za kukemea maovu na kuwafunga wasaliti zimekwisha kwani wasaliti ni ndugu zetu wa damu na mashemeji zetu.

  Naona TANZANIA inataka kumeza bomu badala ya kumrushia adui...So ingeneous Tanzania.
  What difference does it make to the dead, the orphans and the homeless, whether the mad destruction is wrought under the name of totalitarianism or the holy name of liberty or democracy?
   
 10. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  nguvu hii ya police iliotumika kuzia siasa za cdm iringa na moro ingetumika kule kwenye wizara ya mali asili na utalii kuzuia ufisadi .........mbona tungejenga majumba na dawa nk kwa wananchi wetu kibao
   
 11. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nasema hakuna marefu yasiyo na ncha, je nani katika Afrika aliyekuwa na Jeshi Imara na vifaa vya kisasa kuliko hata baadhi ya nchi zilizoendelea kama Gadaffi, je huyo shupavu wa jeshi leo yupo wapi?

  mwenye akili hawezi kupuuza ukweli bali atahakikisha ukweli unashinda mbele ya uongo
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa chadema siyo Rangi, Bendera, kadi au mavazi peke yake, nadhani hawezi kufuta. Lengo hapa ni kuchafua au kupitisha sheria mbovu. Kwa sababu kufanikisha hilo lazima uwafute pia viongozi wote akina Mbowe na Slaa ili ufanikiwe. Maana wote wakihamia Chausta wakashinda majimbo yote ya sasa ya Chadema watakuwa wameiongezea umaarufu. Chadema iko kwenye mioyo ya watanzania. Huwezi futa fikra zinazotaka mabadiliko.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na logic ya mleta mada. Tukio zima lilipangwa na kama tujuavyo , kwenye uovu haapachi kuacha trace. \

  Matamko ya akina Tendwa na Nchimbi yaliandalaiwa lakini kama ilivyo movie ya Mabwepande imejidhihirisha wazi mbele za watu wote kwamba wameua wao kwa bomu close range na Mungu akawaanika wazi. Aliyepiga zile picha anastahili pongezi nyingi mno maana wangemgundua lazima wangempiga bomu usoni. Kama sio hizi picha hiyo movie yao ingeleta taswira tofauti. Tena wakabuni mbinu za kutuma sms kwa IGP eti Dr. Slaa aonekane ndie aliyeinjinia sakata hilo.

  Ukiangalia hata bila umakini utaona kwamba CCM hawajijui hadi sasa hivi. Hawajui ni jinsi gani Watz wamewachukia, kwa hiyo wanadhani wanaweza kuwaconvince tena. Mwisho inakuwa kama watoto wanaocheza makida makida. Hopeless kabisa.
   
 14. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CDM wameridhika na yote yanayotokea ndio maana hawataki kufanya maamuzi magumu kwa Imani kuwa wataitoa ccm 2015 Mimi sio mtabiri lakini nawaapia CDM hamtoweza kamwe kuitoa ccm madarakani kwa kipande cha karatasi au kura sahauni ccm imeshika mpini Na wako tayari kumuua Hata yesu Angekuweko ili mradi wabaki madarakani......viongozi wa juu CDM chukueni maamuzi magumu na muache kuimba taarabu Kama Nape

  Hii taarifa ya Molemo nayo inatisha.

  NB;Wakati huo huo, usisahau kwamba mrithi wa Shehe Yahaya Nape Nnauye alitabiri kifo cha Ali Zona pale alipowatahadharisha wananchi wa Morogoro redioni siku mmoja kabla kuwa wasiende ktk mikutano ya Chadema Morogoro kwa sababu vurugu zitatokea. Mtabiri Nnauye alipatia na mtu akafa. Je, yeye ni mtabiri mzuri au alijua kitakachokea? alijuaje?


  Mwisho ni je, jitihada zao zimefika mwisho? Muda utatuambia. tafakari.

  [/QUOTE]
   
 15. M

  MTK JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Yote hayo ni kutapatapa kwa mfa maji tu wala usihofu lolote; watahangaika sana wataua watu wengi na watafanya kila uchafu ili kujinusuru lakini mabadiliko yatakuja na yatafika ufukweni, the moment watu wakishajitambua hakuna jinsi ya kuzima vuguvugu hilo, haki ya mtu haipotei bali wanaweza kuichelewesha tu, na kwa bahati mbaya kila wanavyojaribu kulizima vuguvugu ndivyo pia watu wanavyojenga usugu dhidi ya uonevu.

  Wakomunisti hawakuweza kuzuia kuanguka kwa ukuta wa Berlin, Gaddafi hakuweza; aliowaita cockroach na panya waliweza kumfanya akajifiche mtaroni, Mubarak hakuweza Misri, Ben Ali wa Tunisia hakuweza, Assad hajaweza Syria; miezi 18 tangu vuguvugu lianze licha ya ukatili wote huo tunaoushuhudia kila kukicha! Makaburu hawakuweza Sauzi, Angola, Namibia, Msumbiji vivyo hivyo, Moi hakuweza Kenya, Amini hakuweza Uganda, Pinochet hakuweza Chile; orodha ni ndefu!

  And afterall historia inatuonyesha kwamba watawala huwa hawakubali kuachia ngazi kwa hiari mpaka wasukumwe; historia hiyo hiyo inatuonyesha pia kwamba wananchi nao wakishajitambua watasonga mbele kwa gharama yoyote mpaka kieleweke. mifano ni kama hapo juu!

  Hakuna kitu kinachoweza kuzuia nguvu ya umma kwa sababu umma ndio unaowaweka watawala madarakani
  ; umma ukisema tumechoka itakuwa ni sauti ya Mungu; kwa hiyo basi kama Mungu yuko upande wa umma nani atakuwa kinyume chao!?

  Might is not neccessarily right, and when improperly applied it becomes evil; and all evil empires will eventually fall, ours being no exception! And because right is devine, it will always rise up and win against any adversity.
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kweli hakuna marefu yasiyo na nchi, nakubali;
  Unakwenda Asia kununua mtambo wa kuingilia simu za watu ili uwabambikizie kesi - unakwama.
  Unamkamata mtu unampiga na kumwua kisha unamtupa mabwepande - Kumbe hajafa anafufuka.
  Unaanza harakati za kuchafua chama na kutunga sheria mbovu - siri zinavuja kabla.
  Unapanga deal la kuwapoteza akina Slaa, Mnyika na LEMA-- Wenzako wanakusaliti wanatoa siri.
  Sasa huko kama siyo kufika mwisho ni nini?

   
 17. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ......... NGUVU YA UMMA NA KUDRA ZA MUNGU is our last hope to win the ccm's brutality
   
 18. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,488
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  aisee ubarikiwe umesema yote hii thread ifungwe kuchangiwa umesema yote,tuone Msajili wa vyama Tendwa na Mwenyezi Mungu nan msajli zaidiinfact ccm ilishafutika kwenye moyo ya wa TZ wengi,Nape anaushahdi wa hili,ccm imebaki kwenye mafle ya Tendwa
   
 19. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sadam, Gadafi, Osama bin Laden, Milosovic, Mubarak, etc sembuse hawa? Nini bhana wataaibika sana
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Umeleta kitu kipya ambacho sikuunganisha dots zangu mwanzoni.
  Unataka kusema kwamba msg zile wanazodai zilitoka kwa Dr Slaa kwenda kwa mwema, kama picha isingekuwepo, lengo lake lilikuwa ni kuonesha kwamba Dr Slaa ndiye alipanga vurugu zilizoleta kifo cha mwandishi? kama ndivyo tuko pabaya zaidi.

  Vile vile naanza kuunganisha hii stroy na umakini mzuri uliotumika kuchagua baadhi ya askari kutoka mikoa ya jirani tena bila askari wengine kujua ili kuja kutekeleza movie hii.
   
Loading...