Kuvaa suti ikiwa na lebo mkononi

mathabane

JF-Expert Member
Jan 27, 2013
2,406
1,889
Habarini wandugu,

Naomba wataalamu wa mambo ya mavazi wanipe elimu kuhusu hili jambo katika uvaaji wa suti zikiwa na label mikononi. Sijajua ni lipi sahihi kati ya haya; Unaponunua suti hizi ready made mara nyingi zinakuwa na label kwenye mkono hasa wa kushoto, kuziondoa ama kuziacha.

Nimeona watu wengi huvaa zikiwa na label yake hivohivo. Mimi binafsi huwa sijisikii huru kuvaa suti ikiwa na hizo label mikononi, hivyo huwa nafanya mpango wa kuziondoa kabla ya kuzivaa.

Sasa ningependa kusikia kwa wengine nini mtizamo sahihi maana nimeona watu wengi tena maarufu kama wasanii na wafanyabiashara wa kati nao huwa hawaondoi hizi label ila sijawahi ona viongozi wa juu wa kitaifa wakivaa suti zikiwa na ma-label mikononi.
 
Habarini wandugu.
Naomba wataalamu wa mambo ya mavazi wanipe elimu kuhusu hili jambo katika uvaaji wa suti zikiwa na label mikononi.
Sijajua ni lipi sahihi kati ya haya: Unapo nunua suti hizi ready made mara nyingi zinakuwa na label kwenye mkono hasa wa kushoto, kuziondoa ama kuziacha. Nimeona watu wengi huvaa zikiwa na label yake hivohivo. Mibinafsi huwa sijisikii huru kuvaa suti ikiwa na hizo label mikononi, hivyo huwa nafanya mpango wa kuziondoa kabla ya kuzivaa.

Sasa ningependa kusikia kwa wengine nini mtizamo sahihi maana nimeona watu wengi tena maarufu kama wasanii na wafanyabiashara wa kati nao huwa hawaondoi hizi label ila sijawahi ona viongozi wa juu wa kitaifa wakivaa suti zikiwa na ma-label mikononi.
Kuvaa suti na label mkononi ni mistake kubwa sana kwenye fashion. Label inatakiwa iondolewe.
 
Wanatangaza biashara pia ili wakuaminishe kavaa ya kampun gan usihis ya kale
 
Kuna siku nimemwona mtangazaji wa habari ITV kavaa suti yenye lebo. Inatakiwa iondolewe
 
Kuvaa nguo yenye labels za kampuni fulani ni kuifanyia matangazo ya kibiashara hiyo kampuni bila kulipwa chochote! Wenzenu hua wanavaa nguo zenye labels za kampuni kwa kulipwa.
 
3c7b65e4b08be5982a15c0214e4099eb.jpg
 
Back
Top Bottom