Kuuza bidhaa katikati ya barabara si busara

Kuuza bidhaa katikati ya barabara si busara

[emoji16][emoji16][emoji16]Kwamba watu watarestishwa inpeace

Kingsmann

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Sio muda mkuu wamejaa kama bamia kwenye kapu,katikati ya barabara,high way kwenye round about, angalia hiyo picha vizuri umbali waliochukua wakaiacha lami nyuma.
IMG_20210308_133038_412.jpg
 
Sio muda mkuu wamejaa kama bamia kwenye kapu,katikati ya barabara,high way kwenye round about, angalia hiyo picha vizuri umbali waliochukua wakaiacha lami nyuma.View attachment 1720336
Na bado.

Katika miaka 10 ijayo population ya Dar inaweza kufikia watu milioni 14 kirahisi sana.

Hiyo ni zaidi ya double population ya sasa.
 
Ngoja utawasikia sio muda yaani ikitokea bahati mbaya gari limekata break mtegemee kusikia makubwa.
Mkuu pole sana. Najua ni jambo la kukasirisha na kushangaza lakini ukishakuwa na mtawala ambaye anaongozwa kwa hulka zake, tena mbovu kabisa, hakuna namna. Yeye anadai ndiyo wapiga kura wake. Mbegu anayopanda imeshamea na itachukuwa muda mrefu kuja kuiondoa. Huwezi kuwa na nchi ambayo haina utaratibu. Kila sehemu haiwezi kuwa sehemu ya biashara. Wengi wanadhani hasara ya hili jambo ni usumbufu kwa watu wengine au ajali kuweza kutokea, lakini mimi naona kuna zaidi. Hawa watu kadiri muda unavyokwenda ndivyo wanavyozidi kuongezeka na kufanya biashara kiholela. Kuna siku isiyo jina litakuja kutokea la kutokea na watageuka kuwa jeshi litakaloipundua nchi. Wanaoshabikia hii hali hawaoni mbali. Vurugu ni rahisi sana kutokea na ikishatokea kuwamudu itakuwa ngumu sana.
 
Na bado.

Katika miaka 10 ijayo population ya Dar inaweza kufikia watu milioni 14 kirahisi sana.

Hiyo ni zaidi ya double population ya sasa.
Kusema ukweli hali ya Dar siku zijazo ni ngumu. Ukipita sehemu zinazoitwa za ''uswazi'' watoto wenye umri kati ya miaka miwili mpaka kumi ni wengi kweli kweli. Utafikiri unapishana na sisimizi.
 
Na bado.

Katika miaka 10 ijayo population ya Dar inaweza kufikia watu milioni 14 kirahisi sana.

Hiyo ni zaidi ya double population ya sasa.

Tuombe tu kwamba hawa jamaa wa Corona Project wasifanikiwe ajenda yao, sawa!???
 
Yaani mkuu hii nchi ina mambo ya kipuuzi sana,yaani robo tatu ya barabara imejaa vitunguu na nyanya magari hayapiti kwa muda,watembea kwa miguu shida tupu,eti sababu ya WANYONGE upumbavu mtupu.
Mkuu hali hiyo ipo kwenye miji yote. Yaani unawakuta wachoma mahindi, wakaanga samaki, wapika chapati na vitumbua wote wameweka majiko yao juu ya lami. Yaani Lissu hajakisea aliposema tuna Rais wa ajabu haijawahi tokea. Mkuu kana baadhi ya barabara yamefungwa na Wamachinga hata wale wanaowategemea kama Wateja wao hawana mahali pa kupita kufanya manunuzi.
 
Yaani Mwanza kweli wamezidi kukaa barabarani mpaka kero Ila nimekuja huku mbeya nimepapenda kweli hakuna huo ujinga barabarani Ila nimefanya uchunguzi wangu nimeona kwasababu ya baridi na Mvua inafanya machinga wakae kwenye masoko yao na huko Mwanza itabidi muombe Mvua inyeshe kila siku Ili waombe masoko bila kupenda.
 
Sio muda mkuu wamejaa kama bamia kwenye kapu,katikati ya barabara,high way kwenye round about, angalia hiyo picha vizuri umbali waliochukua wakaiacha lami nyuma.View attachment 1720336
Kusema ukweli hali ya Dar siku zijazo ni ngumu. Ukipita sehemu zinazoitwa za ''uswazi'' watoto wenye umri kati ya miaka miwili mpaka kumi ni wengi kweli kweli. Utafikiri unapishana na sisimizi.
Na hao wakianza kufikisha miaka 18 wanaanza kuzaana.
 
Wakuu salaam;

Katika pilika pilika zangu za hapa na pale nimekutana na hali ambayo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubariana nami kuwa huku sio kuwajali au kuwapenda wafanyabiasha wadogo maarufu kama (machinga), bali ni kuwajaza ujinga na kuwahatarishia maisha yao na (wao pia kujiweka katika mazingira ya kupoteza maisha au hata vilema vya kudumu).

Ukifika katika mji wa Mwanza utashika kichwa na kustaajabu kuona jinsi gani akili za watanzania wengi (wenye mamlaka na wasio na mamlaka) hazifanyi kazi kwa busara.

Kwanini nasema hivi? Katika hali isiyo ya kawaida katika makutano ya barabara (round about) za Pamba na Nyerere wafanya biashara wamepanga bidhaa hadi katika ya barabara, robo tatu ya barabara imejaa vitunguu, nyanya ndimu/limao dagaa, mchicha na watu,barabara ambayo inaruhusu magari kuanzia matatu kwenda kwa pamoja sasa haiwezekani linakwenda gari moja tena kwa tabu watu wamejaa barabarani round about eti wanafanya biashara!

Huu ni zaidi ya upumbavu, serikali ya jiji inaona na inakusanya mapato njia zimeziba watu wanauza tembele katikati ya barabara.

Huu si uzalendo au kuwapenda wafanyabiasha ni kuwatafutia vifo na vilema vya maisha, barabara ni sehemu ya kuheshimu na hazitakiwi ku be blocked, tujifunze kwa wenzetu, huwezi kuta shughuli za ajabu ajabu barabarani wala kwenye hifadhi ya barabara.

Serikali ya jiji la Mwanza litafutieni ufumbuzi suala hili, isijifiche kwenye mwanvuli wa serikali ya wanyonge, hali ya kuwa maisha ya hao wanaoitwa wanyonge yako hatarini.

Zaidi ya kusababisha foleni zisizo na msingi na adha kwa waenda kwa miguu,inahatarisha maisha ya wauzaji na wanunuzi kwa kiwango kikubwa mno.

Napendekeza watu hawa watafutiwe sehemu nzuri na salama wafanye biashara na waliingizie taifa kipato na wao pia wapate kuendesha maisha yao,kuuza bidhaa hadi katikati ya barabara italeta maafa hivi karibu,sipendi itokee ila bila kuchukua tahadhali haliwezi kuepukika.

View attachment 1720275
Siyo Mwanza tu hiyo ni kwa Tanganyika yote
 
Kiukweli inakera sana,siasa inatumika vibaya sana kwenye mustakabali wa maisha ya mtanzania.
Mwaka jana walikufa wawili hapo round about ya nyerere road.
Alafu yametengwa masoko, lakini unakuta hayatumiki ipasavyo,kisa kulinda ahadi za uchaguzi,na inaharibu kabisa taswira ya mkoa.
Mamlaka husika zichukue hatua stahiki mapema kurekebisha hili, maana linachangia na misongamano isiyo na lazima,uchafuzi wa mazingira na kuchangia ongezeko la magonjwa,hasa wakati hii wa covid-19
 
Mkuu hali hiyo ipo kwenye miji yote. Yaani unawakuta wachoma mahindi, wakaanga samaki, wapika chapati na vitumbua wote wameweka majiko yao juu ya lami. Yaani Lissu hajakisea aliposema tuna Rais wa ajabu haijawahi tokea. Mkuu kana baadhi ya barabara yamefungwa na Wamachinga hata wale wanaowategemea kama Wateja wao hawana mahali pa kupita kufanya manunuzi.
Yaani hii nchi hii basi tu,viongozi wa kujaribu hawa ni tatizo kubwa, watanzania wengi elimu ndio shida,eti mtu akijua kupayuka na kuongoea ujinga huyo ndiye kiongozi bora,haijalishi anafuata kanuni, taratibu na sheria za nchi au la.
 
Kiukweli inakera sana,siasa inatumika vibaya sana kwenye mustakabali wa maisha ya mtanzania.
Mwaka jana walikufa wawili hapo round about ya nyerere road.
Alafu yametengwa masoko, lakini unakuta hayatumiki ipasavyo,kisa kulinda ahadi za uchaguzi,na inaharibu kabisa taswira ya mkoa.
Mamlaka husika zichukue hatua stahiki mapema kurekebisha hili, maana linachangia na misongamano isiyo na lazima,uchafuzi wa mazingira na kuchangia ongezeko la magonjwa,hasa wakati hii wa covid-19
Yaani sio hapo tu mkuu ukienda kule jiji ndio hovyo kabisa,biashara juu ya lami, barabara kuvuka hovyo hovyo bila tahadhali yaani tabu tupu.
 
Taifa lililogeuka wachuuzi wa bidhaa za wachina unategemea nini cha ziada?
Hicho ulichokiona ni symptoms tu za tatizo kubwa zaidi.
 
Afu likitokea la kutokea anatafutwa mchawi nani,watu hawajihurumii ila yote hii ni sababu ya umaskini

Kingsmann

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Naam tena wanakuwa wa kwanza kuandika salama za rambirambi Twitter kuwa wamesikitishwa sana,na wako pomoja na familia za wahanga katika kipindi hicho kigumu,ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom