Kuuza bidhaa katikati ya barabara si busara

Kuuza bidhaa katikati ya barabara si busara

Invigilator

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
3,219
Reaction score
6,080
Wakuu salaam;

Katika pilika pilika zangu za hapa na pale nimekutana na hali ambayo kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubariana nami kuwa huku sio kuwajali au kuwapenda wafanyabiasha wadogo maarufu kama (machinga), bali ni kuwajaza ujinga na kuwahatarishia maisha yao na (wao pia kujiweka katika mazingira ya kupoteza maisha au hata vilema vya kudumu).

Ukifika katika mji wa Mwanza utashika kichwa na kustaajabu kuona jinsi gani akili za watanzania wengi (wenye mamlaka na wasio na mamlaka) hazifanyi kazi kwa busara.

Kwanini nasema hivi? Katika hali isiyo ya kawaida katika makutano ya barabara (round about) za Pamba na Nyerere wafanya biashara wamepanga bidhaa hadi katikati ya barabara, robo tatu ya barabara imejaa vitunguu, nyanya ndimu/limao dagaa, mchicha na watu,barabara ambayo inaruhusu magari kuanzia matatu kwenda kwa pamoja sasa haiwezekani linakwenda gari moja tena kwa tabu watu wamejaa barabarani round about eti wanafanya biashara!

Huu ni zaidi ya upumbavu, serikali ya jiji inaona na inakusanya mapato njia zimeziba watu wanauza tembele katikati ya barabara.

Huu si uzalendo au kuwapenda wafanyabiasha ni kuwatafutia vifo na vilema vya maisha, barabara ni sehemu ya kuheshimu na hazitakiwi ku be blocked, tujifunze kwa wenzetu, huwezi kuta shughuli za ajabu ajabu barabarani wala kwenye hifadhi ya barabara.

Serikali ya jiji la Mwanza litafutieni ufumbuzi suala hili, isijifiche kwenye mwanvuli wa serikali ya wanyonge, hali ya kuwa maisha ya hao wanaoitwa wanyonge yako hatarini.

Zaidi ya kusababisha foleni zisizo na msingi na adha kwa waenda kwa miguu,inahatarisha maisha ya wauzaji na wanunuzi kwa kiwango kikubwa mno.

Napendekeza watu hawa watafutiwe sehemu nzuri na salama wafanye biashara na waliingizie taifa kipato na wao pia wapate kuendesha maisha yao,kuuza bidhaa hadi katikati ya barabara italeta maafa hivi karibuni,sipendi itokee ila bila kuchukua tahadhali haliwezi kuepukika.

IMG_20210308_133140_257.jpg
 
Nchi hii ukishakuwa na kitambulisho cha mjasiriamali, unaruhusiwa kufanya biashara popote pale unapotaka na hakuna wa kukufanya lolote.

Uamuzi ni wako tu, maana Baba yetu ni mtetezi wa wanyonge.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nchi hii ukishakuwa na kitambulisho cha mjasiriamali, unaruhusiwa kufanya biashara popote pale unapotaka na hakuna wa kukufanya lolote..
Yaani mkuu hii nchi ina mambo ya kipuuzi sana,yaani robo tatu ya barabara imejaa vitunguu na nyanya magari hayapiti kwa muda,watembea kwa miguu shida tupu,eti sababu ya WANYONGE upumbavu mtupu.
 
Naona ubungo wamewatoa kimya kimya
Cheap politics kwenye maisha ya watu hazitakiwi,kutaka sifa eti unajali wanyonge kumbe unawapalia makaa ya moto,mkuu nakwambia watu watavunjwa miguu sio muda.
 
Mjadala mzuri, nadhani tuwaache mpaka litokee la kutokea halafu wakurupuke na matamko
Mkuu sio muda wanaendelea kusogea yaan gari linapita miguuni kwao kabisa,wamekaa na nyanya na vitungu kwenye lami,high way halafu round about.
 
Back
Top Bottom