Kuuwa tembo na kukutwa na pembe za tembo

Apr 6, 2012
97
0
Ulikuwa unakatiza porini, ukakuta tembo amekufa, na ameanza kuoza. Ukapaki baiskeli yako nakuanza kuukagua mzoga ule, ukaona pembeni mavi ya tembo ukakumbuka kuwa yatakufaa kutibu degedege pindi mmoja wawatoto wako atakapo ugua, ukachukua yakutosha katika kapu lako. Ukiwa unajiandaa kuondoka, ukakumbuka jambo akilini kuwa meno na pembe za ndovu ni mali, ukausogelea mzoga wa tembo yule nakuanza kuchomoa pembe zake mbili pia na meno yake, ukafunga vizuri kwenye baiskeli yako ukaanza kupiga pedeli kuelekea nyumbani kwako. Ukiwa njiani unakutana na askari wanyama pori wanakusimamisha na kuanza kukukagua nakukuta na MAVI YA TEMBO, PEMBE ZA TEMBO NA MENO. Unafungwa pingu nakufikishwa mahala panapokustahili kwani umekutwa na nyara za serikali. Sasa hapo wakuu naomba niulize kitu, hapo nitafunguliwa mashtaka mangapi kwa mujibu wa sheria? Je! nitahesabika kuwa mimi ndiye niliye muua tembo? Siruhusiwi kubeba vitu vile nilivyoviokota na nibora niviache viozelee porini?
Naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom