Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
meno.jpg


Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Askari wa Uhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa Ruaha wanamshikilia Cyprian Kasula miaka 42, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kipera kwa tuhuma za kukutwa na kichwa cha Tembo kikiwa na meno yote mawili katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Iringa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa wanamshikilia Cyprian Kasula miaka 42, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kipera akiwa na kichwa cha Tembo kikiwa na meno yake mawili, Nyama ya Tembo, Mkia wa Tembo, Silaha tatu za kienyeji aina ya Gobore, Vipande vya nondo 35, makopo matatu ya unga wa baruti na Panga moja.

ACP Bukumbi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa amekaa porini chini ya mti pamoja na mwenzake mmoja ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kuona askari wamefika eneo hilo na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Mtuhumiwa mwingine anayeshikiliwa ni Agnes Chaula miaka 38, mama lishe na mkazi wa Mwangata D kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitano vya meno ya Tembo.

ACP Bukumbi amesema kuwa mama lishe huyo anatuhumiwa kujihusisha na uwindaji haramu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Jamhuri
 
Back
Top Bottom