kuunganisha kompyuta kwa kutumia Ad-Hoc Network. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuunganisha kompyuta kwa kutumia Ad-Hoc Network.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by gwaya, Apr 1, 2011.

 1. g

  gwaya New Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika suala zima la mawasiliano hasa bila kutumia nyaya(yani wireless communication) tuna aina mbila za toplogy, ya kwanza uitwa Ad-Hoc Network topology na aina ya pili uitwa infrastructure network topology .


  Ad-Hoc Network topology :hii ni aina ya topology ambayo mara nyingi utumika wakati tunaitaji kutegeneza netiweki ambayo itawezesha kompyuta kwa kompyuta ziweze kuwasiliana bila ya kutumia access point kwa njia ya wireless,access point inaweza ikawa router,switch au base station.
  Mara nyingi Ad Hoc netweki zinatumikaga kwenye vikao,wahusika wa kikao wanaweza kubadilishana mawazo, kutumiana mafaili au data nyingine kwa kutumia kompyuta zao bila ya kurupushani.Aina hii ya netiweki utumika kwa muda mfupi tu kwahiyo topology yake sio fixed na inaweza kubadilika muda wowote.


  [​IMG]

  Infrastructure network topology :Aina hii ya topology mara nyingi utumiwa na Service Providers(kama vile Vodacom au TTCL na nk)ili kutua huduma kwa wateja husika.
  Mtu binafsi huwezi kutengeneza topology kama hii kwani huitaji manunuzi ya vifaa tata kama vile Transceiver,Antennas,Amplifier,Repeater,Base station,Cable na vifaa vinginevyo ili kuweza kukamilisha mfumo.Pia uhusisha manunuzi ya frequency band kutoka serikalini.Lakini Ad Hoc network utumia frequency ambazo hazilipiwi.
  [​IMG]


  Infrastructure network topology pia uhusisha manunuzi ya frequency band kutoka serikalini.Lakini Ad Hoc network utumia frequency ambazo hazilipiwi,
  na hakuna management yoyote inayo itajika baada yakuwa umefanya setingi kwenye operating system ya computers ambazo unataka kuziungnisha,kwa
  upande wa infrastructure network topoplogy unaitajika husimamizi wa hali ya juu kuweza kumonita utendaji wa mfumo kila wakati.


  Kijarida hiki kinaelezea jinsi ambavyo tunaweza kuziunganisha computer mbili au tatu ili ziweze kuwasiliana kwa kupitia Ad-Hoc Network, window xp itakuwa kama mfano katika kukamirisha zoezi ili.Cha muhimu kabisa lazima huakikishe computer ambazo unataka kuziunganisha kwa kupita radio channel zina wireless network interface cards ambazo hazina matatizo.


  Nitachukulia tuna computer tatu, kwanza itabidi ufanye setingi zifuatazo kwenye computer moja(host computer) ili nyingine mbili ziweze kuidetect baadae na kuunda Ad-Hoc network:


  1.kwenye desktop yako: bofya Start>Control panel>Network and Internet Connections>Network Connections.


  2.Bonyeza kwa kutumia upande wa kulia wa mouse yako kwenye neno”Ethernet Network Connections” alafu changua “properties”,”Andvanced” tiki maneno “Allow other network users to connect through this computer’s Internet connection” na ondoa tiki kwenye maneno “Allow other network users to control or disable this shared Internet connection “(kwa computer zote tatu lazima zifanyiwe hii setingi).  [​IMG]  3.kwa kutumia upande wa kulia wa mouse yako bonyeza “wireless network connection” alafu bonyeza “properties”,baada ya kufunguka kwa window changua “Wireless Networks” bonyeza neno “add” andika jina lolote ambalo unaona ni safi kwa hiyo ad-hoc network kwenye kibox mbele ya maneno “Network name (SSID)”.Unaweza kuchagua kutumia paswedi kwa ajiri ya usalama au husitumie,na hii paswedi itatumika kwa kompyuta nyingine ili ziweze kutegeneza netiweki.
  [​IMG]


  Sasa inabidi uiwezeshe computer ya pili hiweze kuwasiliana na computer ya kwanza(host computer),mpaka hapa computer zote mbili zilizobakia zitakuwa tayari zimekwisha detetect kuwepo kwa Ad-Hoc network kwani zinaweza kupokea signal kutoka kwenye computer ya kwanza lakini bado zinakuwa haziwezi kuwasiliana mapaka zifanyiwe setingi mbili tatu.


  4.Kompyuta zote mbili tayari zitakuwa zime detect kuwepo kwa network,bonyeza kwenye “task bar” kama inavyo onekana kwenye picha chini,utaliona jina la network husika bonyeza jina la network (kwa mfano tenda) ita connect moja kwa moja na kama uliseti paswedi kwenye host computer ita kuamru paswedi kwanza then ndio itaconnect.
  [​IMG]


  Mpaka hapa tayari utakuwa umeweza kutetengeza ad-hoc network! mawazo yana karibishwa,maswari maoni na n.k.


  Wadau si mbaya mkiongezea idea nyingine ambazo hazikuwa included kwenye maelezo.  Source:Karibu Kijiji cha ICT-Elimika kwenye ICT kupitia E learning,webcast,podcast,blogs,forums na download
   
Loading...