Kuumbwa BINADAMU/nani kamuumba?

Kuumbwa BINADAMU/nani kamuumba?

Hata Mimi nashangaa Jua kuning'inia juu kwa juu bila kuanguka , mtasema mambo ya gravity, na hiyo nguvu nani kaiweka ? Please!! What's the first cause? Also who caused the first cause ??

Who cause the first caurse is no other than the CAUSA CAUSAN.
 
brother hata Mimi nilikua blind,kupitia mabandiko yako yenye fact na nondo zilizoshiba niliamua kua free minded nikaanza kuona mambo kwa jicho la tatu na niaanza kuishika elimu na kusoma mambo yenye logic na contradictions kiujumla,
Kiufipi kipindi nilipo ingia secondary tu nilianza kua mtu mwenye kuhoji mambo magumu Kama hayo sikupata majibu
Nilikua nashangaza sana mbaka Kuna baadhi ya watu wakasema nimechizika ila misimamo yangu haikuwahi kuyumbishwa
Sio hivyo tu hata kifamilia niliahawahi kalishwa kikao na wafia dini fulani nikanushe maneno yangu nikawaambia walete uthibitisho juu ya huyo wanaesema yupo wakapoteana vikabaki vitisho tu!

Big up mkuu
Haya mambo ukijua kusoma Kiingereza wala hayashangazi.

Tatizo kwetu watu wengi hawajasoma Kiingereza, hususan kusoma kwa utashi wa mtu mwenyewe, si kwa ajili ya mtihani.

Ila ukisoma kidogo tu hata Political Science utakutana na atheism katika Communism, ukisoma kidogo tu dini utakutana na atheism katika Buddhism, ukisoma kidogo tu History au Philosophy utakutana na atheism katika Enlightenment Europe.

Ndiyo maana unaweza kumsikia mzee aliyesoma zamani Edinburgh kama Nyerere anahutubia taifa anasema alikuwa hajui baraza lake la mawaziri nani Mkatoliki nani Mprotestanti, kwa sababu wote wanaapa kwa Biblia moja, na hata siku akipatikana mtu asiye na dini, anaweza kuwa rais, tutakubaliana tu jinsi ya kuapa.

Mzee alisoma mambo ya historia na falsafa anajua.Na hakusema tu hayo, aliishi hivyo, kwa sababu hata msaidizi wake wa muda mrefu Mama Joan Wicken alikuwa ni mtu asiyekubali wala kujali habari za kuwepo Mungu (Agnostic).

Ssa watu wenye upeo na elimu ndogo wakikusikia unakataa uwepo wa Mungu wanakuona bonge la shetani.
 
Hoja ya "first cause" inatokana na ushamba wetu wa kufikiri kwamba mambo yote yapo sawa na mambo ya dunia tunayoiona.

Mara nyingi watu wanaoamini uwepo wa Mungu hutumia hoja ya "ulimwengu usioonekana" kujenga hoja ya kuwepo kwa Mungu, kwa hadithi tu ambazo hazithibitishiki.

Na hutumia hoja ya "first cause" kulazimisha lazima kuwe na first cause, na hiyo first cause ni lazima iwe Mungu.

Mpaka hapo, hata ukiwakubalia kwamba lazima kuwe na first cause, hoja yao ina makosa ambayo kilatini yanaitwa "non sequitur".
Siku ukinipa usahihi wa mantiki katika kuhoji au kuujua ukweli,sitajadiliana tena wewe kuhusu hii kadhia.

Ila sababu najua fika huwezi jambo hili,sidi huwa tuna vunja misingi ya mantiki. Kati ya uhalisia na mantiki kipi kilianza...? Sababu mantiki ni matokeo ya namna ya ufikiriaji wa kimakosa wa kina Aristoto.
 
Unaelewa kwamba hata kuandika hapa umetumia mantiki?

Kwa hivyo kama mantiki ni namna ya ufikiriaji wa kimakosa, na haya uliyoandika hapa ni makosa pia?
 
Ukichunguza sana utaona hizi ni hadithi za kutungwa na watu tu, huyo Mungu anayesemwa hayupo.
Ukiweza kuthibitisha ukweli juu ya uchunguzi huu,kadhalika utarejea nilichokiandika hapo juu. Mtu mwenye akili timamu hawezi kusema haya kisha akiombwa ushahidi na kueleze mchakato wa hadithi hizi na utungwaji wake ulianzaje na ilikuwaje unashindwa. Hapa ndipo unaona madhara ys kuhoji mambo kwa misingi ya mantiki.

Unahitimisha ya kuwa Mungu hayupo kwa jambo usilo kuwa na elimi nalo wala kulidiriki. Nimeshakuuliza zaidi ya mara tatu utueleze hadithi hizo ni zipi na ilikuwaje zikatungwa na ilikuwa lini ? Kuhitimisha kwa mtindo huu ni kuhitimisha kivivu na kufikiri kitoto.

Lakini swali lingine,imekuwaje ukafikia hitimisho pasi na ushahidi ?
 
Unaelewa kwamba hata kuandika hapa umetumia mantiki?
Sijatumia mantiki yoyote sababu uandishi ulikuwepo kabla ya kuwepo mantiki,mantiki ni fani kama zilivyo fani nyingine kama uhandisi umeme,ujenzi,uchawi,ushairi. Laiti kama ungekaa siku na kujiuliza imekuwaje hizi fani zikawepo,hui ujinga wa Mantiki usingekuwa marejeo yako.
Kwa hivyo kama mantiki ni namna ya ufikiriaji wa kimakosa, na haya uliyoandika hapa ni makosa pia?
Si kweli sababu,hapa naandika uhalisia,na mantiki inajiweka mbali sana na uhalisia kwa namna yake ya kuhoji na kuhitimisha,kama ulivyo fanya hapa,yaani huwa hamgusi hakika ya hoja bali mnaipitia juu juu,ndiyo maana maisha yenu yote mnaishi katika makosa.

Mimo swali langu liko pale pale,nipe uhakika na utuambie kwanini unarejea mantiki katika hitimisho la jambo pasi na kuwa na ithibati ?
 
Swali dogo tu la kuthibitisha kwamba Mungu yupo linapokuwa halijibiwi kimantiki, na linapigwa danadana za longolongo nyingi sana, linaonesha huyo
Kauli hii inakuwa batili sababu haina uthibitisho. Mathalani nikikwambia fulano hayupo. Kuna njia nyingi za kuonyesha hayupo.

Lakini kwanini jambo lijibiwe kimantiki ? Kwako wewe mantiki ni nini hasa ? Lakini je kutokujibiwa kwa swali ni kweli kunaonyesha kutokuwepo kwa Mola ? Lakini je kweli swali hilo halijibiwi ? Jibu laa hasha,bali nijabiwa na limeshajibiwa sana. Shida ipo kwenu hamtaki kuukubalo ukweli na hoja hamna.
 
Elimu ya kumjua Mungu ipo katika realm tofauti na hii casual realm, hii ni sawa katika physics kuna Classical physics na modern physics, kuna mambo huwezi kuyatanzua kupitia classical physics ila lazima upitie modern physics halikadhalika kumjua Mungu kuna njia zake alizotuwekea na wala sio hizi njia za crude-casual analysis ambazo watu wasiojua wamejitungia kulingana upeo wa akili zao.

Kumjua Mungu yataka unyenyekevu mbele yake ili ajidhihirishe kwako na sio Egos za nafsi kwani Mungu ni Supreme.

Kama mtu hajui kucheza mchezo fulani kwanini uulaumu huo mchezo kuwa ni mbaya na asilaumu uwezo wake mdogo wa kuweza kucheza mchezo huo??? Ndio hivyo kutokumjua kwako Mungu usihitimishe kwamba Mungu hayupo bali kagua uwezo wako kiakili uliofanya ushindwe kumjua Mungu, ni mambo Mengi katika Mazingira yetu bali ndani yetu sisi wenyewe yanayotosha kwa mwenye akili kujua kwamba kuna A Conscious Supreme creator.

Wenye busara hutafakari na kuomba msaada ili Mungu azidi kuwaongoza na milango ya perceptions za utambuzi wao izidi beyond the 5 senses.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo asingekuwa mkatili hivyo ajifiche sana, watu wauane katika vita za kidini wakibishana kumtafuta.
Matumizi ya tamko "nge" katika uhojaji,huonyesha dhana,na dhana ambayo iko chini ya asilimia hamsini pasi na kuungwa mkono na shahidi hii haifanyiwi kazi sababu inakuwa ni UONGO.

Mola wetu hajajificha kama unavyodai,sababu kila kitu amekiweka wazi,kauli yako inaonyesha wazi humjui unaye mkanusha,hili nakwambia kila siku.

Weee umejuaje kama angekuwepo asingekuwa hivi alivyo,na huku huns ushahidi wowote na udai hayupo ? Hivi ndivyo mantiki inakifindisha hivi ? Maana naona inakufanya kuwa mjinga zaidi kujadili jambo ambalo huwezi kulithibitisha.

Ushawahi kujiuliza kwanini kuna jihadi ya mapigano ?

Ukatili ni nini na unaupimaje ? Marejeo yako ni wapi kujua ukatili hasa kwa kumnasibishia Mola muumba ?
 
Mungu huyo angekuwepo ingekuwa kila mtu anazaliwa akimjua kwa urahisi tu, bila kuhubiriwa, bila kuhitaji kitabu, bila ya watu tofauti kumjua kiutofauti
Umejuaje hili ?
 
Mpaka hapo tu utaona huyu Mungu anayesemwa na watu katungwa tu na watu.
Kwa uthibitisho gani ? Hizi dhana za "nge" ? Inakuaje unaikosea adabu akili uliyo pewa bure ?

Bado hujathibitisha ya kuwa Mola ametungwa kwa wasi wasi na dhana. Mathalani mimi ndiyo ningekuwa wewe (siwezi kuwa wewe sababu akili yangu inafanya kazi vizuri na kurafakari) ningeshusha shahidi kibao na marejeo tele.
 
I wonder how they know this, mfumo wa engine ni wakushangaza Sana, na si engine tu vitu vingi sana vilivyoundwa na mwanadamu vinashangaza , unajiuliza wamepata wapi hii knowledge ya kutengeneza haya mavitu ,
Wazungu kuna vitu wanavijua na wametuficha sisi maniga.
This knowledge is beyond human thinking capacity, there is someone who transfer this knowledge to white people.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mechanism ya gari ilikua haiwezekani ku imagine kua ipo tu na haina mtengenezaji basi hapo utakubali kua kila kitu ambacho kwako kinakustaajabisha kwa ufanisi wake ni lazima kiwe na chanzo

Gari lina chanzo ambacho ni mtu na mtu actually mtu anaweza kuthibitishika hilo halina ubishi, lakini naye huyo mtu umempachika chanzo chake kua ni "Mungu" je unaweza kuthibitisha?

Je hicho chanzo cha mtu (Mungu) nini kimesababisha chanzo hicho kikawepo? ( chanzo cha mungu)

Itakua ni ujinga kusema gari linamtengenezaji mtengenezaji wa gari anamtengenezaji ila aliyemtengeneza mtengeneza gari hajatengenezwa (hana chanzo)

Mtu anaye kubali chanzo cha mtu (Mungu) kua hakina chanzo, mtu huyo anakua hana tofauti na yule anayesema gari ulimwengu hauna chanzo
Nikiliangalia gari au mfumo mzima wa gari , na kuwa siamini kama mwanadamu ndo ameanzisha huu ufahamu, wazungu kuna kitu wanatuficha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili aliwahi kulizungumza huyu mwamba wa spaceship, mwenye history nzuri sana katika vichwa vya wamarekani

The natural laws of the universe are so precise that we have no difficulty building a spaceship to fly to the moon and can time the flight with the precision of a fraction of a second. These laws must have been set by somebody.”—Quoted from Wernher von Braun, who had much to do with sending American astronauts to the moon.
 
I wonder how they know this, mfumo wa engine ni wakushangaza Sana, na si engine tu vitu vingi sana vilivyoundwa na mwanadamu vinashangaza , unajiuliza wamepata wapi hii knowledge ya kutengeneza haya mavitu ,
Wazungu kuna vitu wanavijua na wametuficha sisi maniga.
This knowledge is beyond human thinking capacity, there is someone who transfer this knowledge to white people.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tofauti kubwa kati yetu na Wazungu ni hii: wao mara nyingi huchukua muda mrefu kushupalia kitu, hawakati tamaa mapema, unapoishughulisha akili yako katika jambo fulani akili inapata mazoezi/mazoea na hicho kitu, mfano bondia au mcheza mpira nk, siku zote hujibidisha kufanya mazoezi ili miili yao iwe mahiri katika michezo husika---- na akili ni hivyo hivyo inahitaji mazoezi ili iwe mahiri katika jambo husika.

Kuna tofauti nyingi ndogo ndogo kati ya watu weusi na wazungu ila tofauti hii ni niliyoitaja ndiyo kubwa zaidi.
 
Elimu ya kumjua Mungu ipo katika realm tofauti na hii casual realm, hii ni sawa katika physics kuna Classical physics na modern physics, kuna mambo huwezi kuyatanzua kupitia classical physics ila lazima upitie modern physics halikadhalika kumjua Mungu kuna njia zake alizotuwekea na wala sio hizi njia za crude-casual analysis ambazo watu wasiojua wamejitungia kulingana upeo wa akili zao.

Kumjua Mungu yataka unyenyekevu mbele yake ili ajidhihirishe kwako na sio Egos za nafsi kwani Mungu ni Supreme.

Kama mtu hajui kucheza mchezo fulani kwanini uulaumu huo mchezo kuwa ni mbaya na asilaumu uwezo wake mdogo wa kuweza kucheza mchezo huo??? Ndio hivyo kutokumjua kwako Mungu usihitimishe kwamba Mungu hayupo bali kagua uwezo wako kiakili uliofanya ushindwe kumjua Mungu, ni mambo Mengi katika Mazingira yetu bali ndani yetu sisi wenyewe yanayotosha kwa mwenye akili kujua kwamba kuna A Conscious Supreme creator.

Wenye busara hutafakari na kuomba msaada ili Mungu azidi kuwaongoza na milango ya perceptions za utambuzi wao izidi beyond the 5 senses.
Isaac Newton THE FATHER OF PHYSICS anakubali Mungu yupo. Kiranga et al wanasema hayupo. Kazi kweli kweli.
 
Ww una uhakika gani Mungu hayupo?
Swali dogo tu la kuthibitisha kwamba Mungu yupo linapokuwa halijibiwi kimantiki, na linapigwa danadana za longolongo nyingi sana, linaonesha huyo Mungu hayupo, katungwa na watu tu.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo asingekuwa mkatili hivyo ajifiche sana, watu wauane katika vita za kidini wakibishana kumtafuta.

Mungu huyo angekuwepo ingekuwa kila mtu anazaliwa akimjua kwa urahisi tu, bila kuhubiriwa, bila kuhitaji kitabu, bila ya watu tofauti kumjua kiutofauti.

Mungu huyo kuwa na utata mwingi kujulikana kwa watu wa dunia nzima, ni ukatili wa hali ya juu, kitu ambacho kina contradict upendo wote anaosemwa kuwa nao Mungu huyo.

Mpaka hapo tu utaona huyu Mungu anayesemwa na watu katungwa tu na watu.

Ndiyo maana utasikia wanampa tabia za watu. Mara Mungu kakaa kwenye kiti cha enzi, sasa Mungu anakaa kwenye kiti anaogopa kuanguka?

Mara Mungu kakasirika, hivi huyu Mungu hana control ya hasira zake? Mungu anayejua kila kitu kitakachotokea anaanzaje kukasirika?

Mara Mungu kaona watu hawamfuati kawaua kwa gharika, ina maana alivyoumba hakujua hawatamfuata?

Mara Mungu ataunguza mabilioni ya watu kwenye moto wa milele.Hivi huyu Mungu anawanyima watu neema ya kumjua, wengine hata kusoma vitabu vyake hawawezi, halafu watu hao awachome motoni milele? Huyu ndiye Mungu mwenye upendo wote kweli jamani?

Ukichunguza sana utaona hizi ni hadithi za kutungwa na watu tu, huyo Mungu anayesemwa hayupo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom