Kuumbuana/kudhalilishana, sometyms kunagharimu

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Wana wa bodi habari zenyu.

Katika safari ya Safina ya Mtume Nuhu, palifikia wakati Nuhu akawa hajui lini safari itafikia ukomo. Aidha wanyama waliokua ndani ya safina waliendelea kujamiana kama ilivyo ada, na kwa maana hiyo waliendelea kuzaana na kufanya idadi ya viumbe kuongezeka kila uchao. Kilichomstua Nuhu ni kuona itafika wakati Safina itazidiwa uwezo wa uzito wa kubeba vilivyomo Safinani, na mwishoe watazama (sinking). Nuhu akaamuru wanyama wote waache kujamiana, na amri hiyo ikaanza kutekelezwa mara moja. Hata hivyo Paka marufuku ama katazo hilo , kwao likawa gumu kulisalimu. Hivyo kwa siri sana wanyama hao walitafuta fursa ama wasaa wakawa wanaendeleza kujamiana.

Aidha ikatokea moja ya siku walizokua wakikulana kwa siri sana, Mbwa akawaona. Mbwa yule hakua wa kukalia jambo! (ni kama wale watu wasemwao akikukuta unakun*a yakalie) Mbwa yule kwa matao akazipeleka habari zile kwa Nuhu. Ingawaje Paka walimsihi sana Mbwa ayakalie wakimtafadhalisha kwamba hata wao walikua wakiiheshimu amri ya Nuhu , na ndiyo maana hawakufanyia tendo lile hadharani, walijificha. Lakini haikusaidia. Nuhu aliwaita wanyama wote na kisha akaitangaza habari ile ya Paka

Paka kwa upande wao walisononeshwa sana na hilo! Wakajiona WAMEDHALILISHWA na KUUMBULIWA. Hivyo nao wakamuomba MUNGU aliyewaumba kama ifuatavyo: "Eee Mungu sisi viumbe vyako tuliokosa! Wewe ndiye uliyemuumba Nuhu (bwana wetu) hapa duniani na ndiye umemuumba Paka, Mbwa na wengineo. Mbwa katudhalilisha pamoja na kua alichokisema ni kweli, tumekifanya, nasi tunakuomba nae Mbwa umdhalilishe".
Dua/maombi haya ya Paka Mungu aliipokea. Pokea ya Mungu katika hili alivyofanya hivi leo kuwakuta au kuwaona Paka wanajamiana ni shughl pevu!

(mimi Judgement ilinichukua miaka 32 ya uhai wangu ndiyo nikawaona Paka wanajamiana kwa mara ya kwanza, tena ilikua sa8 za usiku) Mbwa Mungu akawapa fedheha. Ni jambo la kawaida sana kuwakuta Mbwa sa7 mchana katikati ya soko au katikati ya uwanja wa mnada/gulio wameng'ang'aniana kwenye jimai. Members wenzangu kisa hiki nimekileta jamvi ndani yake kuna subject!

Hata leo ukimuumbua rafikio, nduguyo, jiranio, jamaa yako kwa dhambi aliyoitenda kweli akikulalamikia kwa muumba uwezekano wa kuitikiwa ni mkubwa.

Chao!
 
sasa sijaelewa....mbona hakuna mahali paka alipoumbuka.....?..coz mambo yake anafanyia sirini....shem hebu dadavua hapa.....
 
sasa sijaelewa....mbona hakuna mahali paka alipoumbuka.....?..coz mambo yake anafanyia sirini....shem hebu dadavua hapa.....

Shem Preta asante kunistua! Hakika nilichanganya marumba!
Nishaifanyia sredi marekebisho.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom