Kuuliza sio ujinga, almond zinalimwa sehemu gani nchini?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,385
2,000
Almond zile kitu zinauzwa kwenye masoko makubwa (super markets).
huwa zinalimwa wapi bongo.

picha.
1112643
 

kiraremapojoni

JF-Expert Member
Nov 30, 2018
390
1,000
Kazi zake?
Lozi (Almond):

Lozi inajulikana kama ni King katika jamii ya njugu, ina elements karibia ya zote zinazohitajika katika mwili wa mwanadam. Ni chakula chenye kutia nishati mwili na akili.
Kuna aina mbili za Lozi, kuna lozi zile tamu na kuna lozi chungu kuna zenye ngozi nyembamba (thin-skinned) na kuna zenye ngozi nene(thick-skinned) hii ni katika aina ya lozi tamu ambazo ndio tunazozitumia na tunahitajika kutumia ama zile lozi chungu zina prussic acid ambayo ni sumu hata hivo hizo lozi chungu zinatumika katika mambo ya kutengenezea cosmetics, mafuta ya lozi (almond oil) pia na perfumes.

Nchi mashuhuri yenye Lozi ni Morocco, pia lozi zilionekana katika miaka mingi nyuma katika nchi ya Syria na Palastine inasemekana katika zama za Nabii Issa A.S. Hata hivo sasa hivi lozi zinazalishwa sehemu nyingi duniani kama Italy,California,Australia,South Africa,Kashmir na sehemu nyingi za Asia.

Food Value: Minerals and Vitamins
Moisture 5.2% Calcium 230 mg
Protein 20.8% Phosphorus 490 mg
Fat 58.9% Iron 4.5 mg
Minerals 2.9% Niacin 4.4 mg
Fibre 1.7%
Carbohydrates 10.5%

Ndani ya lozi pia kuna upatikanaji wa copper, iron phosphorus na Vitamin B, vitu hivi vinasaidia katika upatikanaji wa new blood cells, haemoglobin pia inasaidia ubongo, mishipa, mifupa, moyo na ini kufanya kazi kwa wepesi kabisa. Lozi insaidia kupanua na kutia nguvu muscles za ubongo katika kuongeza fahamu.

Old ages:Utu uzima wa kiumri.
Chukua lozi kiasi na uziroweka katika maji na baadae utoe ngozi yake ikisha uzisage na kufanya paste kwa kutumia kama siagi, hii huongeza proteins ndani ya mwili na hasa kwa watu wazima, pia unaweza kutia katika maziwa na ukanywa hii nzuri kwa watoto.

Anaemia: upungufu wa damu
Kuna upatikanaji wa copper katika lozi katika rate 1.15mg per 100 grams, copper pamoja na iron na vitamins hizi zinatumika kama ni catalyst katika mfumo wa blood haemoglobin. Kwa hiyo wenye maradhi ya upungufu wa damu ni vizuri mtu kutumia lozi kwa sana.

Constipation:kupata choo
Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, ni uzuri kula lozi wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala.

Impotency:upunguvu wa nguvu za kiume
Kwa wale wenye upunguvu wa nguvu za kiume na za kike, wale lozi kwa wingi.

Skin Disorder:maradhi ya ukoma
Kwa wale wenye maradhi ya ukoma, wasage lozi iwe laini ikisha wajipake pale palipoathirika, na pia kwa wale wenye pimples.

SOURCE:https://www.jamiiforums.com/threads/faida-za-lozi-almond.183022/
 

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,242
2,000
Mkuu kiraremapojoni amejaribu kujibu.Almond kwa lugha isio rasmi mbeya zinaitwa KWEME hizi ni jamii ya Karanga pori, mbeya huliwa zaidi na watoto.Mmea huu asili yake ni Afrika mashariki na Zimbabwe.Ni mmea wa kitropiki hivyo unaweza ota mahala pengi Afrika.Mmea huu haujafanyiwa tafiti za kutosha duniani na hasa Tanzania, zaidi unatumika kiasili tu.
Kweme hapa Tanzania zinapatikana highland areas kama Kilimanjaro na Tukuyu Mbeya milimani huko zimejiotea tu! Sehemu mahususi ni maeneo ya Upare na safu za mlima Rungwe na lake Ngosi.
Kwa utafiti wangu hakuna Shamba kubwa linalojulikana hapa Tz kwa sababu kweme sio maarufu sana hasa low land areas.
Binafsi nipo katika utafit nataka nizopande Njombe nimetafuta mbegu lakini bei sio njema moja Sh.200.Nimenunua mbegu chache nijaribu nione matokeo.
Kweme zinaanza kuzaa baada ya miaka miwili na huishi hadi miaka 30, Huota kwa kutambaa kwenye mti mwingine na kufikia urefu wa mita 30.
Ukitaka mbegu halisi tembelea upare au tukuyu mwakaleli msimu wake in kuanzia mwezi wa 12 lakini huwa hazipotei kabisa mtini.Karibu kwa maswli.
Nadhani umechanganya mafile kweme na lozi ni Vitu viwili tofauti,
kwanza Kweme ni kubwa na rangi ya khaki,
Ila lozi ni ndogo rangi ya brown

pili kweme inatambaa kama Pasheni Ila lozi Ipo kwenye Mti kama wa tundaDamu(matundanyanya)

tatu gamba La kweme ni gumu kupasua Ila gamba La lozi linapasuka baada ya lozi kukomaa..
 

vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,510
2,000
Nadhani umechanganya mafile kweme na lozi ni Vitu viwili tofauti,
kwanza Kweme ni kubwa na rangi ya khaki,
Ila lozi ni ndogo rangi ya brown

pili kweme inatambaa kama Pasheni Ila lozi Ipo kwenye Mti kama wa tundaDamu(matundanyanya)

tatu gamba La kweme ni gumu kupasua Ila gamba La lozi linapasuka baada ya lozi kukomaa..

Lozi? Kweme? Seseme?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom