Kuugua kwa Prof. Mwandosya, Dk. Mwakyembe pigo Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuugua kwa Prof. Mwandosya, Dk. Mwakyembe pigo Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 3, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya


  Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wamesema kuugua kwa muda mrefu Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kumeutikisa mkoa huu kutokana na viongozi hao kuwa tegemeo katika harakati za kuletea maendeleo ya mkoa na kupiga vita ufisadi.

  Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti jana baada kufuatilia vyombo vya habari hali ya Dk. Mwakyembe na jinsi aliyobadilika ngozi yake, walisema kuugua kwa viongozi hao waandamizi kumekuwa ni pigo kubwa kwa mkoa wa Mbeya kwasababu walikuwa ni tegemeo kubwa.

  Mkazi wa Tukuyu mjini, John Mwakifuna, alisema Profesa Mwandosya, alikuwa tegemeo kubwa kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

  Mwakifuna alisema wananchi wa Mkoa wa Mbeya na mikoa ya kanda hiyo wataendelea kumuombea ili apone haraka na kuendelea na majukumu yake.

  Patrick Mwakanosya, mkazi wa Mbeya mjini, alisema Dk. Mwakyembe na Profesa Mwandosya, wanategemewa sana katika masuala ya kisiasa ambapo wamekuwa ni kiunganishi kikubwa kati ya wabunge, viongozi na wanachama.

  “Siasa za Mbeya ni za makundi makundi lakini viongozi hawa wanasikika sana na wanapobaini kuna jambo fulani linalalamikiwa na kuhatarisha kukiyumbisha chama wanaingilia kati kulisuluhisha,” alisema Mwakanosya.

  Mkazi wa Kyela, Emmanuel Mwakalukwa, alisema kimsingi kuugua kwa viongozi hao imekuwa pigo kwa Mkoa wa Mbeya ambao sasa umebaki na simanzi kwa kukosa watu makini ambao wanaweza kujenga hoja nzito kitaifa.

  Hivi karibuni wakati akifunga kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa Mbeya, kilichofanyika Desemba, mwaka jana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, aliwaomba wananchi wa mkoa huu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwaombea viongozi hao ili wapone haraka.

  Hata hivyo, Profesa Mwandosya ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki, alirejea nchini Desemba Mosi, mwaka jana kutoka nchini India alikokuwa akipata matibabu na baadaye tena amekwenda India kwa matibabu.
  Kwa upande wa Dk. Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela, aliondoka nchini Oktoba 9, mwaka jana kwenda India na alirejea nchini na hali yake inaendelea vizuri.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,122
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  naungana na wewe,
  kwa kweli ni pigo kwa wana mbeya,
  hawa ndugu ni wasomi waliobobea,
  looh, kweli kama ni MUNGU ashukuriwe,
  na kama ni mwanadamu alaaniwe milele na milele.
   
Loading...