Kuuelewa mfumo wa Utawala wa Kifisadi - 101

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
KUUELEWA MFUMO WA UTAWALA WA KIFISADI - 101
Na. M. M. Mwanakijiji

Maadui wa Tanzania siyo Rostam, Lowassa, Chenge, Mramba, Yona au mtu yeyote ambaye ameonakana na kutajwa kuwa ni fisadi au kuhusishwa na kashfa za kifisadi. Hawa wote na wengine wengi ambao nimewabatiza majina ya “makuwadi wa ufisadi” na “vikaragosi vya ufisadi” ni matokeo tu ya yule adui yetu namba moja ambaye bila ya kumshughulikia basi juhudi zote za kupigana na “ufisadi” zitakuwa ni kama juhudi za anayezama majini huku kwa hasira akiyapiga ngumi maji hayo ili “kuyakomoa”. Ni zoezi lisilo na tija.

Anayepigana vita dhidi ya ufisadi (awe ndani ya CCM au nje yake) akifikiria kuwa anapigana dhidi ya watu “fulani” basi hajajua uzito wa vita hii iliyo mbele yetu; vita ambayo hatukuitafuta bali tumejikuta tunalazimika kuipigana kwani imeletwa kwetu bila kumchokoza mtu na haitaondoka isipokuwa kwa kuishinda tu.

Tukijifunza katika vita ya Kagera tunaweza kuona kuwa lingekuwa kosa kubwa sana kwa wapiganaji wetu kuwaadhibu wanajeshi wa UPDF (Jeshi la Wananchi wa Uganda) tukifikiria kuwa wao ndio walikuwa adui zetu. Tunaelewa kwamba wanajeshi wale walikuwa wanatekeleza amri ya vita toka kwa amiri Jeshi Mkuu wao wa wakati ule Idi Amin Dada. Sasa kama tungepigana ili kushinda wapiganaji wa Uganda kwenye jukwaa la vita halafu basi tungechekwa na jumuiya ya kimataifa kwa kutokuelewa tulipigana dhidi ya nani hasa.

Adui yetu wakati ule ulikuwa ni utawala wa Nduli Idi Amin na mfumo zima wa utawala wake uliosababisha sisi twende vitani licha ya juhudi zote za kuepuka vita kuchukuliwa na kushindikana. Ndio sababu wakati wa tangazo la vita kwa Taifa letu Baba wa Taifa aliweka lengo lililokuwa wazi kabisa, kuyarudisha majeshi ya Amin toka ardhi yetu (kama kuwarudisha nyuma makuwadi wa ufisadi), kumkata makali Amin kabisa asiweze kuthubutu kutuvamia na kuwa tishio kwetu tena.
 
Attachments

  • KUUELEWA MFUMO WA UTAWALA WA KIFISADI 101.doc
    72 KB · Views: 244
Naona umeingia kwa gia kubwa, hii project-X inabidi iwe na wapambe/wafuasi wengi kama ilivyokuwa kwa Tsvangirai kule Zimbwabwe.
 
Ndugu zangu, adui nambari moja wa maendeleo na mafanikio ya Watanzania ni mfumo haramu uliotengenezwa wa utawala wa kifisadi. Ni lazima kwa mpiganaji yoyote kuelewa mfumo huu unavyofanya kazi kwani wale wote tunaowaita mafisadi leo hii ni matokeo ya mfumo huu wa kiutawala; mfumo ambao ni mchanganyiko wa mifumo midogo midogo ya kisiasa, kiuchumi, na kisheria ambayo msingi wake ni ubinafsi, kutokuwajibika, kulindana, utawala wa hofu, kubebana na kuvumiliana kwa kadiri ya kwamba wanufaikaji ni kikundi cha watu wachache walio katika utawala na wale wanaohusiana nao kwa karibu.
.

hapa sawasawa mzazi!
 
Kupambana na mfumo ni kazi ambayo tumekuwa tunaikwepa kila siku, lakini huko ndiko kwenye kiini cha matatizo yetu mengi
 
Mfumo wetu wa kisheria katika utawala wa kifisadi umeundwa ili kuondoa hasira na siyo kushughulikia tatizo lenyewe hasa linalosumbua jamii.
very yes,
nilipojaribu kuclarify kwa mifano mtandao ukawa busy,anyways tufanye hivi:
1-
2-
3-
4-
 
Naona umeingia kwa gia kubwa, hii project-X inabidi iwe na wapambe/wafuasi wengi kama ilivyokuwa kwa Tsvangirai kule Zimbwabwe.

never before in Tanzania's political history has something like this ever attempted...
 
Moja ya makosa ya hivyo vita ni kwamba, Nyerere alishindwa kupigana na UFISADI uliokuwepo ndani ya chama chake. Kama aliweza kupigana na Amini, kwanini alishindwa kupigana na MAFISADI ndani ya Serikali yake? Uganda wanamaendeleo sasa hivi kuliko sisi; sasa kwanini Nyerere alishindwa kuweka mising imara ya kupigana na huo Ufisadi ndani ya TZ? au alishindwa hivyo vita?
 
Mafisadi wakati wa Nyerere ni akina nani hao?..
 
Ukosefu wa elimu pia ni nyenzo kubwa ambayo inatumiwa na huo mtandao wa mafisadi. Ni rahisi kudili na mtu mmoja mmoja hasa pale inapoonekana huyo mmoja anafikiria, lakini kama jamii ya watanzania angalau nusu tungekuwa na elimu inayo tusaidia kufikiria, hawa mafisadi wanaolindwa na mfumo mzima wa sheria, mfumo wa kisiasa, viongozi (vibaraka) ndani ya huu mfumo wangekuwa wanajifikiria mara mbili mbili kabla ya kufanya ufisadi.

Inafurahisha kwamba, tumeanza kufikiria.
 
Tusipobadilisha mfumo wa kiutawala wa ufisadi tutaendelea kuzalisha mafisadi tu. Haijalishi ni chama gani kiko madarakani.

Mkuu MMM,
Kama kawaida heshima mbele. Ni kiri kwamba wewe ni Mwalimu. Kama ni somo umelitoa na limeeleweka sana.
Nimeguswa sana na hii makala or call it Project X.
Kweli kabisa ni mfumo ndio tatizo.

Mfumo wa kisheria kama ulivyoelezea hapa:

Mfumo wetu wa kisheria katika utawala wa kifisadi umeundwa ili kuondoa hasira na siyo kushughulikia tatizo lenyewe hasa linalosumbua jamii. Kwa kiasi kikubwa utaona kuwa sheria mbalimbali zimeundwa zikiwa na majina mazuri na ya kupendeza lakini zikiangaliwa kwa karibu utaona kuwa zimeundwa ili kuwafanya watu wasikasirike sana.

Ina umiza na kukasirisha sana. Nikiangalia kesi nyingi zilizo mahakamani utakuta kwamba zipo tu kupunguza hasira za jamii. Mfano mzuri ni kesi ya akina zombe imechukua miaka ili kupunguza hasira. Kesi ya akina Nalaila Kiula nayo vivyo hivyo. Njoo hii ya mramba na kina yona the same thing. Hivyo tatizo ni mfumo. Mfumo mzima. Totally agree with you.
 
Mafisadi wakati wa Nyerere ni akina nani hao?..

Waswahili wanasema "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo". Utawala mzima wa Nyerere ulijaa mafisadi. Utawala wa kibabe wa Nyerere ndiyo matunda tuliyokuwa nayo sasa hivi. CCM wameweza kuchukua kila nyezo alizokuwa anatumia Nyerere kukaa madarakani milele. Angalia in USA, George Washington, alikataa kukaa madarakani milele; sasa kwanini Nyerere alishindwa kuweka misingi kama hiyo? Aliamua kukaa madarakani ili kuweza kutawala nchi kibabe bila ya uchaguzi wenye haki, freedom nk. Ufisadi uliokuwepo sasa hivi ni mizizi ilyopandwa na utawala wa Nyerere. Kwa hiyo, Nyerere na utawala wake ndiyo walionzisha utamaduni wa UFISADI. Tungekuwa na foundation nzuri tusingekuwa hapa tulipo.
 
Ukosefu wa elimu pia ni nyenzo kubwa ambayo inatumiwa na huo mtandao wa mafisadi. Ni rahisi kudili na mtu mmoja mmoja hasa pale inapoonekana huyo mmoja anafikiria, lakini kama jamii ya watanzania angalau nusu tungekuwa na elimu inayo tusaidia kufikiria, hawa mafisadi wanaolindwa na mfumo mzima wa sheria, mfumo wa kisiasa, viongozi (vibaraka) ndani ya huu mfumo wangekuwa wanajifikiria mara mbili mbili kabla ya kufanya ufisadi.

Inafurahisha kwamba, tumeanza kufikiria.

Pejohny,

Kwanza karibu sana JF.

Hapo nilipohighlight, kabisa ndo nyenzo muhimu sana ambayo mfumo huu wa kifisadi hujiimarisha bila ya kuagushwa!

Hebu angalia kwa mfano kny chaguzi ndogo za hivi karibuni, watu wa mjini wameonekana kuwa na uelewa mkubwa sana hali ya kisiasa tz na kuamua kukataa kwa vitendo kudhulumiwa haki zao kuliko wale wenzao wa vijijini ambao elimu hata ya uraia kwao ni tatizo kubwa!

Elimu ni muhimu sana kwa Tanzania tunayoipigania iwe huru kutoka kny mfumo wa kifedhuli na kifisadi unaoongozwa na sisiemu!
 
Natamani hii mada ingeunganishwa na ile ya "wapambanaji wa ufisadi....."
 
maneno mengi hayavunji mfupa,ngoja ngoja huumi zatumbo-TUCHUKUE HATUA TUONDOE WAKOLONI CCM.slow but sure,aliye juu mngoje chini,no hurry in africa-MANENO MBOFU MBOFU.
Mimi nasema:-
''Mvumilivu hula mbivu.....ila mvundika mbivu hula mbovu''
Tusipo thubutu sisi kizazi gani kitathubutu,tuseme no inatosha kwa ccm
 
Moja ya makosa ya hivyo vita ni kwamba, Nyerere alishindwa kupigana na UFISADI uliokuwepo ndani ya chama chake. Kama aliweza kupigana na Amini, kwanini alishindwa kupigana na MAFISADI ndani ya Serikali yake? Uganda wanamaendeleo sasa hivi kuliko sisi; sasa kwanini Nyerere alishindwa kuweka mising imara ya kupigana na huo Ufisadi ndani ya TZ? au alishindwa hivyo vita?

Ndugu hapa siyo, hayo maendeleo waliyonayo Uganda kuliko TZ ni yapi jamani au unaongea tu na Uganda hujafika!!!!
 
Waswahili wanasema "Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo". Utawala mzima wa Nyerere ulijaa mafisadi. Utawala wa kibabe wa Nyerere ndiyo matunda tuliyokuwa nayo sasa hivi. CCM wameweza kuchukua kila nyezo alizokuwa anatumia Nyerere kukaa madarakani milele. Angalia in USA, George Washington, alikataa kukaa madarakani milele; sasa kwanini Nyerere alishindwa kuweka misingi kama hiyo? Aliamua kukaa madarakani ili kuweza kutawala nchi kibabe bila ya uchaguzi wenye haki, freedom nk. Ufisadi uliokuwepo sasa hivi ni mizizi ilyopandwa na utawala wa Nyerere. Kwa hiyo, Nyerere na utawala wake ndiyo walionzisha utamaduni wa UFISADI. Tungekuwa na foundation nzuri tusingekuwa hapa tulipo.

Ukiacha Botswana, Namibia na SA, hebu nipe mifano angalau nchi unayofikiria wamefanya makubwa ktk kipindi sawa alichotawala nyerere ktk southern sahara.
 
Mwanakijiji huwezi kuutengenisha mfumo na wanaoendesha mfumo huo. Ukitaka kumuua nyoka unamponda kichwa. Au hatujui kichwa cha mfumo huo ni nani/nini?
 
Mwanakijiji huwezi kuutengenisha mfumo na wanaoendesha mfumo huo. Ukitaka kumuua nyoka unamponda kichwa. Au hatujui kichwa cha mfumo huo ni nani/nini?

Well said! Ondoa CCM madarakani and hopefully that will lead the way for other changes. I'm sick of them.
 
Mwanakijiji unakumbuka lile swali la Mwalimu linalosema 'Serikali ni nani?' Sasa hapo badilisha neno 'Serikali' weka neno 'Mfumo'.

Mfumo ni nani?

Ukilijibu hilo swali basi utagundua kuwa huwezi kubadili 'mfumo' bila kuwabadilisha hao kina 'nani'!
 
Back
Top Bottom