Kuuelewa mfumo wa Utawala wa Kifisadi - 101

KUUELEWA MFUMO WA UTAWALA WA KIFISADI - 101
Na. M. M. Mwanakijiji

Maadui wa Tanzania siyo Rostam, Lowassa, Chenge, Mramba, Yona au mtu yeyote ambaye ameonakana na kutajwa kuwa ni fisadi au kuhusishwa na kashfa za kifisadi. Hawa wote na wengine wengi ambao nimewabatiza majina ya “makuwadi wa ufisadi” na “vikaragosi vya ufisadi” ni matokeo tu ya yule adui yetu namba moja ambaye bila ya kumshughulikia basi juhudi zote za kupigana na “ufisadi” zitakuwa ni kama juhudi za anayezama majini huku kwa hasira akiyapiga ngumi maji hayo ili “kuyakomoa”. Ni zoezi lisilo na tija.

Anayepigana vita dhidi ya ufisadi (awe ndani ya CCM au nje yake) akifikiria kuwa anapigana dhidi ya watu “fulani” basi hajajua uzito wa vita hii iliyo mbele yetu; vita ambayo hatukuitafuta bali tumejikuta tunalazimika kuipigana kwani imeletwa kwetu bila kumchokoza mtu na haitaondoka isipokuwa kwa kuishinda tu.

Tukijifunza katika vita ya Kagera tunaweza kuona kuwa lingekuwa kosa kubwa sana kwa wapiganaji wetu kuwaadhibu wanajeshi wa UPDF (Jeshi la Wananchi wa Uganda) tukifikiria kuwa wao ndio walikuwa adui zetu. Tunaelewa kwamba wanajeshi wale walikuwa wanatekeleza amri ya vita toka kwa amiri Jeshi Mkuu wao wa wakati ule Idi Amin Dada. Sasa kama tungepigana ili kushinda wapiganaji wa Uganda kwenye jukwaa la vita halafu basi tungechekwa na jumuiya ya kimataifa kwa kutokuelewa tulipigana dhidi ya nani hasa.

Adui yetu wakati ule ulikuwa ni utawala wa Nduli Idi Amin na mfumo zima wa utawala wake uliosababisha sisi twende vitani licha ya juhudi zote za kuepuka vita kuchukuliwa na kushindikana. Ndio sababu wakati wa tangazo la vita kwa Taifa letu Baba wa Taifa aliweka lengo lililokuwa wazi kabisa, kuyarudisha majeshi ya Amin toka ardhi yetu (kama kuwarudisha nyuma makuwadi wa ufisadi), kumkata makali Amin kabisa asiweze kuthubutu kutuvamia na kuwa tishio kwetu tena.

Mwanakijiji

Umesema kweli. Hoja kama hii niliisikia kwa mara ya kwanza kwenye hotuba ya Freeman Mbowe akifungua mkutano mkuu wa CHADEMA. Unayo nakala yake uiweke hapa?

Lazima tubadili mfumo wa utawala!

serayamajimbo
 
Mwanakijiji umenena na nakubaliana kimsingi na nadharia yako. Hata hivyo vita havina macho na katika vita hususan vya umma kila silaha ndogo na nzito hutumika...na adui hachaguliwi pa kupigwa... mwenye uwezo wa kupiga kidole hufanya hivyo..na mwenye uwezo wa kulenga moyo pia hufanya hivyo, na wote wakiwa na lengo moja tu la kumwangamiza adui. Mafisadi na Mawakala wao lazima washughulikiwe sanjari na taratibu za kumaliza huo mfumo wa kifisadi ambao unahitaji muda na jitihada kubwa zaidi. Tukumbuke kuwa si watu wengi wanaofahamu kuwa kiini cha ufisadi nchini ni mfumo wa kisiasa, kiuchumi na kisheria uliopo, lakini wanawafahamu wanaonufaika na ufisadi.
 
siku tutakapokubali na kuelewa kuwa Ufisadi ni matokeo ya mfumo mbaya na si mtu mmoja mmoja au sura, siku hiyo itakuwa ni ya kwanza ya ushindi dhidi ya Ufisadi.
 
siku tutakapokubali na kuelewa kuwa Ufisadi ni matokeo ya mfumo mbaya na si mtu mmoja mmoja au sura, siku hiyo itakuwa ni ya kwanza ya ushindi dhidi ya Ufisadi.

Asante.

System haina checks and balances, inavuja kila sehemu na ndio maana ufisadi unawezekana.
 
Back
Top Bottom