Kuuaga umasikini........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuuaga umasikini........

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by WomanOfSubstance, Oct 31, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kuuaga umaskini Tanzania, ni kazi kweli kweli.Fikiria haya yafuatayo:
  • Asilimia 50% ya idadi ya watu Tanzania ni wale wenye umri chini ya miaka 18.Hii inaashiria fertility rate kubwa sana. Asilimia 49% wakiwa kati ya miaka 15-64 ambao ni umri wa kuzalisha. Hii ina maana kuwa nusu ya watanzania bado hawako katika nafasi ya kuchangia ukuaji wa pato la taifa na hatimaye kuuondosha umaskini.Cha kusikitisha zaidi ni kuwa, katika kila watu 100 walio katika kundi la kuweza kuzalisha, ujue kuna watu 104 ambao ni tegemezi.Just think about the age dependency ratio here in relation to growth and poverty reduction.
  • Robo ya households, zinaongozwa na wanawake ambao inasemekana ni maskini zaidi ukilinganisha na wanaume.
  • Asilimia, 3% ya watoto chini ya miaka 18 wamepoteza mzazi mmoja, ambapo asilimia moja ya wale chini ya miaka 18 wamepoteza wazazi wote.Hii inaonyesha kiwango cha uyatima na mzigo wa kulea watoto yatima.
  • Ni asilimia 11% tu ya household Tanzania zenye umeme, Mijini ni aslimia 38 tu ndio wana umeme
  • Asilimia 80 ya household bado wanatumia vyoo vya shimo ( pit latrines).Ni asilimia 3 tu ndio wanatumia vyoo vya kisasa (modern flush toilets) !!
  • Asilimia 30 wanaishi kwenye nyumba ya chumba kimoja cha kulala wakati asilimia 37 wanaishi nyumba ya vyumba viwili vya kulala.
  • 4/10 households za mijini Tanzania bara wanaishi nyumba yenye chumba kimoja tu cha kulala.
  Unaweza kupata takwimu zaidi kutoka TDHS 2004/5 which is the latest.

  kwa mwendo huu, umaskini unapungua?
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hiyo takwimu ndio hali halisi ya watanzania tulio wengi, tunajifariji bongo tambarare lakini bado sana tena sana. Kama tambarare ni kwa watu wachache maana gape la tajiri na masikini ni kubwa mno.

  Ukitaka kujua hali halisi nenda vijijini huko, usiangalie mijini japo kuna sehemu sehemu za mijini nako hakuna umeme, vyoo vya shimo na watu kujazana kulala chumba kimoja.
  Kwa kweli watanzania wenzangu tuna safari kubwaa ya kujitoa katika wimbi hili la umasikini.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  nimeweka hizo takwimu ili kufunua macho tuone kama kweli ni tambarare kama inavyofikiriwa...
  Hizi takwimu ni za hali generally.... vijijini wala usiseme!
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Naomba umalizie datas kwa kuonyesha ni aslimia ngapi ya watanzania hawajui kwa nini wawe kwenye daftari la wapiga kura na hawajui kwa nini wapige kura.
   
 5. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  na hapa wame estimate.....
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Its from very credible and reliable source - Demographic and Health Survey
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nitajitahidi kutafuta...ila na wewe pia chimbua ili utuletee hapa
   
 8. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa data, tukiacha na households dependent hivi daladala moja inawategemaezi wangi (wapiga dede, koda deleva, mwenye gari, watoto wake, ndugu zake, trafic, TRA, etc) ni mfano tu kuonyesha utegemezi ulivyo mkubwa Tanzania na mwingi si walazima. kama serikali hataweka mikakati dhabiti basi umasikini ni halali yetu.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Vera, homework on a weekend, nisaidie nijue kwani wewe nakuaminia sana. Tukipata hizo data tutajua matatizo yetu Watanzania.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ngambo Nguli,

  Nimeipenda signature yako maana inaelezea hali halisi ya watanzania na mustakabali wao.

  Hivi lakini, tukiangalia hizi takwimu chache hatuoni kuwa umaskini mwingi pia ni wa kujitakia? Fikiria kwanini fertility rate iwe juu wakati uwezo ni mdogo, na huduma za uzazi wa mpango zinajulikana na kupatikana?

  Inakuwaje watu tunashindwa kuboresha mazingira yetu tunamoishi ilhali tuko tayari kuchangia mapesa mengi kwa vitu visivyo endelevu kama harusi, kitchen party n.k.?

  Katika ngazi ya juu zaidi, umeme umekuwa ni ishu, maji, huduma za jamii.... kama mipangilio ingekuwa mizuri na kama mianya ya rushwa ingezibwa, basi huenda hali ingekuwa bora zaidi.

  Kufuatana na Afrobarommeter surveys za mataifa 11 barani Africa, Watanzania wanaonyesha kuwa na hasira sana na kiwango cha chini cha uchumi wao, wakionyesha kuunga mkono mageuzi ya kiuchumi.Pamoja na hali hii bado watanzania wameonyesha kuwa the "most uncritical citizens" with a habit of accomodation.Wanavumilia sana kuona hali ni mbaya tu.Althought Tanzania is a highly politicized society, it is not a highly organised one.Watanzania wako tayari kuendelea kuvuta subira katika kungojea matokeo ya mageuzi ya kiuchumi.

  Kwa maneno mengine watanzania wengi hawako tayari kujifanyia juhudi kujiletea maboresho katika maisha yao.
  Tofauti na nchi nyingine barani Afrika, watanzania ndio pekee utakuta kote mijini na vijijini wakijikuta kukosa huduma muhimu kama vile maji, huduma za afya,na hata elimu kwa karibu kiwango kilekile.

  Tofauti iliyopo ni katika upatikanaji wa umeme tu ambapo mijini ndiko kuna umeme.

  Ukiangali per capita income, Tanzania inakaribiana na Malawi kwa viwango vya chini ambapo Tanzania ni $696 wakati MALAWI ni $773.Linganisha na Botswana $5611, Namibia $4052, South Africa $ 4234.( hizi ni Takwimu za 1999)
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Unaposema watanzania hawajui kwanini wawe wenye PNVR ( DAFTARI KA WAPIGA KURA - PERMANENT NATIONAL VOTERS REGISTER)...au hawajui kwanini wapinge kura sijui kama zipo takwimu za kuunga mkono hoja hii.
  Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa watu waliokwisha jiandikisha kupiga kura kwa uchaguzi wa 2010 wameongezeka hadi kufikia watu milioni 18,014,667 ukilinganisha na 15,935,493 waliojiandihikisha kwa uchaguzi wa 2005.
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  You make my day!..taxi inawategemezi chungu nzima..day worker, (day and night), Driver, mwenye mali, tra, watoto wao etc..hii kitu inapunguza sana moyo wa kufanya kazi kwenye informal sector...chain ya walaji ni wengi utafikiri mchwa..kitu kimoja..wapi maendeleo
   
 13. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  • Hiyo asilimia ya yatima ni negligible compared to the entire "nguvu kazi" population(15-64 ni 49%)
  • Large population ya China inatumika kama internal market nzuri sana(ndio maana kampuni nyingi za west zinatafuta market China),cheap labor safi,and bcoz of that kila mmoja ana compete katika sector yake aweze kuondokana na hali aliyonayo.
  • Despite umaskini na relatively low per capita ya China na India,jamaa wanakuja juu;almost kila PC 3 zilizopo duniani 1 ni made in China,sasa hivi made in US inakuwa replaced by made in China(tutalalamika sana ooh,jamaa vitu vyao fake mara vile,but you can't stop them).
  • Mzee wa kijijini China anapakia pipa la uchafu kwenye baiskeli,anachokifanya ni kuunganisha mota kweye free wheel(hub) ya baiskeli yake,,,hii pia tunashindwa?
  • Soma hapa India's toilet king(http://development.asia/issue04/field.asp), halafu zingatia idadi ya wasomi wetu katika field hiyo.

  DIT,MOSHI TECH,UDSM etc haziwezi kutoa product walau inayoweza kuwaza kama huyu kijana?
  • Bonde la mto Rufiji laweza toa mpunga wa kulisha east africa yote,tuna mabonde mangapi kama yale....,SUA has nothing to do on this?wanaweza ku train panya wa kutegua mabomu,vipi washindwe issue kama hizi?Bora shangingi za milion 40 kwa kila mbunge,mkuu wa wilaya...,more expensive as you go up in status kuliko tractors na zana zingine za kilimo(keep in mind kuwa 70% ni wakulima).
  • Kuna nchi duniani kwa kiasi kikubwa zinategemea bandari katika uchumi wao,tuna bandari zisizopungua 4...(Dar may be more than 3,Zenji,Tanga,Mtwara).
  • Maliasili chungumbovu,tofauti na nchi kama China inayo rejuvinate desert into productive land,Netherland....bahari into productive land etc,sisi dah,,,hadi hasira.madini pekee yake yangepunguza angalau 50% ya matatizo uliyoyaeleza hapo juu.
  • Pia kuna matatizo binafsi ya mtu;tunajiona watoto always,sijui ulimaanisha nini uliposema chini ya miaka 18 na yatima,ninachojua mtu ukishafikia puberty tu uyatima unakuondoka na unatakiwa ujiandae na responsibilities za maisha...miaka 18 ni mtu mzima,hii hali ndio inatufanya tuchelewe kwenda shule may be,hadi mtu wafika miaka 20-25 bado ni tegemezi,na unaona ni haki yako kuhudumiwa.
  • Kila kitu chaanza from the scratch,tu develop innovative ideas,tupige kazi,tuone tunaweza wapi na tunashindwa wapi.Tuwe friendly kama wanajamii wenye lengo moja,kama una elimu basi implement na jaribu kushare na wasio nayo practically,kule vijijini wanahitaji msaada wa utaalam wa kilimo kutoka SUA and the like,kadhalika fani zingine.
  • Tuna produce kidogo tunatumia sana badala ya kusave ili uweze kutumia kama capital ya kutatua matatizo yetu.Mimi sio mchaga ila nafigilia sana hawa Mangi aisee,akija Dar hata kwenye kibanda cha mkaa atalala,ila baada ya muda utaona outcome.{By the way natafuta mchumba(a beautiful girl with good morals) mchaga au mpare}.
  Peace
  Qadhi
   
 14. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135

  Hapo nilipokoleza rangi kwa kifupi si kweli kwamba vyuo vyetu vimeshindwa kutoa watu wenye taaluma ambao wanaweza kuwaza na kufanya mambo makubwa na yakaonekana binafsi naona policy za nchi yetu hazijalenga kuwasaidia vijana wengi ili kuweza kutumia taluma zao na matunda yakaonekana.
  Nitoe labda mfano mmoja ambao naukumbuka wakati Mkapa akiwa bado madarakani alienda Botswana akapata fursa ya kutembezwa kwenye shamba la mifuko akawaona ng'ombe na wanavutia kuliko wale tunaochunga badala ya kufuga TZ ilimbidi ahoji kwamba wamefanya nini hadi wakafikia mafanikio hayo alishangaa kuambiwa kuwa ni vijana wako waliomaliza VET SUA ndo wanaoweza kujibu hili swali.
  Kuna haja ya kujiangalia zaidi kwanini watanzania wengi hatupo productive kwa nchi yetu achilia mbali mafisadi n.k Hapa utaona kwa jinsi gani nchi yetu ilivyo na allergy na wataalamu wake.
  Na tufanye nini ili tuweze ku import raw materials na ku export manufactured goods tofauti na kinyume tunavyofanya sasa?
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Vera asante kwa data, kama hizo data ni hivyo kwa nini aslimia 88.4 waendelee kupenda kuongozwa na watu ambao ndio chanzo cha umaskini wao siku nenda rudi, jamani hatuoni kuwa kuna problem kubwa sana hapa. Tukichambua hiyo idadi ya wapiga kura 18,000,000 halafu kuchukue kwa kila jimbola uchaguzi kwa mfano mbeya vijijini, busanda na biharamulo utaona kuwa kuna shida hapa ila tu watu hawajafanya postmortem vizuri.Watu hawashindwi kuchangia, wakichanga michango inaenda mikononi mwa wachache ambao hawatamaliza tatizo so wananchi wanaona mchango mzuri ni wa harusi ambapo wanaona hela zao zinavyotumika. ( Sina maana kwamba nakubaliana na kuchanga millions to be spent in hours) Lakini huu ndio ukweli wa watanzania.Increase in fertility rate inatokana na ukweli kuwa kutokana na low poverty level za majority ya wananchi wa Tanzania, (wengi wao wakiwa vijijini). Mwananchi anaamka asubuhi anatembea 5 km kwenda shamba anatumia jembe la mkono mpaka saa tano, anarudi nyumbani lishe duni Mtu kama huyo Starehe yake ni pombe na zinaa, sehemu ambayo hakuna umeme saa mbili usiku kila mtu kajifungia chumbani, the rest is known, It is a vicious circle sort of.Labda tujiulize what should be done, to alleviate these problems.
   
 16. Kivuko

  Kivuko Member

  #16
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  If you ever do a one to one with one of our "top leaders",you would understand why we are poor.We are being lead by people who have no idea about leadership.they are bosses,waheshimiwa,wazee,etc..,

  To them solving people's problems is more of a bug,a trouble seeking process,that is not beneficial political wise.

  if a i give a person $100 everyday for doing nothing,it will be very hard for that person to work for $50 a week.

  That is the situation with our leaders,they are given bonus years in power,lots of cheers,lots of praises from the west and here in the country for doing almost nothing.How do we expect them to work their buts off for Nothing?only more pressure to perform and calls for more to be done?

  How do we expect them to work diligently to develop our country?while they could do nothing and be awarded billions from mischievous deals and corruptible practices?

  We should stop rewarding them when they don't do anything,and punish them when they underachieve.and that is best done through the ballot box.

  For those with less education we should do best to empower them,and for those with education,we should be less selfish to share.Just for the greater good.
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  88.4 ...ianikumbusha redio ya watu Clouds FM mhh!
  Nitajitahidi kuchangia hoja zako kama ifuatavyo na huenda wengine wataongezea:
  Kura/kuchagua viongozi
  Kura ni nguvu ya mwananchi kuamua hatma ya uongozi kwa taifa na ni silaha kubwa, ila wananchi hawajui ukubwa wa silaha hii.Kura ikitumiwa vizuri inaweza kuleta mabadiliko to the better kwa maana ya kuwaweka madarakani viongozi makini wenye ari ya kuleta mabadiliko ya kweli.Kura hii hii ikitumiwa vibaya inaweza kulididimiza taifa moja kwa moja.Kinachotokea ni kuchanganya kura nzuri na mbaya ambapo tunapata cocktail ya wawakilishi - wema na wabaya na hawahawa wanakuja kuchanganyika kwenye chungu kimoja.Kwa msingi huu hata pawe na jitihada kubwa namna gani kubadilisha maisha ya wananchi, inakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
  Chukulia chaguzi zote zinazofanyika, haina maana kuwa wanaochaguliwa wote ni wabaya.,La hasha.Baadhi ni wazuri tena waadilifu.Ila wanapomelt kwenye chungu kimoja...matokeo unaweza kufikiria mwenyewe.
  Swali - je mwananchi akishapiga kura yake , what next? Watanzania mara nyingi wakishapiga kura wanajiona wamemaliza kazi.Hawajishughulishi kuwafuatilia wabunge wao na kuwabana mbavu kuhakikisha wanatimiza ahadi walizotoa.Hawajishughulishi kufuatilia shughuli mbalimbali za umma katika ngazi zote kuona je kile serikali ilichoahidi ndicho? NGOs zinajitahidi lakini bado sauti yao ni ndogo.Pia kuna forum mbalimbali ambazo zingeweza kutumika kuwabana viongozi lakini ushiriki wa wananchi bado kabisa - na pia haileti effect kubwa sana pale baadhi ya vikundi au hata forums kama hizi JF na zingine wanapopiga kelele kama tunavyofanya.Hii wakati mwingine inaonekana kama vijikelele vya wakosaji na hupuuzwa.Fikiria hizi kelele zingepigwa na makundi makubwa ya wananchi nadhani effect ingekuwa kubwa na huenda mabadiliko makubwa yangetokea.
  Changamoto - kelele kama hizi ziwashirikishe vipi wananchi wengi zaidi? Sina jibu rahisi.

  2. High fertility rate
  Kama ulivyosema vema, high fertility rate ni kigezo au kiashiria cha umaskini na pia ni matokeo ya umaskini - si unajua tena TAJIRI NA MALI YAKE, MASIKINI NA WATOTO!Huwezi ukawa na rundo la watoto ukategemea uweze kujikwamua na umasikini.Mara nyingi uzazi wa mara nyingi na muda karibukaribu huchukua nguvu, fursa na hata muda wa mzazi hasa mama ambayo angeweza kujishughulisha na uzalishaji au kuongeza kipato.Vile vile kwa sababu ya umaskini, hakuna shughuli za ziada ukiachilia mbali unywaji na kulala ( matokeo ni kuongeza watoto).Ni viscious cycle.Mipango ya kuhamasisha watu wapange idadi ya watoto imekuwepo lakini uitikiaji wake sijui una mashiko kiasi gani.Serikali za nchi mbalimbali kama China na hata India na kwingineko zimewahi kuchukua drastic crude measures kuhakikisha familia zinakuwa na idadi ndogo ya watoto.China ilikuwa na one child policy - na ukizaa zaidi ya mtoto mmojaunawekewa vikwazo hadi uone moto.Swala likwaja, familia zikaanza kushuriki utoaji mimba ili kupata mtoto huyo mmoja wa kiume.Mimba za watoto wa kike zikawa zinatolewa.Huko India hivyo hivyo na hata ukatili kwenye familia kwa wanawake na watoto wa kike uliongezeka kufikia hata kuwaua watoto wa kike kwa njaa ,hawanyonyeshwi, wala kupewa huduma wakiwa wagonjwa!Huko Nigeria waliwahi kuwa na sera ya kila amilia iwe na watoto wanne maximum.Ikawa kwa wanawake kuwa na watoto wanne lakini unakuta mume ana wake zaidi ya mmoja.Mpango ukawa hauma maana yoyote.Hili suala la kupunguza idadi ya watu nalo liko tete.Huko India nako enzi za Indira Gandhi, mpango ukawa lenga wanaume - wanaume hata walifanyiwa vasectomy kwa nguvu ili kuhakikisha idadi ya watoto/watu haiongezeki kiholela.( ukimlenga mama tu , mwanaume atakuwa bado na uwezo kuzalisha! Hivyo target ikawa wanaume na hili lilim cost katika siasa.Nadhani wananchi wanapaswa kutambua kuwa idadi kubwa ya watoto inaongeza adha na mateso na umaskini ili wenyewe wachukue jukumu kujipangia uzazi.Kwamba serikali itaweka umeme kila mahali ili angalau kupunguza adha na shurba za maisha, tusubiri maana kisingizio sasa ni mvua haba, mitambo mibovu, uchumi wa dunia uliodorora nk.Sijui mipango ya umeme wa sola nao iko vipi.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Nov 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kweli mtu unahitaji takwimu ili kujua bongo maisha magumu? Kuna mambo mengine wala hata hayahitaji takwimu. Ni tembea tu ujionee.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ukitembea utaona lakini utajengaje hoja ? anecdotal evidence haina mashiko!
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Sasa wewe linganisha na utofautishe China na Tanzania.A big population can be a market when there is something to market. What is Tanzania marketing as of now? Tanzania tumeua viwanda vyote vilivyokuwepo through privatisation.Viwanda kama bora na urafiki viko wapi? Sasa hivi tumebaki kuwa a trading economy - watu wanaenda huko huko China na Hongkong, Marekani na Uingereza kuleta bidhaa hafifu kuuza. Ukienda bandari au hata AIRPORT JNIA utakachoshuhudia ni uingizwaji wa bidhaa kama Nguo, viatu, vipodozi, second hand cars, electronics zikiingizwa kwa wingi .Dar/Kariakoo imegeuka Dubai ya East Africa kwa maana ya bidhaa hizi kuingizwa kwa wingi na kuja kuuzwa kwa watanzania na hata wafanyabiashara wa Kenya, DRC, Zambia, Malawi, Uganda, Comorros etc.
  China ilipitia a bitter experience kufikia walipo.Wakati wa Mao from the early 1950s onwards there was quest for rapid industrialisation and arms accumulation, in order to force-march China into becoming a "superpower". Contrast with Tanzania during the Ujamaa era where leaders were just busy indoctrinating the citizens with such idealology that did not as much force people to work hard as was the case with China.

  Consider that "The Great Leap" of China (1958-61) combined demands for impossible levels of agricultural production, huge forced-labour projects like dams and canals, and of course the infamous and useless back-yard steel production.Im not by any standards supporting Mao's ideaology nor his strategies..but I think there are some lessons to be extracted therein.Tanzanians are coming from a background of laxity and inaction, they never tested bitter experiences which would then propel them into agressive quest for better lives.

  Watanzania "hawaijui shida" wamekuwa kwenye "comfort zone" muda wote....haijalishi kama hiyo comfort zone ni slam au chumba kimoja kinachokaliwa na familia ya watu 10 , choo passport size, mlo mmoja kwa siku....maji ni ya madimbwi na umeme ni ndoto!!
   
Loading...