Kutumia marehemu kisiasa ni zaidi ya kufilisika kisiasa

Kukumbatia maiti ili kutaka kujua ukweli wa kilichotokea sio siasa, wala cdm hawahitaji kufanya hivyo ili kujijenga kivyovyote kwani tayari wako mioyoni mwa watanzania.. kama hujui hilo endelea kuutesa moyo wako!

hivi kama serikali ya ccm imeua wezi.. kuna ulazima gani wa wao kukimbilia kutaka kuzika miili ya marehemu na kutaka kutoa m3 kama ni wezi? kuna vitu vingine tuwekeni ushabiki kando na tujadili sisi kama watanzania kwa sababu hao waliouliwa ni watz wenzetu,
 
mkuu nadhani kwa ufaham wangu kinachoonekana hapa ni ushabiki wa kisiasa zaidi ya kile kilichotokea maana waliouwawa inasemekana ni majambazi na kama ni majambazi hakukuwa na haja yoyote ya serkali kutoa ubani na kwenda kuwazika marehem kuna nini hapo kinachofichwa ambacho watu hawakijui
 
Umeona yaliyomtokea Mukama huko.Ni harakati za kuutetea UMMA wa wanzania ambao kila kukicha wanauawa watendaji wa Serikali hii na Viongozi WAKUU wananyamaza
 
Nnauye Jr,
Mkuu kuwepo kwako hapa JF tunategemea unakuja na vigongo vinavyotuhabarisha maswala muhimu ya chama ktk utekelezaji wa sera na ilani zake. Hizi habari za mazishi na katuni zinahusu nini ikiwa hili ni swala na haki ya msanii ambaye sii lazima awe mshabiki wa chama chochote cha kisiasa. Picha hueleza sawa na maneno milioni hivyo hatuwezi chukua lako tukaacha ukweli mwingine ulojitokeza ktk picha hiyo..

Tupe vigongo mkuu wangu, pengine wananchi watarudisha imani zao kwa chama..

Huyu ndiye msemaji wa Chama tawala! For heavens sake, hii kazi bora apewe Willy frm New York. Anyway, anawakilisha chama chake na inaonyesha chama kina watu wa aina gani. Hata kwenye mambo ya msingi wao wana-smile.
 
Mkuu kule kugumu na hoja ni nzito na hana majibu ya haraka ndo maana hawezi kurejea kule may be anaandaa hoja

Nnauye Jr. naona leo anapima upepo JF kwa hoja fupifupi zisizo na mashiko, I guess atakuwa ana-test mtandao aliofungiwa kwenye ofisi yake kama unafanya kazi. Naona on road politics zimeanza kumkatisha tamaa, baada ya kuona watu hawako upande wao.

Nafikiri anatakiwa kujifunza kuwa, ni busara sana kwa CCM kukaa kimya wakati huu na kutekeleza yale iliyoyaahidi ili by 2015 iwe na hoja zenye kuonesha vitu. Kampeni za kufanyia pembeni ya mapipa ya lami, au mabwawa ya maji na majengo hazisaidii kitu watu wanataka pocket issue kama ajira kuwa na ajira za uhakika, siyo ajira za polisi 20,000 huo ni utoto katika kuendesha nchi.

Fupa alilolishindwa Makamba na Tambwe Hiza Nnauye hataliweza, ila as time goes atakuwa anajishusha mpaka kuwa dissolved kwenye lindi ya ufisadi na yeye. Nnauye is a talented politician but alifanya makosa sana kukubali nafasi ya kuwa msemaji, alitakiwa kuwa kwenye strategic positions badala ya frontlines, maana ana hasira, akiwa probed analipuka na kujikuta anaharibu kama pale alipoambiwa alitaka kujiunga CDM na hii ya CCJ imemnyong'onyeza kabisa!. Bora sisi tusio na ushabiki wa vyama bali ni ushabiki wa Tanzania yenye demokrasia iliyo pevuka na kuepuka ubabaishaji.
 
Nnauye Jr,
Kwa kweli inashangaza Katibu Uenezi wa CCM kuja na hoja ya kikatuni (naamini mwenye akaunti ni Nape Moses Nnauye)! Sioni ukija na mikakati ya ki-chama kuzungumzia 'mtakavyoibana' serikali yenu ya CCM katika masuala kama
  • Kutumia kodi vizuri kwa masuala kama afya, elimu, miundo mbinu ya usafiri kuanzia serikali za mitaa mpaka serikali kuu.
  • ufumbuzi wa haraka wa mgao wa umeme
  • mafanikio ya kupiga vita rushwa
  • utekelezaji wa ahadi mlizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa udiwani, ubunge na Urais
  • sera za mambo ya shirikisho la Afrika Mashariki
  • n.k
 
Mbona mnapoteza maana, jadilini hoja iliyo kwenye board. Kama unaona haina mshiko unapitiliza.
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?
Hicho kikatuni umekiona wapi? Usije ikawa umekuja na stori za pauka pakawa. Nibe link, anyway tuachane na hicho kikatuni naamini lengo lako lilikuwa kuuliza mass je ni sawa marehemu kutumika kama mtaji wa kisiasa?

Ukweli ni kuwa si vema kabisa lakini inapobidi kuonyesha uonevu wa serikali isiyojali vilio vya wananchi inabidi watu kwenda kuwaelimisha wananchi bila kuogopa nini kitasemwa?

CDM wasingekwenda kule ile issue ingekuwa handled kimafia sana lakini saizi imepoa kwa hofu kuwa tukifanya fyongo tena tunazidi kujibebesha gunia la misumari na kichwani tuna kipara. Poleni CCM najua hamkutegemea hali hiyo lakini huo ndiyo ukweli.
 
huu ni mtizamo wake na hapa ina maana kuwa anawadhihaki wakuryya!! haha!(kicheko cha dhihaka kidogo)
huyu asije akatia mkuu kule kwetu mara abaki dsm tu , akija kule tutamuonyesha jinsi ya kuongea na watu vizuri , simtishi
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?
Nape,

Wewe hupaswi kuleta hoja za aina hii kwenye hili jamvi. Wewe unapaswa kuleta hoja zenye mashiko, hizi za udaku waachie kina MS na akina Majimulshindo.

Belive me, kwa hoja za aina hii nobody will take you seriously.
 
CCM walijaribu kumtumia Marehemu Chacha Wangwe kama mtaji wao wa Kisiasa kuichafua CDM lakini waliangukia Pua. Pia wengine kama Mtikila waliishia kutoka na ngeu kichwani. Kwenye hili la Nyamongo hakuna anayetumia marehemu kisiasa,Serikali imeua raia wake na raia na chama chao chenye kujali watu wamechukia.

05_11_77emjc.jpg

President Jakaya Kikwete consoles the widow of the late Sheikh Yahya Hussein, at her home in Magomeni Mwembe Chai on Sunday. The renowned astrologer passed away on Friday. (Photo by Muhidin Issa Michuzi)
 
Huyu ndiye msemaji wa Chama tawala! For heavens sake, hii kazi bora apewe Willy frm New York. Anyway, anawakilisha chama chake na inaonyesha chama kina watu wa aina gani. Hata kwenye mambo ya msingi wao wana-smile.

Mkuu hapo kwenye RED ni William @ New york
 
05_11_77emjc.jpg

President Jakaya Kikwete consoles the widow of the late Sheikh Yahya Hussein, at her home in Magomeni Mwembe Chai on Sunday. The renowned astrologer passed away on Friday. (Photo by Muhidin Issa Michuzi)
Mkuu unakusudia kumwambia nini Nape kupitia hii picha ?
 
Nnauye Jr. naona leo anapima upepo JF kwa hoja fupifupi zisizo na mashiko, I guess atakuwa ana-test mtandao aliofungiwa kwenye ofisi yake kama unafanya kazi. Naona on road politics zimeanza kumkatisha tamaa, baada ya kuona watu hawako upande wao.

Nafikiri anatakiwa kujifunza kuwa, ni busara sana kwa CCM kukaa kimya wakati huu na kutekeleza yale iliyoyaahidi ili by 2015 iwe na hoja zenye kuonesha vitu. Kampeni za kufanyia pembeni ya mapipa ya lami, au mabwawa ya maji na majengo hazisaidii kitu watu wanataka pocket issue kama ajira kuwa na ajira za uhakika, siyo ajira za polisi 20,000 huo ni utoto katika kuendesha nchi.

Fupa alilolishindwa Makamba na Tambwe Hiza Nnauye hataliweza, ila as time goes atakuwa anajishusha mpaka kuwa dissolved kwenye lindi ya ufisadi na yeye. Nnauye is a talented politician but alifanya makosa sana kukubali nafasi ya kuwa msemaji, alitakiwa kuwa kwenye strategic positions badala ya frontlines, maana ana hasira, akiwa probed analipuka na kujikuta anaharibu kama pale alipoambiwa alitaka kujiunga CDM na hii ya CCJ imemnyong'onyeza kabisa!. Bora sisi tusio na ushabiki wa vyama bali ni ushabiki wa Tanzania yenye demokrasia iliyo pevuka na kuepuka ubabaishaji.

Sasa mkuu badala ya kuutumia kutangaza sera za chama anaingia JF
Kwa kweli anahitaji aje na majibu mazito kwa hoja nzito sio majibu mepesi kwa hoja nzito
 
05_11_77emjc.jpg

President Jakaya Kikwete consoles the widow of the late Sheikh Yahya Hussein, at her home in Magomeni Mwembe Chai on Sunday. The renowned astrologer passed away on Friday. (Photo by Muhidin Issa Michuzi)

Sasa Mkuu hii picha una maana gani kuiweka kwenye post hii
 
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaambia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?
mkuu heshima yako
nimeshtuka kuona post yako hiyo ambayo imekaa "ki-facebook facebook" jaribu kuitambua hadhi na heshima yako katika chama chako, unapaswa kupost hoja nzito kama nini sasa chama kinaendelea kufanya katika kurudisha hadhi na imani ambayo imepotea miongoni mwa watanzania, au kupitia hoja mbalimbali humu ambazo zinahitaji majibu,acha taarabu, najua wewe unaweza kuifanya kazi hii vyema kwani wewe ni kizazi cha dot com tofauti na wazee waliojaa ccm ambao wanaiona JF kama tishio kwao. kama una masikio na usikie au endeleza taarabu nawe utapotea kama makamba, mapuri na tambwe hiza walivyopotea.
 
Back
Top Bottom