Kutuhumiwa kwa kosa la kimaadili haitoshi kumwondolea mtu sifa ya uongozi?


K

kwitega

Senior Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
166
Points
0
K

kwitega

Senior Member
Joined Apr 10, 2012
166 0
Ndugu zangu;

Bado miaka mitatu tuingie kwenye uchaguzi Mkuu mwingine yaani 2015. Naomba tusaidiane kwa hili jambo. Hivi kiongozi wa kisiasa akituhumiwa kwa kosa fulani la kimaadili; akiomba kwa hiari yake kuachia ngazi, ni heshima kwake au ni kukiri kwake kushiriki kwenye kosa husika? Je, mwanasiasa ambaye uadirifu wake ulishakuwa na doa la kimaadili pamoja na kwamba hakufikishwa mahakamani, haitoshi kumwondolea sifa ya nafasi anayoitaka? Kama kiongozi wa aina hii alianguka kimaadili kwa nafasi ndogo aliyokuwa nayo, je, akipewa nafasi kubwa zaidi, Taifa litabaki salama? Naleta hoja hii kwa makusudi kwani kwa sasa wapo wanasiasa wa aina niliyotaja hapo juu ambao wanataka urahis 2015. Wanatumia hata njia za hovyo kwa kuwachafua na kuwatukana wenzao kwenye chama chao. Karibuni!
 

Forum statistics

Threads 1,295,830
Members 498,404
Posts 31,224,539
Top