Kutongoza sasa hivi ni kama kupush mlevi tu

Kutongoza sasa hivi ni kama kupush mlevi tu

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Zamani bana kulikuwa hamna simu wala nini, nilikuwaga naogopa kutongoza mno nikikutana na binti nimpendae roho itanidunda weee kama nataka kupigwa risasi hata kusema nashindwa naishia kupiga porojo tu! Au tulikuwa tukiandika barua enzi hizo:

Salamu sana kwako dada mpendwa, Mara ooh nakupenda kama sukari, nikinywa maji nakuona kwenye kikombe.
Halafu mwisho unamalizia naomba jibu!

Haaahaaa zamani bana.

Siku hizi simple mnakutana kwenye sherehe au msibani au kwenye daladala unaomba tu namba ya simu, ukishafika home tu unamtext nimekupenda na mchezo kwisha mnapanga na siku ya kuonana kugegedana!

Duuuh jamani!

Natamani iwe kama zamani
 
Kuna ambao hatufanyi hivyo kwenye simu ,japo simu zimerahisisha sana ikiwemo hata namna ya kupanga appointment ya uhakika zamani mtu ulikuwa unaweza kuchomeshwa mahindi kwenye kichaka mpaka majogoo na asitokee mtu.
 
digital hii kila kitu kimerahisishwa mkuu. Yako mambo meng ya kufanya ukikaa zaid ya lisaa unajinad kwa dada utafanya lin mambo mengne? Dk 10 znatosha tu
 
Upande wa simu, nafikiri ndo dhana ya technology, kumrahisishia mtu kazi zake.
 
Enzi hizo za ujana wangu nishamsababisha binti kupukutisha karibia nusu ya majani ya kijimti fulani cha maua kitenge upenuni mwa nyumba yetu..

Yaani pamoja na tongozo hilo la takribani dk 45 lakini bado hakikueleweka!!!

Kuna mtindo ulikuwa unaitwa ngwara AKA mtama ulitumika sana vichakani
 
 
Last edited by a moderator:
siku hizi binti ukimwomba namba tu anajua unachotaka ukifika nyumbani ashaanza kukutext et umefika salama wangu Hapo unabaki kuandaa ratiba ya kumgegeda michepuko haiwezi isha
 
Demu ukimtongoza kwenye simu unamuogopa
Simu inatumika tu kupanga appointment
 
Enzi hizo za ujana wangu nishamsababisha binti kupukutisha karibia nusu ya majani ya kijimti fulani cha maua kitenge upenuni mwa nyumba yetu..

Yaani pamoja na tongozo hilo la takribani dk 45 lakini bado hakikueleweka!!!

ha ha ha.....
niliwahi kumtongoza Aneth kwa saa 4. ila mimi kilieleweka.
 
Naona wazee champions league mnakumbushana...
 
Back
Top Bottom