Kutongoza ni kipaji jamani

Kutongoza ni kipaji jamani

Pen pal...school debates...long live those days!!!
 
Kwa habari zaidi, wakati huo binti hawezi kujibu barua yako ila unaletewa na rafiki yake kitambaa cha mkono alichokifuma na huo moyo wenye mkuki utakuwepo tu kwa sababu ndiyo fasheni, hiyo ni confirmation kwamba umekubaliwa. Lakini bado tatizo lipo pale pale ukishakubaliwa, utaanzaje kuomba mwende ku-nanihii? Hiyo pia ni kazi, pili mtaenda wapi? sana sana mnaishia kwenda "snake lodge" na rafiki yake anaranda randa kulinda usalama, hapo ikitokea ameona watu wanaelekea pande hizo atamwita shoga yake kumwambia kuna watu wanakuja, duh hapo mzee ujue kama mlikuwa hamjaanza ndiyo imetoka hiyo, anatoka mbio na hujui lini tena itatokea hiyo chance. mbona ilikuwa kazii.
 
Hahahaa Mkuu haya mambo yalikuwa na ladha tofauti sana, mi nshawahi kumsubiri binti mmoja zaidi ya masaa sita hakutokea, tena ilikuwa siku ya sabato, si unajua watoto wa kisabato ndo huwa wanapata ruhusa ya kwenda kutembea!!!!!!!! yaani kila ukisikia vishindo ushageuka halafu mwisho wa siku hakutokea, siku nlipokutana nae kumuuliza akaniambia hakujiskia tu kuja dah, acha tu.....

Mkuu yalinikuta lakini mwenzio nilikomaa nae tu mtoto wa kisabato,kumsindikiza kanisani na kumsubiri mpaka atoke haikuwa taabu kwangu, kuhudhuria makambi mwanzo wake mpaka wanapoyavunja, nipo tu. mwisho wa yote kaingia laini ikawa anakacha hata hayo makambi na hivi sasa ni wangu wa nyumbani baada ya ndoa ya kiislamu. ni upendo wa kweli kweli uliokuwepo.
 
Mie nakumbuka nimehudhuria sana mikesha ya Christmas naishia kuChunga Lindo hata style ya Kula Povu la mdomoni ilikua haijaanza! No body can Undue the time!
 
memory ya mbali sana, mi mara ya kwanza kuandikiwa letter si nikamkataa jamaa, alikuwa student mwenzangu. akadai atajiua, acha niogope nikajua napata murder case. ilibidi nimwambie mama
pia nakumbuka jamaa mwingine alivyokuwa napita mbele ya nyumba yetu hata mara 10 kwa siku ili nimuone nitoke nje. funguo ya posta nilikuwa nashika mwenyewe ili kaka zangu wasifungue box wakakutana na barua yangu.. those old good days
 
ya kumuacha mwanaume je
"nilikupenda sana lakini mapenzi yameisha, kuanzia leo sikutaki tena, nimeshapata mwingine ninayempenda zaidi yako..... duh mengine sikumbuki...
nakumbuka niliandika hivyo chini ya usimamizi wa mpenzi mpya, ananiambia maneno ya kuandika... wacha mtalaka anilaani kwenye majibu yake, akasema anawish na mimi huyo niliyempata aje anitende kama nilivyomtenda yeye.. mmh wkt huo ulikuwa unaona kama mapenzi yanauma
 
Back
Top Bottom